Mstahiki Meya wa Jiji la Dar es Salaam Isaya Mwita amezitaka halmashauri zote jijini kuajiri watumishi ambao watakuwa wanafan...
Mstahiki Meya wa Jiji la Dar es Salaam Isaya Mwita amezitaka
halmashauri zote jijini kuajiri watumishi ambao watakuwa wanafanya
kazi ya kuzika miili ya watu ambao watabainika kuwa hawana ndugu.
Meya
Mwita ametoa kauli hiyo leo, kwenye kikao cha robo ya pili ya Baraza la
Madiwani wa Jiji la Dar es Salaam, ambapo amewaeleza madiwani hao kuwa
jukumu la kuzika marehemu wasiokuwa ndugu ni la jiji, kwakushirikiana na
halmashauri hivyo wanapaswa kuwajibika katika hilo.
Amefafanua kuwa hadi sasa jiji limeshanunua gari pamoja na mahitaji mengine ya kuhifadhia miili hiyo pindi inatokea na kwamba changamoto iliyopo sasa ni watu ambao watashirikiana kutekeleza jukumu hilo.
“Mtakuabliana na mimi kwamba tulishakubaliana kwamba jambo hili lifanyike kwenye halmashauri zetu, lakini hadi sasa Kinondoni pekee ndio wametimiza agizo hili, sasa ninaagiza tena halmashauri nyingine za jiji hili kuajiri watu hao. Hivyo marehemu wanapokuwa wamekaa muda mrefu wanalazimika kuzikwa na jiji, natulikubali kuchangia usafiri,dawa na sanda,” amesema Meya Mwita.
Amefafanua kuwa watu wasiokuwa na ndugu wanapokufa, wanapokaa hospitalini zaidi ya siku 20,jiji linalazimika kuwazika hivyo wapo ambao wanazikwa kwenye halmashauri mbalimbali