http://wepesimedia.blogspot.com/p/blog-page.html

post-feature-image

Rais Magufuli Afuta Agizo La Kufunga Ndoa Kwa Sharti La Kuwa Na Cheti Cha Kuzaliwa


TANGAZA NASISI KWA BEI NAFUU NA UPATE MATOKEO MAZURI KATIKA BIASHARA YAKO.

Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania Dkt. John Pombe Magufuli amelifuta agizo lililotolewa jana tarehe 16 Machi, 2017 na Waziri wa Kat...

Nondo wakimalizana naye Iringa watuletee - Makonda
Jeshi la Polisi latoa maana ya maandamano
BREAKING NEWS, KADA WA CCM AJIUA KWA RISASI MAFINGA BENK

Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania Dkt. John Pombe Magufuli amelifuta agizo lililotolewa jana tarehe 16 Machi, 2017 na Waziri wa Katiba na Sheria Dkt. Harrison Mwakyembe linalotoa sharti la kuwa na cheti cha kuzaliwa kwa watu wote watakaofunga ndoa kuanzia tarehe 01 Mei, 2017.


Rais Magufuli amefuta agizo hilo leo wakati akizungumza na Waandishi wa Habari muda mfupi kabla ya kuondoka katika Ikulu ya Chamwino Mkoani Dodoma na kurejea Jijini Dar es Salaam.


Rais Magufuli amesema Serikali haiwezi kuruhusu sharti hilo kutumika kwa kuwa litawanyima haki ya kuoa na kuolewa Watanzania wengi ambao hawana vyeti vya kuzaliwa, huku utaratibu wa kupata vyeti hivyo ukiwa bado unakabiliwa na changamoto nyingi kwa wanaohitaji.


Amesema mpaka sasa idadi ya Watanzania walio na vyeti vya kuzaliwa ni chini ya asilimia 20 huku wengi wao wakiwa ni wananchi waishio vijijini ambako ni vigumu kupata vyeti hivyo, na wengine wakiwa ni waliozaliwa kabla ya kuanza kutolewa kwa vyeti vya kuzaliwa nchini mwaka 1961.


“Kwa hiyo ndugu zangu Watanzania msiwe na wasiwasi wowote, endeleeni na utaratibu wenu wa kuoa na kuolewa kama kawaida na kama kuna kifungu chochote cha sheria kinachomlazimisha mtu awe na cheti cha kuzaliwa ndipo aoe ama aolewe nitamuelekeza Waziri wa Katiba na Sheria Harrison Mwakyembe apeleke Bungeni kikarekebishwe” Amesema Rais Magufuli.


Rais Magufuli ametoa wito kwa wanasheria kuziangalia vizuri sheria zinazohusiana na kuzaliwa na kifo na kuoa na kuolewa ili zisilete mkanganyiko kwa wananchi.


Hata hivyo Mhe. Rais Magufuli ametoa wito kwa Watanzania kuendelea kupata vyeti vyao vya kuzaliwa kama kawaida na amewataka viongozi wote kuwahamasisha wananchi kuwa na vyeti hivyo.



Name

BIASHARA NA UCHUMI BREAKING NEWS BURUDANI ENGLISH NEWS GOSIIP GOSPEL HABARI HABARI PICHA MAGAZETI MAKALA MATUKIO MICHEZO MUSIC VIDEO WAZO LANGU
false
ltr
item
WEPESI MEDIA : Rais Magufuli Afuta Agizo La Kufunga Ndoa Kwa Sharti La Kuwa Na Cheti Cha Kuzaliwa
Rais Magufuli Afuta Agizo La Kufunga Ndoa Kwa Sharti La Kuwa Na Cheti Cha Kuzaliwa
https://blogger.googleusercontent.com/img/b/R29vZ2xl/AVvXsEj7ILOrKmHUdL92B7YZrhq0J8kudS0y9HMLBAzgchRgTkXqwUMrHCDNZ-WCZr2S-M7HWsp87OXZC0GVWbe2AzghVKN2OBoWDKXu59NWR3PFHkxKzkbas6a3RSc6-pIr1cY6lf1Qmc4A4s9v/s640/2.jpg
https://blogger.googleusercontent.com/img/b/R29vZ2xl/AVvXsEj7ILOrKmHUdL92B7YZrhq0J8kudS0y9HMLBAzgchRgTkXqwUMrHCDNZ-WCZr2S-M7HWsp87OXZC0GVWbe2AzghVKN2OBoWDKXu59NWR3PFHkxKzkbas6a3RSc6-pIr1cY6lf1Qmc4A4s9v/s72-c/2.jpg
WEPESI MEDIA
https://wepesimedia.blogspot.com/2017/03/rais-magufuli-afuta-agizo-la-kufunga.html
https://wepesimedia.blogspot.com/
http://wepesimedia.blogspot.com/
http://wepesimedia.blogspot.com/2017/03/rais-magufuli-afuta-agizo-la-kufunga.html
true
925270315725722404
UTF-8
Not found any posts VIEW ALL Readmore Reply Cancel reply Delete By Home PAGES POSTS View All

USIPITWE NA HIZI HAPA CHINI LABEL ARCHIVE SEARCH ALL POSTS Not found any post match with your request Back Home Sunday Monday Tuesday Wednesday Thursday Friday Saturday Sun Mon Tue Wed Thu Fri Sat January February March April May June July August September October November December Jan Feb Mar Apr May Jun Jul Aug Sep Oct Nov Dec just now 1 minute ago $$1$$ minutes ago 1 hour ago $$1$$ hours ago Yesterday $$1$$ days ago $$1$$ weeks ago more than 5 weeks ago Followers Follow THIS CONTENT IS PREMIUM Please share to unlock Copy All Code Select All Code All codes were copied to your clipboard Can not copy the codes / texts, please press [CTRL]+[C] (or CMD+C with Mac) to copy