http://wepesimedia.blogspot.com/p/blog-page.html

post-feature-image

Wema, Huddah Waingilia Ugomvi wa Zari, Hamisa


TANGAZA NASISI KWA BEI NAFUU NA UPATE MATOKEO MAZURI KATIKA BIASHARA YAKO.

Wema Sepetu Wakati kitendawili cha nani ni baba wa mtoto wa pili wa mwanamitindo Hamisa Mobeto kikiteguliwa baada ya mwenyewe kukiri hadhara...

Stereo ataja mambo yanayowaponza wasanii wa hip hop,soma hapa kuyafahamu..
Hivi ndivyo Chidi Benz alivyo fafanua kauli yake ya kusema hakuna rapa wa Bongo aliyefikia mafanikio yake
Video,Mubenga atangaza rasmi kujitoa PKP ya Ommy Dimpoz na kuanzisha lebo yake ya BANGERZ.


Wema Sepetu

Wakati kitendawili cha nani ni baba wa mtoto wa pili wa mwanamitindo Hamisa Mobeto kikiteguliwa baada ya mwenyewe kukiri hadharani jana, wasichana wawili ambao waliwahi kutoka kimapenzi na baba wa mtoto huyo, Wema Sepetu na Huddah Monroe wamejitokeza na kuingilia ugomvi kati ya Zarinah Hassan ‘Zari’ na Hamisa Mobeto.



Kwa muda mrefu kumekuwa na tetesi kuwa mtoto huyo wa Hamisa aliyepewa jina la Abdulatif Nasibu Abdul ni wa msanii mmoja mkubwa wa muziki wa kizazi kipya, ingawa kwa muda alikuwa akikanusha. Lakini jana, akihojiwa na kituo kimoja cha redio jijini, msanii huyo ambaye pia amezaa watoto wawili na Zari, alikiri kushiriki mapenzi na mwanamitindo huyo na kwamba amekuwa pia akimhudumia kwa kumpa kiasi cha shilingi laki tano kwa wiki, sambamba na kumnunulia gari.


Huddah Monroe

Msanii huyo alisema baada ya kuelezwa na kuukubali ujauzito huo, alimtaka mpenziwe huyo kukaa kimya kwani yeye tayari alikuwa kwenye uhusiano na Zari na hakuwa tayari kuachana na mwanamke huyo aliyemzalia watoto wawili.



Kivumbi kiliibuka upya mwishoni mwa wiki iliyopita, baada ya Hamisa kuvujisha picha alizozipiga kwa siri, akiwa na msanii huyo wa Bongo Fleva, wakiwa kitandani kimahaba, picha ambazo ziliamsha upya gumzo kubwa kwenye mitandao ya kijamii, wengi wakimtuhumu msanii huyo kwa kumkana mwanaye wakati ushahidi wote upo wazi.



Ni kelele hizo ndizo zilizomlazimu msanii huyo wa Bongo Fleva kupitia kituo kimoja cha runinga na redio, jana kuibuka na kutoa ufafanuzi wa kina kuhusu picha zilizovujishwa na Hamisa, ambapo alitumia fursa hiyo kukiri hadharani kwamba yeye ndiye baba wa mtoto huyo.



“Tulikubaliana na Hamisa Mobeto kuwa ujauzito huo usitangazwe kuwa ni wa kwangu, na alikubali,” alinukuliwa msanii huyo. Inadaiwa mwanamitindo huyo hakukubaliana na suala la kufanya mambo yote kuwa siri, hivyo akawa anavujisha taarifa kwa mashosti zake ambao nao walikuwa wakiposti kwenye mitandao ya kijamii, jambo linalotajwa kumtibua msanii huyo na kusababisha apunguze fedha za matumizi mpaka shilingi laki mbili (200,000) kwa mwezi. Hatua ya kupunguziwa matumizi, inatajwa kuwa ilimkasirisha zaidi Hamisa ambaye aliamua kuposti picha zilizowaonesha wakiwa kitandani, ambazo zilichafua hali ya hewa.



Wakati mahojiano hayo yakiendelea redioni, wadau mbalimbali walijitokeza kuzungumzia hali hiyo, lakini wakigawanyika, wengine wakimuunga mkono Hamisa na wengine Zari. Wema Sepetu ambaye uhusiano wake na msanii huyo ulikuwa ndiyo habari ya mjini wakati huo, kupitia akaunti yake ya mtandao wa Instagram, akionekana kumuunga mkono Zari, alisema anatambua wakati mgumu anaoupitia mwanamke huyo aliyempora bwana, katika kipindi hiki kigumu.



“Najua anaweza kusema maneno ya ovyo juu yangu, lakini najua hali anayopitia kama mwanamke, nadhani sasa ni wakati muafaka kwake kuweza kumvisha pete, mnyonge mnyongeni lakini haki yake mpeni,” aliandika Wema. Huddah Monroe, mwanamitindo kutoka Kenya ambaye naye pia aliwahi kuhusishwa kushiriki mapenzi na msanii huyo, katika namna ya kumpiga kijembe Zari, alisema ‘mwanaume ni wako anapokuwa ndani kwako, akitoka siyo wako’.


Name

BIASHARA NA UCHUMI BREAKING NEWS BURUDANI ENGLISH NEWS GOSIIP GOSPEL HABARI HABARI PICHA MAGAZETI MAKALA MATUKIO MICHEZO MUSIC VIDEO WAZO LANGU
false
ltr
item
WEPESI MEDIA : Wema, Huddah Waingilia Ugomvi wa Zari, Hamisa
Wema, Huddah Waingilia Ugomvi wa Zari, Hamisa
https://globalpublishers.co.tz/wp-content/uploads/2017/09/zari-and-hamisa-mobeto.jpg
WEPESI MEDIA
https://wepesimedia.blogspot.com/2017/09/wema-huddah-waingilia-ugomvi-wa-zari.html
https://wepesimedia.blogspot.com/
http://wepesimedia.blogspot.com/
http://wepesimedia.blogspot.com/2017/09/wema-huddah-waingilia-ugomvi-wa-zari.html
true
925270315725722404
UTF-8
Not found any posts VIEW ALL Readmore Reply Cancel reply Delete By Home PAGES POSTS View All

USIPITWE NA HIZI HAPA CHINI LABEL ARCHIVE SEARCH ALL POSTS Not found any post match with your request Back Home Sunday Monday Tuesday Wednesday Thursday Friday Saturday Sun Mon Tue Wed Thu Fri Sat January February March April May June July August September October November December Jan Feb Mar Apr May Jun Jul Aug Sep Oct Nov Dec just now 1 minute ago $$1$$ minutes ago 1 hour ago $$1$$ hours ago Yesterday $$1$$ days ago $$1$$ weeks ago more than 5 weeks ago Followers Follow THIS CONTENT IS PREMIUM Please share to unlock Copy All Code Select All Code All codes were copied to your clipboard Can not copy the codes / texts, please press [CTRL]+[C] (or CMD+C with Mac) to copy