Aliyekuwa Diwani kupitia Chama cha NCCR MAGEUZI kata ya Makere wilayani Kasulu mkoani Kigoma, Laurent Poteza, amejivua nyazifa z...
Aliyekuwa Diwani kupitia Chama cha NCCR MAGEUZI kata ya Makere wilayani
Kasulu mkoani Kigoma, Laurent Poteza, amejivua nyazifa zake zote ndani
ya chama hicho na kujiunga CCM na kusema kuwa anamuunga mkono Rais
Magufuli.
Akizungunza
katika baraza la Halmashauri Kuu ya wilaya ya Kasulu Mara baada ya
kukabidhiwa kadi ya CCM na Katibu wa Itikadi na Uenezi wa CCM Taifa,
Hamphrey Polepole amesema ameamua kujiunga na CCM ili kuungana na Rais
Dkt. John Pombe Magufuli kuijenga nchi.
Katibu wa Itikadi na Uenezi wa CCM Taifa, Hamphrey Polepole kwa sasa yupo katika mkoa wa Kigoma na inadaiwa atakuwepo huko kwa muda wa mwezi mzima katika kujenga chama chake cha CCM.

Katibu wa Itikadi na Uenezi wa CCM Taifa, Hamphrey Polepole kwa sasa yupo katika mkoa wa Kigoma na inadaiwa atakuwepo huko kwa muda wa mwezi mzima katika kujenga chama chake cha CCM.