Kiukweli ni mmoja ya swali kutoka kwa watu wengi wakihoji endapo Adamu na Eva ndiyo walikuwa wanadamu wa kwanza na kujaliwa kuwa na watot...
Kiukweli ni mmoja ya swali kutoka kwa watu wengi wakihoji endapo Adamu na Eva ndiyo walikuwa wanadamu wa kwanza na kujaliwa kuwa na watoto wawili Kaini na Habili lakini baadaye Kaini akamuua nduguye Habili na kisha Mungu kumlaani Kaini kwa kitendo alichokifanya kwa ndugu yake. (Mwanzo 4:1-15).
Baadaye bilili ikaeleza Kaini akaenda nchi ya mbali nchi ya Nodi kisha akamjua mke wake na kujaliwa kuwa na motto Henoko.
SWALI LA WENGI
Je Kaini alitoa wapi mke aliyemuoa na kuzaa nae angali katika uso wa Dunia walikuwepo watu wanne kwa mujibu wa Biblia Adam, Eva, Kaini na Habili aliyeuwawa na nduguye?(Mwanzo 4:16-17)
JIBU
Kwa mujibu wa ufahamu wangu wa kusoma kitabu hiki cha Biblia na kutoka kwa watumishi wa Mungu.
Kwa kawaida enzi za kale kwa mababu zetu Adam, Musa na wengine wengi katika tamaduni zao za kipindi kile watu wakiesabiwa wanaesabiwa wanaume tu bila watoto na wanawake tukichukulia mfano wa idadi ya watu waliolishwa na Yesu jangwani kwa mikate 5 na samaki 2. Idadi ni wanaume 5 000 (Yohana 6:5-7.)
Ivyo Adam na Eva Walikuwa na watoto wakiume na wakike ila watoto wakike awakutajwa katika biblia ivyo Biblia imesema Kaini Akaka Nodi akamjua mke wake ikiwa na maana yakuwa wakakutana kimwili na mke wake na kisha kupata mtoto.

Kwa mtazamo wangu Kaini akwenda peke yake Nodi bali aliambatana na Mke wake ambaye biblia aijamtaja kuwa ni nani tukilinganisha na kuwa duniani akukuwa na mwanadamu yeyote zaidi yake na familia yake kisha kuanzisha nchi nyingine ya Henoko aliyelitaja kwa jina la mwanae wakwanza.
kwa mawazo yangu na ufamu wngu Kaini alimuoa ndugu yake wakike ambaye biblia aijawatambulisha kutokana na tamaduni zao
Asante sana kwa kusoma Naamini ukichanganya na uwelewa wako utapata majibu yakukutosheleza usiache kutembelea Ukurasa wangu wa Facebook,Twitter na Instagram kwajina la WEPESI MEDIA Na Youtube Wepesi Tv..www.wepesimedia.blogspot.com.
