Halmashauri ya jiji la Arusha imeendelea kung'ara kwa kupeleka wanafunzi 578 kidato cha tano toka katika shule zake 23 za sekondari. ...
Halmashauri ya jiji la Arusha imeendelea kung'ara kwa kupeleka wanafunzi 578 kidato cha tano toka katika shule zake 23 za sekondari.
Baadhi ya wazazi Jijini humo wameendelea kuishukuru serikali ya awamu ya tano kwa kuendelea kuhakikisha elimu bora inatolewa kwa watoto wao.
"Kwakweli tunamshukuru sana rais John Magufuli kwa elimu bure na pia tunamshukuru kwa wateule wake mkuu wa mkoa Mhe Gambo, DC Daqqaro na zaidi Mkurugenzi wa jiji Athumani Kihamia kwa kua karibu na walimu na kamati za shule katika kuhakikisha wanatatua changamoto za walimu ili kuwapa motisha wafundishe watoto wetu vizuri" alinukuliwa Johari Lyimo mzazi wa mwanafunzi toka shule ya Sekondari Kaloleni.
Akizungumza kwa njia ya simu mkurugenzi wa Jiji Ndg Kihamia amewataka walimu kutokubweteka kwa matokeo hayo bali waendelee kuongeza bidii ili uwekezaji unaofanywa na serikali uakisiwe katika ufaulu wa watoto, na ameendelea kuwataka wazazi na walezi waendelee kutoa ushirikiano kwa walimu na serikali ili kusukuma mbele gurudumu la elimu nchini.
Halmashauri ya Jiji la Arusha imekua inakabiliwa na changamoto nyingi katika sekta ya elimu, serikali ya awamu ya tano kupitia kwa mkurugenzi wa Jiji Athuman Kihamia imekua ikijitahidi kutia majawabu kwa changamoto mbalimbali ikiwa ni pamoja na kulipa madeni ya walimu kwa mapato ya ndani na kuongeza vyumba vya madarasa 147 kwa msingi na sekondari na ukarabati mkubwa wa vyumba 27 vya madarasa kwa kipindi cha miaka miwili na kuhakikisha kila shule ya sekondari ina maabara yenye vifaa vya kisasa.