Msanii na mtayarishaji wa muziki pia ni Hitmaker wa ‘Lover Boy’ Barnaba Classic. Mapema hii leo amefunguka kuhusiana na album yake ambayo ...
Msanii na mtayarishaji wa muziki pia ni Hitmaker wa ‘Lover Boy’ Barnaba Classic. Mapema hii leo amefunguka kuhusiana na album yake ambayo iko mbioni kutoka, ambapo mnamo mwaka jana alidai alizimika kusitisha kuachia albamu hiyo ilikujipa muda zaidi wa kujipanga.
Muimbaji huyo ambaye pia ni mtayarishaji wa muziki wa High Table Sound, Kupitia ukurasa wake wa Instagram, ametusanua ujio wa album hiyo na kudai kuwa ndani ya album hiyo kutakuwa na ladha tofauti tofauti za muziki.
Ujumbe huo ulisomeka hivi.. “Kwenye Album Yangu kutakua na kila aina ya muziki mungu akipenda|#% na ukibahatika Kupata Copy yako basi utakua umepata Historia Ya muziki africa na dunia nzima Utalia|| Utatabasamu ||% Utasikitika :/Utaburudika utojutia classic Music na ndani Yake kutakuw na kitabu kifup cha history ya maisha Yangu Barnabaclassic from uko yani adi Taharabu ziko ndani Inspiration Voice Mtu wa watu Namaliza Final na maandalizi yanaendele Now niko studio sana ndomana mnaniona Kimya watu wangu na #LONLEY iko mbioni kuja kwa masikio Yako.
ingawa nimebadirisha mfumo wa utoaji kazi zangu so endelea kuwa na mimi muda si mrefu nitakwambia mwongoZo Ukoje baada ya kujadili na management Yangu” Album hiyo mpya ya Barnaba ameipa jina la ‘Lover Boy’ ambalo linatokana na wimbo wake aliouachia miezi mitano iliyopita.