http://wepesimedia.blogspot.com/p/blog-page.html

Sababu ya samaki kupungua Ziwa Tanganyika

Image copyright GETTY IMAGES Image caption Watu waliongezeka eneo hilo miaka ya 1990 kutokana na ongezeko la wakimbizi Utafiti mpya umeb...

Ziwa Tanganyika

Image copyrightGETTY IMAGES
Image captionWatu waliongezeka eneo hilo miaka ya 1990 kutokana na ongezeko la wakimbizi
Utafiti mpya umebaini kupungua pakubwa kwa idadi ya samaki katika Ziwa Tanganyika, mojawapo ya maziwa muhimu zaidi kwa uvuvi duniani, kumetokana na ongezeko la joto duniani katika karne moja iliyopita.
Ziwa Tanganyika ndilo la kale zaidi Afrika na samaki wake huwa muhimu sana kwa lishe katika mataifa yanayopakana na ziwa hilo.
Lakini idadi ya samaki imepungua sana, huku wavuvi wakiendelea kuongezeka.
Ongezeko hili la wavuvi lilidhaniwa kuwa chanzo kikubwa cha kupungua kwa idadi ya samaki.
Lakini utafiti mpya unaonesha chanzo hasa ni ongezeko la joto duniani kutokana na mabadiliko ya tabia nchi.
Ziwa Tanyanyika ndilo la pili kwa ukubwa duniani miongoni mwa maziwa yenye maji yasiyo na chumvi na maji yake huwa katika mataifa manne: Burundi, Jamhuri ya KIdemokrasia ya Congo, Tanzania na Zambia.
Samaki kutoka kwa ziwa hilo hutoa asilimia 60 ya protini zitokanazo na wanyama ambazo huliwa na watu eneo hilo.
Aidha, ni eneo lenye aina nyingi ya wanyama na mimea.
Ziwa TanganyikaImage copyrightGETTY IMAGES
Image captionSamaki kutoka Ziwa Tanganyika hutegemewa sana na wakazi
Ili kufahamu mabadiliko yanayotokea katika ziwa hilo, watafiti wamechukua sampuli za mchanga kutoka kwenye kina cha ziwa hilo.
Baada ya kufanya utathmini wa mchanga huo na visukuku, wamepata viashiria kwamba idadi ya samaki imekuwa ikishuka sambamba na ongezeko la joto duniani.
Wanasayansi wanasema katika maziwa yanayopatikana maeneo yenye joto karibu na ikweta, ongezeko la joto katika maji hupunguza kuchanganyikana kwa maji kutoka sehemu ya juu ya ziwa ambayo huwa na oksijeni pamoja na maji yenye virutubisho vingi sehemu ya chini kwenye ziwa.
Kutochanganyikana vyema kwa maji haya husababisha virutubisho vinavyofika juu kwenye ziwa kupungua, hili hupunguza ukuaji wa miani (mimea ya rangi ya kijani, kahawia au nyekundu inayoota chini ya bahari) na hili hupelekea kupungua kwa lishe ya samaki.
Ziwa Tanganyika
Watafiti waliohusika katika utafiti huo wanasema ongezeko la joto limepunguza kuchanganyikana kwa maji, kupungua kwa ukuaji wa miani pamoja na kupungua kwa maeneo ambayo viumbe waishio chini ya bahari wanaweza kuishi na kustawi.
"Wazo letu lilikuwa kuchunguza visukuku na kubaini kushuka kwa idadi ya samaki kulianza wakati gani," anasema Prof Andrew Cohen kutoka Chuo Kikuu cha Arizona.
"Iwapo hili lilifanyika kabla ya kuanza kwa uvuvi wa kiviwanda miaka ya 1950, basi ungekuwa na ushahidi mkubwa kwamba hili halitokani na ongezeko la uvuvi na hivi ndivyo tulivyobaini."
Wanasayansi hao hata hivyo hawajapuuzilia mbali athari za ongezeko la uvuvi katika miongo sita iliyopita.
Wanasema kumekuwa an ongezeko la watu tangu miaka ya 1990, hasa kutokana na wakimbizi waliotoroka mizozo na kuhamia maeneo yaliyo karibu na ziwa hilo.
Ziwa TanganyikaImage copyrightGETTY IMAGES
Image captionWavuvi hutumia taa kuwavutia dagaa, ambao ndio sana huvuliwa kutoka kwenye ziwa hilo
"Ukizingatia mtindo wa sasa wa kuendelea kugawika zaidi kwa maji kwenye ziwa, idadi ya samaki itaendelea kupungua. Watu wanaosimamia sera wanafaa kuanza kufikiria kuhusu chanzo mbadala cha mapato na lishe kwa watu wanaoishi eneo hilo."
Matokeo ya utafiti huo yamechapishwa katika jarida la kisayansi la Proceedings of the National Academy of Sciences.

COMMENTS


TANGAZA NASISI KWA BEI NAFUU NA UPATE MATOKEO MAZURI KATIKA BIASHARA YAKO.

MAGAZETI$type=sticky$count=4


Name

BIASHARA NA UCHUMI BREAKING NEWS BURUDANI ENGLISH NEWS GOSIIP GOSPEL HABARI HABARI PICHA MAGAZETI MAKALA MATUKIO MICHEZO MUSIC VIDEO WAZO LANGU
false
ltr
item
WEPESI MEDIA : Sababu ya samaki kupungua Ziwa Tanganyika
Sababu ya samaki kupungua Ziwa Tanganyika
http://ichef.bbci.co.uk/news/660/cpsprodpb/EB15/production/_90718106_gettyimages-467222046.jpg
WEPESI MEDIA
https://wepesimedia.blogspot.com/2016/08/sababu-ya-samaki-kupungua-ziwa.html
https://wepesimedia.blogspot.com/
http://wepesimedia.blogspot.com/
http://wepesimedia.blogspot.com/2016/08/sababu-ya-samaki-kupungua-ziwa.html
true
925270315725722404
UTF-8
Not found any posts VIEW ALL Readmore Reply Cancel reply Delete By Home PAGES POSTS View All

USIPITWE NA HIZI HAPA CHINI LABEL ARCHIVE SEARCH ALL POSTS Not found any post match with your request Back Home Sunday Monday Tuesday Wednesday Thursday Friday Saturday Sun Mon Tue Wed Thu Fri Sat January February March April May June July August September October November December Jan Feb Mar Apr May Jun Jul Aug Sep Oct Nov Dec just now 1 minute ago $$1$$ minutes ago 1 hour ago $$1$$ hours ago Yesterday $$1$$ days ago $$1$$ weeks ago more than 5 weeks ago Followers Follow THIS CONTENT IS PREMIUM Please share to unlock Copy All Code Select All Code All codes were copied to your clipboard Can not copy the codes / texts, please press [CTRL]+[C] (or CMD+C with Mac) to copy