Mtandao wa kijamii wa WhatsApp upo mbioni kuongeza sehemu mpya kwa watumiaji wake itakayomuwezesha mtumiaji kuonesha eneo alipo kwa mud...
Mtandao wa kijamii wa WhatsApp upo mbioni kuongeza
sehemu mpya kwa watumiaji wake itakayomuwezesha mtumiaji kuonesha eneo
alipo kwa muda huo (Live Location) kwa watu atakaowasiliana nao kupitia
WhatsApp.
Haya ni maboresho ambayo mtandao huo umedhamilia
kuyafanya kwa mwaka huu ili kuendana sawa na programu nyingine kama
Snapchat, Facebook, iMessanger n.k .
Sehemu hiyo ya Live Location itakusaidia kuwaonesha
marafiki, ndugu na jamaa zako sehemu uliyopo kwa dakika 15, hadi masaa 8
kutokana na wewe mwenyewe unavyotaka, lakini pia unaweza kuibadilisha
kwa aidha uiweke Automatic au Manually kama ilivyo kwa mitandao mingine
pindi unapotuma kitu.
Kupitia blog ya WhatsApp wamesema kuwa sehemu hiyo itakuja kwa watumiaji wote wa Android na iOS.
Hivi ndivyo utakavyotumia Live Location Shairing kwenye programu yako.
1- Ingia sehemu ya kuchat kama kawaida chagua jina au
kundi unalotaka lijue sehemu uliyopo. Kisha bonyeza na chini ya jina
lake au jina la kundi utaona sehemu imeandikwa ‘Live Location Share’ na
utabonyeza hapo kuruhusu.

Kumbuka huduma hii bado haijaanza kufanya kazi na
ikishaanza kupatika itakupasa u-update simu yako ili uweze kuanza
kuitumia. WhatsApp wamesema sehemu hii itaanza kupatikana wiki chache
zijazo. Je, maboresho hayo ya WhatsApp yatafanya mitandao mingine kama
Snapchat kukosa watumiaji?