Mbunge wa Serengeti, Marwa Ryoba Chaha (CHADEMA) ameonyesha kutofurahishwa na kitendo cha polisi kutaka kuzuia mkutano wa Mbunge...
Mbunge wa Serengeti, Marwa Ryoba Chaha (CHADEMA) ameonyesha
kutofurahishwa na kitendo cha polisi kutaka kuzuia mkutano wa Mbunge wa
Tarime Vijijini CHADEMA, Mhe. John Heche kwa kile kinachodaiwa kuhofia
maandamano yanayoratibiwa na Mange Kimambi.
Mara
Ryoba amesema kuwa polisi wamekuwa na upendeleo kwa kuwa wanaona watu
wa CCM wakiendelea kufanya maandamano na mikutano ya kisiasa ili hali
watu wa upinzani wakizuiliwa.
"Haki huinua taifa; bali dhambi ni aibu ya watu wote. Nimepata taarifa kwamba Mbunge wa Tarime vijijini Mh. John Heche alizuiliwa asifanye mkutano Sirari eti kisa kuna maandamano ya Mange Kimambi, kwanza maandamano sio dhambi yapo kwa mujibu wa katiba yetu" alisema Mbunge Marwa Ryoba
Kwa mujibu wa Mbunge wa Tarime Vijijini kwa tiketi ya CHADEMA, John Heche amethibitisha hilo kuwa ni kweli kulikuwa na jaribio la kutaka kuzuiwa kufanya mkutano wake na wananchi wa Sirari kwa hofu ya maandamano ya tarehe 26 mwezi wa nne.
"Ni kweli polisi walitaka kutuzuia kufanya mkutano ila pamoja na polisi Sirari kufanya jaribio la kutaka kuzuia mkutano wangu na wananchi, kwa kisingizio cha hofu ya maandamano ya tarehe 26. Mkutano wangu ulifanyika na umemalizika salama, Asanteni sana wananchi wa Sirari kwa kujitokeza kwenye mkutano wetu" alisema John Heche.