Wabunge wa EFF wakikabiliana na maafisa wa usalama ...
| Wabunge wa EFF wakikabiliana na maafisa wa usalama |
Wabunge nchini
Afrika Kusini wamepigana bungeni baada ya spika kuamuru maafisa wa
usalama kuwaondoa kwa lazima wabunge wa upinzani ambao walimbeza rais
Jacob Zuma alipoingia bungeni tayari kulihutubia kikao.
Hata hivyo ujio wake uliwakera sana wabunge wa chama cha upinzani Economic Freedom Fighters (EFF).
Wabunge hao chini ya kiongozi wao Julius Malema walipiga mayowe na kumtupia matusi bw Zuma jambo lililomlazimu spika wa bunge kuamuru wabunge hao wa EFF kuondolewa nje.
| Zuma amekanusha madai yote dhidi yake. |
Zuma amekanusha madai yote dhidi yake.
Anatarajiwa kukamilisha hatamu yake mwaka wa 2019.
Uamuzi huo wa mahakama ulikuwa msumari wa moto kwa kidonda cha Zuma ambaye mwezi uliopita alipatikana na hatia ya matumizi mabaya ya madaraka yake alipokaidi amri yakulipa pesa za umma zilizotumiwa kukarabati nyumba yake ya Nkandla.



