Muigizaji wa Bongo movie na mzazi mwenza wa staa wa Bongo fleva Diamond Platnumz, Hamisa Mobetto amewajia juu watu wanaombeza baada ya ...
Muigizaji
wa Bongo movie na mzazi mwenza wa staa wa Bongo fleva Diamond Platnumz,
Hamisa Mobetto amewajia juu watu wanaombeza baada ya kusema kuwa yeye
sio Single mothers.
Siku ya juzi ilikuwa ni Mother’s Day/ siku ya Mama duniani na Hamisa aliweka wazi kuwa yeye sio Single mother kwa sababu anasaidiwa kulea watoto wake na Baba watoto wake.
Hamisa
ana watoto wawili ambapo mtoto wake wa kwanza Fantansy amezaa na
Majizzo na mtoto wake wa pili Dylan amezaaa na staa wa Bongo fleva
Diamond Platnumz.
Lakini
baada ya video hiyo kuingia mtandaoni watu walianza kumsema vibaya
kutokana na yeye kuongelea suala lake la kuzaa na wanaume wawili tofauti
ambao wote ameweka wazi wana uwezo.
Kupitia ukurasa wake wa Snapchat Hamisa altoa povu hili:
“Alafu
ngoja niwaambie kitu. Mimi ni mbaya kweli nakubali kabisa, alafu pia ni
maskini kweli kwenye maisha bado najikongoja kwahiyo hayo sio matusi
bali ni hali halisi. Kwahiyo mkikubali hali kama niliyokubali mie labda
mtaacha matusi yasio na faida.”
Aliongeza
kuwa “Alafu miaka inaenda siku zinakimbia pia…hamuwezi kuwa mna hasira
kila siku kisa nimezaa na wanaume wenye hela..hivi nachanganyikiwa au?
maana sababu ningine hamna zaidi ya hao wanaume wawili.”
Aliendelea
kuandika hivi, “Mnatakiwa mjua kwamba Fancy na Dee Mungu ndo alipanga
wazazi wa hawa watoto wawe nani..hasira zenu please msinimalizie mie
mtoto wa marehemu Mzee hassan..Its getting boring now.”


