Kila mtu huwa anaogopa kufeli katika kile anachokifanya.Kwa sababu hii kuna watu wengi sana ambao wameshindwa kupiga hatua katika maisa ya...
Hata hivyo kuna watu pia ambao kila wakati wanajikuta wanafeli na kushindwa kuendelea mbele kwenye maisha yao wka sababu huwa hawako tayari kutafakari na kutathmini mambo ya msingi ambayo yaliwafanya washidnwe kuendelea mbele katika kila ambacho wanataka kukifanya.
Katika kuchukunguza na kutafuta maarifa nimegundua kuwa kuna sababu tatu ambazo zinawafanya watu wafeli katika yale wanayoyafanya na ili ujihakikishie kutokufeli katika hatua ambazo zinafauata kwenye maisha yako unatakiwa uzijue sababu hizi na uanze kuzifanyia kazi haraka:
Moja ni kufeli kwa maono/ndoto:Hii huwa tunaiita ni sababu ya “Why” kwenye maisha ya mtu.Hii ni pale mtu anapofeli kwenye maisha kwa sababu ya kutojiwekea mwelekeo maalumu wa kwenye maisha yake.Kuna watu wengi sana wanafeli kwenye maisha yao sio kwa sababu hawana uwezo au hawana akili ya kuwawezesha kufanikiwa.bali ni kwa sababu wamekosa kujiwekea mwelekeo maalumu wa maisha yao kujua wanataka nini na wanaelekea wapi.Hata wewe unaposoma makala hii leo,inawezekana kabisa kinachokufanya usiweze kupiga hatua kwenye maisha yako ni kwa sababu bado haujajiwekea mwelekeo maalumu kuhusu maisha yako.Hii inasababisha mtu kujikuta kila siku unakuwa unaanza kitu kipya na haumalizii hadi mwisho kile cha zamani ambacho umekianza.
Njia bora ya kuepuka kutokuwa mmoja wa wale ambao wanafeli katika kiwango hiki ni kuhakikisha kuwa unajiwekea mpango maalumu na thabiti sana wa kujua na kuamua ni mwelekeo gani wa maisha yako umeamua kuuchukua kuanzia leo.Je,unao mpango maalumu kuhusu maisha yako?
Aina ya pili ya kufeli ni ile inaitwa “What”-Hii unatokana na kufeli kwa mbinu(Strategy).Hii inamaanisha unaweza kuwa unajua unachotaka na kule ambako unaelekea bali unashindwa kupata na kufanikiwa kwa sababu unakuwa umefeli katika mbinu fulani ambazo umezitumia.Kumbuka kuwa unapoweza kujua unachotaka ama unakotaka kwenda kwenye maisha,baada ya hapo uanweza kuchagua na kuamua mbinu gani uitumie ili ikuwezeshe kufika kule ambako unatakiwa kwenda.Mara nyingi wako watu wengi sana ambao wanajua kwa hakika kile ambacho wanakitafuta katika maisha yao ila wanashindwa kwa sababu wametumia njia amayo sio sahihi katika kukitafuta.
Mbinu rahisi ya kujikwamua hapa baada ya kugundua kosa lako katika eneo hili ni wewe sasa kuanza kutafuta njia mbalimbali za kufanya kile ambacho umekusudia kukikamilisha.Siku zote kumbuka kuwa kuna njia mbadala ya kufanya kile ambacho umekusudia.
Aina ya tatu ya kufeli ni kule kunakoitwa “How”-Au namna ya unavyofanya.Hii huwa inaitwa “Tactic Failure”.Hii inamaanisha kuwa unaweza kujua unachotaka kwenye maisha,unajua mbinu ya kuitumia lakini inapofika wakati wa kutekeleza unafanya kwa njia isiyo sahihi.Mara nyingi hii hutokana na watu kukosa umakini kwa kitu ambacho anakifanya na mbinu aliyoamua kuitumia.Hii ndio maana,mtu mmoja anaweza kuwa anatumia njia fulani na akafanikiwa na yule mwingine anaonekana anatumia njia ileile lakini anafeli.Mara nyingi ambacho kinatokea ni kuwa mtu yule anayefeli huwa la kushindwa kuzingatia kila kipengele cha mbinu ambayo ameamua kuitumia.
Hebu na wewe jaribu kufikiria kufeli kwako kulikotokea mara ya mwisho kulisababishwa na nini kati ya haya matatu?Kama hautajifanyia uchunguzi kujua kuwa ni jambo gani lilisababisha ukafeli basi itakuwa ngumu sana kwa wewe kuweza kuvuka na kuendelea kwenye hatua ambayo inafuata.
Nakutakia mafanikio mema na kushinda katika kila changamoto uliyonayo.
See You At The Top
@JoelNanauka