Msanii wa rap Tanzania,Darassa amefunguka na kusema kuwa video yake ya wimbo wa Too Much ndio video ambayo imemtesa zaidi kwenye kuifanya...
Msanii wa rap Tanzania,Darassa amefunguka na kusema kuwa video yake ya wimbo wa Too Much ndio video ambayo imemtesa zaidi kwenye kuifanya.
Akiongea kwenye kipindi cha funiko Base cha radio 5,Darassa amesema imemgharimu muda mwingi na pesa nyingi kuikamilisha video hiyo kwani alitaka kufanya kitu kikibwa kwenye uwanja wa nyumbani.
“Too Much kwangu ni video kubwa na imetu cost,imetuchukua muda,imetuumiza hapa ninavyoongea hakuna tulichobakiwa nacho zaidi ya nguvu na akili tu.Tulichokuwa tunataka ni kuhakikisha tunatengeneza video nzuri nyumbani hata tukifanikiwa kimataifa watu wajue jamaa ameendelea tu ila alianzia nyumbani ndio tunachopambania,watu wa nje wahitaji kufanya kazi na sisi” alifunguka Darassa.