Picha kwa mujibu wa mtandao Jamaa: Hello mrembo, samahani, una mpenzi? Binti: Hapana. Sina mpenzi. Jamaa: Kitabu cha Mwanzo 2: 1...
Jamaa: Hello mrembo, samahani,
una mpenzi?
Binti: Hapana. Sina mpenzi.
una mpenzi?
Binti: Hapana. Sina mpenzi.
Jamaa: Kitabu cha Mwanzo 2: 18
"Bwana Mungu akasema, Si vema huyo
mtu awe peke yake, nitamfanyia
msaidizi wa kufanana naye."
Binti: Lakini mimi sikupendi jamani.
Jamaa: Waraka wa kwanza wa Yohana
4:8 "Yeye asiyependa, hakumjua
Mungu, kwa maana Mungu ni upendo."
Binti: Mh! Mi ntajuaje kwamba na
wewe unamaanisha hayo maneno?
Jamaa: Injili ya Mathayo 12:34b
"Maana, kinywa cha mtu huyanena
yaujazayo moyo wake."
Binti: Jamani leo kazi. Mi ntajuaje
kwamba we ni mkweli na mwaminifu?
Jamaa: Injili ya Marko 13:31 "Mbingu
na nchi zitapita; lakini maneno yangu
hayatapita kamwe."
Binti: Wewe! Na kwanini umekuja
kwangu? Wasichana mbona wako wengi
tu!
Jamaa: Mithali 31:29 "Binti za watu
wengi wamefanya mema, Lakini wewe
umewapita wote."
Binti: We una mambo wewe! Sasa mimi
kwangu umependa kitu gani?
Jamaa: Wimbo Ulio Bora 4:7 "Mpenzi
wangu, u mzuri pia pia, Wala ndani
yako hamna ila."
Binti: Mh! Huo uongo, mbona mimi
hata sio mzuri kihivyo. Unaongeza
chumvi tu!
Jamaa: Mithali 31:30 "Upendeleo
hudanganya, na uzuri ni ubatili; Bali
mwanamke amchaye Bwana, ndiye
atakayesifiwa."
Binti: Nikisema nimekukubalia
itakuaje?
Jamaa: Mwanzo 2:24 " Kwa hiyo
mwanamume atamwacha baba yake na
mama yake naye ataambatana na
mkewe, nao watakuwa mwili mmoja."
Binti: Jamani we mkaka. Inakuaje
unajua maandiko kiasi hicho?
Jamaa: Yoshua 1:8 "Kitabu hiki cha
torati kisiondoke kinywani mwako, bali
yatafakari maneno yake mchana na
usiku, upate kuangalia kutenda
sawasawa na maneno yote
yaliyoandikwa humo; maana ndipo
utakapoifanikisha njia yako, kisha
ndipo utakapositawi sana."
Binti: Wowwww! Naona unampenda
sana Mungu.
Jamaa: Zaburi 34:8 "Onjeni mwone ya
kuwa Bwana yu mwema; Heri mtu yule
anayemtumaini."
Binti: Mh! Haya bwana. Basi nipe
muda nifikirie ombi lako.
Jamaa: Wafilipi 4:8 "Hatimaye, ndugu
zangu, mambo yo yote yaliyo ya kweli,
yo yote yaliyo ya staha, yo yote yaliyo
ya haki, yo yote yaliyo safi, yo yote
yenye kupendeza, yo yote yenye sifa
njema; ukiwapo wema wo wote, ikiwapo
sifa nzuri yo yote, yatafakarini
hayo."
Binti: Mh! Jamani wewe, haya,
nimekubali. Mpaka hapo nakupenda
tayari!!
JAMAA.
"Amina"