http://wepesimedia.blogspot.com/p/blog-page.html

HADITHI YA KUSISIMUA:- DALILI YA MVUA NI MAWINGU...!

Hii ni hadithi kuhusu kijana mmoja, aliyechagua msichana wa kumwoa, na kuzaa naye watoto, na kwa kali hiyo kuukuza ukoo wake. Lakini kabl...


Hii ni hadithi kuhusu kijana mmoja, aliyechagua msichana wa kumwoa, na kuzaa naye watoto, na kwa kali hiyo kuukuza ukoo wake. Lakini kabla ya mipango ya mwisho ya harusi na baba mkwe wake, aliamua awajaribu wakwe zake kwa mtihani mdogo.

Asubuhi moja, akaomba ruhusu kwa wake zake aende kijijini kwao akachukue vifaa vyake vya kulimia, na angeshukuru kama shemeji yake, dada wa atayekuwa mkewe atafuatana naye. "Umekuja hapa, kumtafuta mke utakayeishi naye, karibu tutakuwa ndugu, kwa hiyo shemeji yako akikubali, sisi hatuna kuzuizi," wakwe walimjibu.

Hivyo Kijana na shemeji yake wakaondoka, na walipofika kijijini kwake, badala ya kuchukua vifaa vya kilimo, akachukua mkuki, pamoja na shemeji yake, wakaenda kuwinda. Kijana akauwa mnyama mkubwa, wakaanza safari ya kurudi kijijini kwa wakwe zake. Shemeji yake akawa amebeba kitoweo huku kijana amebeba mkiku wake.

Njiani akamwambia shemeji yake, kuwa kuleta kitoweo nyumbani, ni njia mojawapo ya kuhakikisha uhodari na uwezo wa kuwatunza wakwe na familia yake. Wakapokewa kwa shangwe, kijana naye akapongezwa kwa uhodari wake.

Usiku huo huo, akawaeleza wakwe zake kwamba alitaka ajaribu tena jwenda kuwinda na vile vile akaomba ruhusu ya kufuatana na shemeji yake.
"Sasa tuko kama ndugu, sisi tunataka tukusaidie kwa kila njia tutavyoweza!" Baba mkwe akamwambia.

Hivyo, siku iliyofuata, wakaondoka tena na haikuchukua muda, kijana kwa uhodari wake, akauwa mnyama wapili. Mara hii mnyama aliyemwua alikuwa mkubwa na mzito kiasi kwamba, wote wawili walishindwa kumbeba. Uamuzi ukawa kwamba yule kijana, arudi kijijini kwenda kuomba msaada, na shemeji yake abakie kuchunga kitoweo. Kijana alipoondoka, yule msichana akapanda juu ya mti, kuhofia wanyama wakali, akisubiri msaada ufike.

Kijana alipofika kijijini akajitupa kwa kilio chini ya miguu ya mkewe wa mtarajiwa. Akisema kama amefanya kosa kubwa sana.
Badala ya kutupa mkuki kumchoma myama, sababu ya giza alimchoma dada yake ambaye sasa amemwacha amekufa porini.
Familia nzima wakajiwa na chuki na wakaanza kumtukana maneno mbali mbali, kusikia kisa hicho. Wakaanza kumpiga vile vile: " unawezaje kusema wewe ni mwindaji hodari, kutaka kutunza familia ikiwa umefanya upumbavu kama huu?" Walimpiga sana mpaka kidogo azirai. wakagundua kwamba wakiendelea kumpiga wanaweza kumuua na wasiweze kupata maiti ya msichana wao. Maana ni yule kijana peke yake alifahamu maiti ilipo. Wakamwamuru yule kijana ambaye alikuwa hai kwa mapigo, aongozane nao akawaonyeshe maiti ya msichana wao ilipo.

Walipofika, walistaajabu sana kumwona msichana wao akiteremka toka juu ya mti. Akishangaa na kuwauliza kwa nini yule kijana alikuwa katika hali mbaya hiyo huku ametapakaa damu. Familia nzima ilishindwa kusema cho chote kuhusu kitendo hicho kwa kuona aibu, Kwa maovu waliyomfanyia. Wakamwomba msamaha yule kijana. Wakasaidiana kumchukua yule mnyama na kumkata vipande. Wakavibeba hivyo vipande na kurudi kijijini. Walipofika tu, yule kijana akafungasha mizigo yake na kabla hajaondoka, akawaambia kuwa hataoa msichana kutoka kwenye familia ya watu wasiokuwa na huruma na wakorofi. Hivyo akafunga safari na kuondoka.

Haukupita muda, kwenye kijiji kingine alichohamia, akapata mchumba mwingine. Vile vile akawajaribu wakwe zake kama alivyofanya awali na mchumba wake wa kwanza. Safari hii mambo yakawa tofauti! Wakwe zake wapya, walishtuka na madhara yaliyotokea, akasamehewa kwa ajali iliyotokea na wakamwomba yule kijana akawaonyeshe sehemuu ambapo ajali ilitokea, ili wachukue maiti na kuja kuzika ipasavyo. Walipofika sehemu ya ajali ilipotokea wakamkuta shemeji yake, yaani msichana wao mzima kabisa amesimama kando ya mnyama aliyeuawa na mkwe wao.

Ikabidi yule kijana aeleze mkasa toka mwanzo mpaka mwisho, akatoa sababu za kufanya kitendo hicho. Na kamaliza kusema kwamba, sasa amepata mke aliyekuwa akimtafuta ambaye tabia yake pamoja na familia yake, ni ya watu adili. Akamuoa mchumba wake, wakaishi kwa muda kabla ya kuhamia kijijini kwa yule kijana na kuishi maisha yao yote
CHANZO:- HADITHI NA VISA KUTOKA TANZANIA

COMMENTS


TANGAZA NASISI KWA BEI NAFUU NA UPATE MATOKEO MAZURI KATIKA BIASHARA YAKO.

MAGAZETI$type=sticky$count=4


Name

BIASHARA NA UCHUMI BREAKING NEWS BURUDANI ENGLISH NEWS GOSIIP GOSPEL HABARI HABARI PICHA MAGAZETI MAKALA MATUKIO MICHEZO MUSIC VIDEO WAZO LANGU
false
ltr
item
WEPESI MEDIA : HADITHI YA KUSISIMUA:- DALILI YA MVUA NI MAWINGU...!
HADITHI YA KUSISIMUA:- DALILI YA MVUA NI MAWINGU...!
https://blogger.googleusercontent.com/img/b/R29vZ2xl/AVvXsEjkGUVy9saxG5AKilMfQGlWQNL95IODabGt9ONdev4zD9rnuqM3mxG3T7cAqyXini-Vj00RI-79b-lQfya8SwgSxEDQXCgc5ama1ffRpQTrObovIngHphl4mh7neCOZk4drB8kyny7-xdY/s640/1BT10339_0252.jpg
https://blogger.googleusercontent.com/img/b/R29vZ2xl/AVvXsEjkGUVy9saxG5AKilMfQGlWQNL95IODabGt9ONdev4zD9rnuqM3mxG3T7cAqyXini-Vj00RI-79b-lQfya8SwgSxEDQXCgc5ama1ffRpQTrObovIngHphl4mh7neCOZk4drB8kyny7-xdY/s72-c/1BT10339_0252.jpg
WEPESI MEDIA
https://wepesimedia.blogspot.com/2017/01/hadithi-ya-kusisimua-dalili-ya-mvua-ni.html
https://wepesimedia.blogspot.com/
http://wepesimedia.blogspot.com/
http://wepesimedia.blogspot.com/2017/01/hadithi-ya-kusisimua-dalili-ya-mvua-ni.html
true
925270315725722404
UTF-8
Not found any posts VIEW ALL Readmore Reply Cancel reply Delete By Home PAGES POSTS View All

USIPITWE NA HIZI HAPA CHINI LABEL ARCHIVE SEARCH ALL POSTS Not found any post match with your request Back Home Sunday Monday Tuesday Wednesday Thursday Friday Saturday Sun Mon Tue Wed Thu Fri Sat January February March April May June July August September October November December Jan Feb Mar Apr May Jun Jul Aug Sep Oct Nov Dec just now 1 minute ago $$1$$ minutes ago 1 hour ago $$1$$ hours ago Yesterday $$1$$ days ago $$1$$ weeks ago more than 5 weeks ago Followers Follow THIS CONTENT IS PREMIUM Please share to unlock Copy All Code Select All Code All codes were copied to your clipboard Can not copy the codes / texts, please press [CTRL]+[C] (or CMD+C with Mac) to copy