http://wepesimedia.blogspot.com/p/blog-page.html

post-feature-image

Godbless Lema Amtumia Waraka Mzito Rais Magufuli


TANGAZA NASISI KWA BEI NAFUU NA UPATE MATOKEO MAZURI KATIKA BIASHARA YAKO.

Mbunge wa Arusha Mjini, Godbless Lema (Chadema), amemuandikia waraka Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania, Dkt. John Magufuli akimsi...

Maalim Seif Sharif Hamad Aitwa Polisi Kuhojiwa Seebait.com 2016
Nape Nnauye Ashindwa Kuhutubia Kwenye Tamasha la Muziki Jijini Mwanza Kutokana na Zomeazomea Ya Wananchi Wanaotaka Bunge Lionyeshwe Live
Profesa Anna Tibaijuka kitanzini Tena......Katuhumiwia Kujimilikisha Shamba la Hekari 4,000

Mbunge wa Arusha Mjini, Godbless Lema (Chadema), amemuandikia waraka Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania, Dkt. John Magufuli akimsihi kuruhusu kufanyika kwa mikutano ya kisiasa nchini bila kujali mipaka ya majimbo.

Lema amepaza sauti yake kupitia waraka wake kwa Rais Magufuli, uliosambazwa kwenye mitandao ya kijamii, waraka ambao alithibitisha kuwa ni wake.

Katika waraka huo, Lema ambaye pia na Mjumbe wa Kamati Kuu ya Chadema, alimsihi Rais Magufuli kuviruhusu vyama vya siasa kufanya mikutano hiyo kwani ni sehemu ya matakwa ya katiba.

Alitahadharisha kuwa endapo mambo yaliyoruhusiwa kikatiba hayataruhusiwa, ipo siku amri za utekelezaji wa masuala muhimu kikatiba hazitachukuliwa kwani hakutakuwa na sababu ya kuheshimu katiba na utawala wa sheria.

“Kama hatuwezi kufanya tunayoruhusiwa na Katiba, na anayetuzuia mamlaka yake yametokana na Katiba, hakika mbegu inayopandwa ni hatari kwa ustawi wa Taifa, ipo siku amri ya utekelezaji juu ya masuala muhimu haitachukuliwa kwa sababu umuhimu wa kuheshimu katiba na utawala wa Sheria hautakuwepo,” aliandika.

Lema alimueleza Rais Magufuli kuwa Siasa ni kazi kama zilivyo kazi nyingine na kwamba mfumo huo ndiyo chanzo cha madaraka waliyonayo hapa nchini.

“Mheshimiwa Rais, siasa ni kazi na ndiyo maana wewe ni rais kwa sababu ya siasa, na mimi ni mbunge kwa sababu ya siasa, tena ni kazi muhimu sana tu kwani ndio mfumo pekee unaotafuta utawala wa ngazi mbalimbali na wa juu kabisa katika nchi,”

Aidha, Lema alimsemea kwa Rais Magufuli ambaye ni Mwenyekitiwa CCM, Msemaji wa chama hicho, Christopher Ole Sendeka kwa kukiuka amri aliyoitoa Rais kwa kufanya mkutano Longido ambako sio jimbo lake.

“Mheshimiwa Rais, jambo hili litaleta mpasuko katika taifa letu, ni kauli inayopaswa kurekebishwa haraka. Hivi karibuni, msemaji wa CCM, Ole Sendeka alifanya mkutano Longido. Je, Ole Sendeka ni Mbunge wa Longido? Au polisi wa Mkoa wa Arusha hawakusikia tamko lake? "Alihoji.

Mbunge huyo alisisitiza kuwa Chadema itafanya maandamano Septemba Mosi mwaka huu, huku akihoji madhara yanayoweza kujitokeza siku hiyo, hivyo akamuomba Rais kutengua amri yake ya kuzuia mikutano ya hadhara

Name

BIASHARA NA UCHUMI BREAKING NEWS BURUDANI ENGLISH NEWS GOSIIP GOSPEL HABARI HABARI PICHA MAGAZETI MAKALA MATUKIO MICHEZO MUSIC VIDEO WAZO LANGU
false
ltr
item
WEPESI MEDIA : Godbless Lema Amtumia Waraka Mzito Rais Magufuli
Godbless Lema Amtumia Waraka Mzito Rais Magufuli
https://blogger.googleusercontent.com/img/b/R29vZ2xl/AVvXsEjiBZ6v9bCWWf6b_RlcaCpS-Wr2ji8qDwERm6bgbYOLEsPZxg_5V885dM1iT3ENZv4C5BTdkX_SpQe-wjedSXx1E1ochEHWbP6ifYiK9pq_j330hGVsp_baxGA9pEiy73pa-AXTC1wys9A/s1600/1.jpg
https://blogger.googleusercontent.com/img/b/R29vZ2xl/AVvXsEjiBZ6v9bCWWf6b_RlcaCpS-Wr2ji8qDwERm6bgbYOLEsPZxg_5V885dM1iT3ENZv4C5BTdkX_SpQe-wjedSXx1E1ochEHWbP6ifYiK9pq_j330hGVsp_baxGA9pEiy73pa-AXTC1wys9A/s72-c/1.jpg
WEPESI MEDIA
https://wepesimedia.blogspot.com/2016/08/godbless-lema-amtumia-waraka-mzito-rais.html
https://wepesimedia.blogspot.com/
http://wepesimedia.blogspot.com/
http://wepesimedia.blogspot.com/2016/08/godbless-lema-amtumia-waraka-mzito-rais.html
true
925270315725722404
UTF-8
Not found any posts VIEW ALL Readmore Reply Cancel reply Delete By Home PAGES POSTS View All

USIPITWE NA HIZI HAPA CHINI LABEL ARCHIVE SEARCH ALL POSTS Not found any post match with your request Back Home Sunday Monday Tuesday Wednesday Thursday Friday Saturday Sun Mon Tue Wed Thu Fri Sat January February March April May June July August September October November December Jan Feb Mar Apr May Jun Jul Aug Sep Oct Nov Dec just now 1 minute ago $$1$$ minutes ago 1 hour ago $$1$$ hours ago Yesterday $$1$$ days ago $$1$$ weeks ago more than 5 weeks ago Followers Follow THIS CONTENT IS PREMIUM Please share to unlock Copy All Code Select All Code All codes were copied to your clipboard Can not copy the codes / texts, please press [CTRL]+[C] (or CMD+C with Mac) to copy