Gazeti la The Sun limeripoti kuwa nyumba ya kocha mpya wa Manchester United Jose Mourinho ilivamiwa na kibaka wakati anatazama mechi ya ...
Gazeti la The Sun limeripoti kuwa nyumba ya kocha mpya wa Manchester United Jose Mourinho ilivamiwa na kibaka wakati anatazama mechi ya fainali ya UEFA Euro 2016.
Kibaka huyu ametajwa kuwa ni Gabor Roman, 25, na amefungwa kwa wiki nne kwa mujibu wa The Telegraph, baada ya kujaribu kuvunja chumba cha chini ya nyumba ya Mourinho iliyopo London mnamo July 10 2016.
Kibaka huyu alikamatwa na walinzi wa nyumba hio kabla ya polisi kufiki,wakati huo Jose hakuwepo nyumbani, alikuwa Paris Ufaransa na kwa sasa anatafuta nyumba mpya Manchester baada ya kuwa bosi pale Old Trafford.