http://wepesimedia.blogspot.com/p/blog-page.html

post-feature-image

Gazeti la MAWIO waijibu serikali baada ya kutangaza kulifungia kwa Miaka Miwili


TANGAZA NASISI KWA BEI NAFUU NA UPATE MATOKEO MAZURI KATIKA BIASHARA YAKO.

Uongozi wa gazeti la MAWIO umeapa kwenda mahakamani kupinga uamuzi wa serikali kulifungia gazeti hilo kutochapishwa kwa kipindi cha miezi...

Mtalii mchina aua mwanamke Kenya
Sababu ya samaki kupungua Ziwa Tanganyika
Godbless Lema Amtumia Waraka Mzito Rais Magufuli

Uongozi wa gazeti la MAWIO umeapa kwenda mahakamani kupinga uamuzi wa serikali kulifungia gazeti hilo kutochapishwa kwa kipindi cha miezi 24.


Uamuzi wa kulifungia gazeti hilo ulitangazwa na serikali kupiti Wizara ya Habari, Utamaduni, Sanaa na Michezo ambapo sababu iliyotajwa ni gazeti hilo kukiuka maagizo ya serikali ya kutowahusisha marais wastaafu Mzee Mkapa na Dkt Kikwete katika ripoti za uchunguzi wa mchanga wa madini.


Mkurugenzi wa Kampuni ya Victoria Media Services Ltd ambaye pia ni Mhariri Mtendaji wa gazeti la MAWIO, Simon Martha Mkina, aliliambia The Citizen kuwa, amuzi huo si wa haki na utapingwa mahakamani.


“Bodi itakutakana kujadili uamuzi huo kama jambo la dharura, lakini tunachoweza kukwambia kwa sasa, tutakwenda mahakamani,” alisema Mkina.


Kwa mujibu wa taarifa ya Waziri Dkt Mwakyembe iliyotolewa na Idara ya Habari (MAELEZO), Waziri alinukuliwa akisema, “Sina budi kulifungia gazeti lako, na kukutaka usitishe kuchapisha nakala ngumu au ya mtandaoni katika kipindi cha muda wa miezi ishirini na nne (24) tangu tarehe ya barua hii, kwa mamlaka niliyopewa chini ya Sheria ya Huduma za Habari Na. 12 ya mwaka 2016 kifungu cha 59.”


Gazeti hilo liliandika habari iliyokuwa na ujumbe wa jumla kuwa, marais hao wamelisababishia taifa hasara kubwa sana kutokana na usafirishaji wa mchanga nje ya nchi kwa kipindi cha miaka 19.


Kwa mujibu wa mamlaka iliyonayo kupitia Sheria ya Magazeti ya mwaka 1976 sura ya 229 kifungu cha 25(1), Januari 15, 2016 Serikali ilitangaza kulifungia kwa muda wote gazeti la MAWIO lakini baada ya mwaka mmoja wa kukaa kifungoni lilirejea mtaani baada ya kushinda rufaa mahakamani.

Name

BIASHARA NA UCHUMI BREAKING NEWS BURUDANI ENGLISH NEWS GOSIIP GOSPEL HABARI HABARI PICHA MAGAZETI MAKALA MATUKIO MICHEZO MUSIC VIDEO WAZO LANGU
false
ltr
item
WEPESI MEDIA : Gazeti la MAWIO waijibu serikali baada ya kutangaza kulifungia kwa Miaka Miwili
Gazeti la MAWIO waijibu serikali baada ya kutangaza kulifungia kwa Miaka Miwili
https://blogger.googleusercontent.com/img/b/R29vZ2xl/AVvXsEixajwgLkrPJMWJHrvKQNttkC21EJzooajfnlJDoJ7K6dJgWGPM-PPPcittDqgR2IEjgHvEm6Tg9GCGzihg-fA6O9VT9p9lFM45wnmrIOgtzaAOqvMzoqVYpm6ylQH-RymMsoxGZq13TqdX/s640/1.jpg
https://blogger.googleusercontent.com/img/b/R29vZ2xl/AVvXsEixajwgLkrPJMWJHrvKQNttkC21EJzooajfnlJDoJ7K6dJgWGPM-PPPcittDqgR2IEjgHvEm6Tg9GCGzihg-fA6O9VT9p9lFM45wnmrIOgtzaAOqvMzoqVYpm6ylQH-RymMsoxGZq13TqdX/s72-c/1.jpg
WEPESI MEDIA
https://wepesimedia.blogspot.com/2017/06/gazeti-la-mawio-waijibu-serikali-baada.html
https://wepesimedia.blogspot.com/
http://wepesimedia.blogspot.com/
http://wepesimedia.blogspot.com/2017/06/gazeti-la-mawio-waijibu-serikali-baada.html
true
925270315725722404
UTF-8
Not found any posts VIEW ALL Readmore Reply Cancel reply Delete By Home PAGES POSTS View All

USIPITWE NA HIZI HAPA CHINI LABEL ARCHIVE SEARCH ALL POSTS Not found any post match with your request Back Home Sunday Monday Tuesday Wednesday Thursday Friday Saturday Sun Mon Tue Wed Thu Fri Sat January February March April May June July August September October November December Jan Feb Mar Apr May Jun Jul Aug Sep Oct Nov Dec just now 1 minute ago $$1$$ minutes ago 1 hour ago $$1$$ hours ago Yesterday $$1$$ days ago $$1$$ weeks ago more than 5 weeks ago Followers Follow THIS CONTENT IS PREMIUM Please share to unlock Copy All Code Select All Code All codes were copied to your clipboard Can not copy the codes / texts, please press [CTRL]+[C] (or CMD+C with Mac) to copy