http://wepesimedia.blogspot.com/p/blog-page.html

post-feature-image

Ukweli kuhusu dua ya Albadiri katika dini ya Uislamu


TANGAZA NASISI KWA BEI NAFUU NA UPATE MATOKEO MAZURI KATIKA BIASHARA YAKO.

Hivi karibuni, kumeibuka harakati za kuomba dua iitwayo Albadiri kwa ajili ya kuwalaani waliompiga risasi Mbunge wa Jimbo la  Singida Ma...

TRA WAAGIZA MADUKA YALIYOFUNGWA YAFUNGULIWE
CHEMSHA BONGO UKIPATA WEWE NI ZAIDI YA.....
Utafiti: Sababu ya wanawake kupiga kelele wakati wa kujamiiana
Hivi karibuni, kumeibuka harakati za kuomba dua iitwayo Albadiri kwa ajili ya kuwalaani waliompiga risasi Mbunge wa Jimbo la  Singida Mashariki, Tundu Antipas Lissu.

Kabla ya kujikita katika maudhui hii, nichukue fursa hii na mimi kutoa pole  kwa yaliyompata na pia kwa familia yake na wale wote wanaomhusu. Kitendo cha kupigwa risasi binadamu yeyote yule hadharani kinapaswa kuchukiwa na kila mpenda amani.

Nikirudi katika hoja ya makala haya, wasiokuwa Waislamu na hata Waislamu wamekuwa wakisikia kisomo cha ‘Albadiri’ au wengine huiita ‘Alalbadiri’ na kwamba hutumika kumsomea mtu au watu waovu kama vile wezi, majambazi na wauaji, watu waliofanya dhulma fulani na mengineyo.

Niwajulishe wasomaji kwamba asili ya neno ‘Albadiri’  au ‘Ahlalbadiri’ ni maneno ya kiarabu Ahlul Badri. Ahlu ni  kitu au watu. Badri ni mahali karibu na mji wa Madina nchini Saudi Arabia ambapo vita vya kwanza kati ya Waarabu wa Kikureshi na Waislamu vilipiganwa na Waislamu wakashinda.

Jeshi la Waislamu lilikuwa na wapiganaji 313 na katika vita hivi wako waliouawa na wengine kujeruhiwa, lakini pia wako waliosalimika na kuishi miaka kadhaa baadae. Wote hao hujulikana kama Ahlul Badri yaani Maswahaba wa Mtume Muhammad (rehma na amani ziwe juu yake) ambao walipigana vita vya Badri. Hivyo tunaposema Ahl badr tunamaanisha wale watu walioipigana vita hii.

Asili ya dua ya Ahlul Badri
Asili ya dua iitwayo Ahlul Badri ni imani potofu kwamba kumuomba Mwenyezi Mungu kupitia majina ya masahaba waliopigana vita vya Badri ni kujikaribisha kwa Mwenyezi Mungu kwa kutaja majina ya watu hao wema.

Kitendo hiki huwa kinaitwa ‘Al-istighaatha’ yaani kumuomba Mwenyezi Mungu msaada, faraja au nusura. Kwa hiyo hicho kiitwacho Alabadri kimechukuliwa kama dua maalumu ya kumuomba Mwenyezi Mungu hasa mtu au watu wanapodhulumiwa.

Je, Albadiri inaruhusiwa  katika Uislamu?
Hakika kumuomba Mwenyezi Mungu msaada, faraja au nusura ni jambo ambalo siyo tu ni jambo lililoruhusiwa katika mafundisho ya Uislamu, bali ni jambo lililosisitizwa kwamba mtu au watu wanapofikwa na msiba au jambo kubwa basi wamuombe Mwenyezi Mungu awape faraja au alete nusura yake.

Hiyo ndiyo inayoitwa Al-istighaatha ya kisharia ambapo ni  kumuomba Mwenyezi Mungu peke yake pasipo kumshirikisha na chochote kile kama malaika, mitume au wachamungu.

Kwa hiyo, kumuomba kiumbe jambo ambalo hana uwezo nalo, kama kumuomba Mwenyezi Mungu awapatilize waliompiga risasi Lissu kupitia majina ya Ahlul Badri, ni kufanya kitendo cha uzushi katika dini ya Kiislamu na ushirikina wa wazi.

Katika Uislamu, wa kuombwa ni Mwenyezi Mungu peke yake kama alivyosema yeye mwenyewe katika Qur’an kwamba: “Na watakapokuuliza waja wangu kuhusu mimi, waambie niko karibu. Ninajibu maombi ya muombaji pale anaponiomba...” (Qur’an Sura ya Pili aya ya 186).

Istighaatha za kisharia ziko za aina kuu mbili, zinazoruhusiwa kisharia na zilizoharamishwa na kwa pamoja zimegawanyika katika aina tatu. Moja ni kuomba msaada kwa mwanadamu aliye hai katika lile ambalo ana uwezo nalo. Mfano ni pale Nabii Musa alipoombwa msaada na ndugu yake Muisraeli dhidi ya adui yake kama ilivyokuja katika Qur’an 28:15.

Al-istighaatha nyingine kumuomba Mwenyezi Mungu moja kwa moja ambako ndiko kunakohimizwa na Uislamu kama ilivyotajwa katika Qur’ana 8:9.

Al-istighaatha nyingine zote ni haramu kama vile kuwaomba viumbe katika jambo ambalo hawana uwezo nao wawe wako hai au wamekufa. Kwa mfano, kwenda kumuomba mtu akuokoe dhidi ya dhulma ulizofanyiwa au kuwaomba waliokufa au watu walioko makaburini.

Istighaatha za aina hii ni aina za ushirikina ambazo Waislamu na wanadamu wengine kwa ujumla wanapaswa kujiepusha nazo. Hizi ni itikadi za kishirikina ambazo zimeingizwa katika Uislamu na hivi leo zinaonekana kama ni  mafundisho ya Uislamu wakati ni uzushi tu watu kwa maslahi yao.

Miongoni mwa uzushi ulioenea sana ni hicho kiitwacho Alabadri au Ahlalbadri kiasi kwamba mtu akiaambiwa nitakusomea Albadiri basi huogopa sana na kwa kweli imechukuliwa kama  aina za uchawi wa Waislamu wakati huo ni ushirikina wa watu tu na wala sio jambo la kidini.

Nini kinaruhusiwa katika kuomba?
Kinachoruhusiwa ni kumuomba Mwenyezi Mungu moja kwa moja au kwa kutaja matendo mema ambayo muombaji ameyafanya katika kumtii Mwenyezi Mungu ili kuvuta huruma yake amsaidie au kumuokoa katika shida aliyonayo.

Aina ya kumuomba Mwenyezi Mungu kwa kutaja matendo mema aliyoyafanya mwanadamu inaitwa Tawassul. Tawassul inatokana na neno la Kiarabu Al-Wasiyla ambalo lina maana ya njia au nyenzo ya kufanyia jambo. Kwa hiyo matendo mema yanakuwa Wasiyla ya dua ya muombaji anapomuomba Mwenyezi Mungu.

Mfano mzuri ni kisa cha watu waliokimbilia katika pango na mlango wa hilo pango ukafunikwa na jiwe kubwa wasiweze kutoka. Hawa wakaona wamuombe Mwenyezi Mungu kwa kila mmoja kutaja mema yake aliyokuwa ameyatenda kuvuta huruma zake na kwa rehema zake jiwe likasogea pembeni wakafanikiwa kutoka.

Pengine hii ndiyo iliyochanganywa na watu wenye kusoma hicho kiitwacho kisomo cha Albadiri ambapo hutajwa majina ya maswahaba 313 na kisha kuombwa dua, kwani wanategemeza maombi yao kwa Mwenyezi Mungu kupitia hao Ahlul Badri ambao kama tulivyoona ni maswahaba au wanafunzi wa Mtume Muhammad waliopigana vita vya Badri.

Nasaha kwa Waislamu
Tunapenda kutoa nasaha kwa Waislamu wote kwamba wasijihusishe na hicho kinachoitwa kisomo cha Albadiri kuwasomea waliompiga risasi Lissu. Kufanya hivyo hakuwatoi katika wale wenye kumuonea huruma  Lissu, bali kunawatoa katika kufanya kitendo cha kumshirikisha Mwenyezi Mungu.

Ikiwa ni kumuombea,  wafanye hivyo kwa namna inayokubalika katika dini ya Uislamu na siyo njia hii ambayo Mtume wa Mwenyezi Mungu hakuifundisha.

Mwenyezi Mungu anasema katika Qur’an 5:35 kwamba: “Enyi mlioamini, muogopeni Allah na tafuteni Wasiyla (kwenda kwake) na fanyeni juhudi katika nia yake ili mpate kufaulu”.

Kingine ni kwamba Waislamu wanapaswa kujiepuesha na mwenendo wa kulaani. Likitokea jambo baadhi  kukimbilia kulaani. Tunapaswa kukumbuka kwamba Mtume wetu alitumwa kuwa rehema kwa walimwengu.

Mwenyezi Mungu anasema katika Qur’an 21:107 kwamba: “Na hatukukutuma (ewe Muhammad) isipokuwa uwe rehma kwa walimwengu”.

Ndiyo maana Mtume watu alipoombwa na mtu mmoja: “Ewe Mjumbe wa Allah walaani washirikina. Akasema “Hakika Allah hakunituma kuwa mwenye kulaumu wala kulaani, lakini amenituma kuwa mlinganiaji na rehma”.

Waislamu humuomba Mola wao tu na ikibidi kuwaombea watu waovu dua, Waislamu wema huwaombea watu waovu Mwenyezi Mungu awaongoe kwani wanafanya uovu au dhulma wanazozifanya kwa kutomjua Mwenyezi Mungu hivyo mwisho wa dhulma ni wao kuongoka.

Ikibidi kuomba dua dhidi ya uovu au dhulma zinazofanyiwa Waislamu na watu wengine kwa ujumla, kinachotakiwa ni kumuiga Mtume Muhammad pindi alipoomba dhidi ya wakuu wa Makureshi kwa kusema “Ewe Mola wangu, nakukabidhi fulani ...”.

Fundisho hapa ni kwamba Mtume hakupata kumuombea mtu yeyote mabaya bali alimuomba Mwenyezi Mungu amfanye mtu huyo kile ambacho yeye anaona kinafaa.

Name

BIASHARA NA UCHUMI BREAKING NEWS BURUDANI ENGLISH NEWS GOSIIP GOSPEL HABARI HABARI PICHA MAGAZETI MAKALA MATUKIO MICHEZO MUSIC VIDEO WAZO LANGU
false
ltr
item
WEPESI MEDIA : Ukweli kuhusu dua ya Albadiri katika dini ya Uislamu
Ukweli kuhusu dua ya Albadiri katika dini ya Uislamu
https://blogger.googleusercontent.com/img/b/R29vZ2xl/AVvXsEgfi1gsUjzdS3pPicQ2WA0ojv1D9fPZjEXcRxgUsb0A6XVO8GSjY18HO3Tx-FWZPtgNk3ZJNuCkDa4kMY9zWLpgnFjDlO6mEAO5VET4Z3LvWgZUYBhWyo3GOlQZa-lnh9cJN5FdsqWpB82f/s640/Blog-Post-The-power-of-dua-slider1-copy.jpg
https://blogger.googleusercontent.com/img/b/R29vZ2xl/AVvXsEgfi1gsUjzdS3pPicQ2WA0ojv1D9fPZjEXcRxgUsb0A6XVO8GSjY18HO3Tx-FWZPtgNk3ZJNuCkDa4kMY9zWLpgnFjDlO6mEAO5VET4Z3LvWgZUYBhWyo3GOlQZa-lnh9cJN5FdsqWpB82f/s72-c/Blog-Post-The-power-of-dua-slider1-copy.jpg
WEPESI MEDIA
https://wepesimedia.blogspot.com/2017/09/ukweli-kuhusu-dua-ya-albadiri-katika.html
https://wepesimedia.blogspot.com/
http://wepesimedia.blogspot.com/
http://wepesimedia.blogspot.com/2017/09/ukweli-kuhusu-dua-ya-albadiri-katika.html
true
925270315725722404
UTF-8
Not found any posts VIEW ALL Readmore Reply Cancel reply Delete By Home PAGES POSTS View All

USIPITWE NA HIZI HAPA CHINI LABEL ARCHIVE SEARCH ALL POSTS Not found any post match with your request Back Home Sunday Monday Tuesday Wednesday Thursday Friday Saturday Sun Mon Tue Wed Thu Fri Sat January February March April May June July August September October November December Jan Feb Mar Apr May Jun Jul Aug Sep Oct Nov Dec just now 1 minute ago $$1$$ minutes ago 1 hour ago $$1$$ hours ago Yesterday $$1$$ days ago $$1$$ weeks ago more than 5 weeks ago Followers Follow THIS CONTENT IS PREMIUM Please share to unlock Copy All Code Select All Code All codes were copied to your clipboard Can not copy the codes / texts, please press [CTRL]+[C] (or CMD+C with Mac) to copy