Kumekuwa na tetesi nyingi sana kuhusiana na ukaribu uliopo kati ya msanii wa bongo fleva,Linah Sanga na rapper Bill Nas ambapo watu weng...
Kumekuwa na tetesi nyingi sana kuhusiana na ukaribu uliopo kati ya msanii wa bongo fleva,Linah Sanga na rapper Bill Nas ambapo watu wengi wanadai kuwa wawili hao wanatoka kimapenzi.
Lakini Linah alipoulizwa kuhusiana na tetesi za yeye kutoka kimapenzi na Bill Nas alikana na kudai kuwa yeye na rapper huyo anayetamba na kibao cha Chafu Pozi hawana mahusiano yoyote ya kimapenzi bali ni rafiki yake wa karibu sana kiasi cha kushirikishana hata siri zao.
“Watu wanatakiwa wajue tu kuwa mimi na Bill Nas si wapenzi ila sisi ni watu wa karibu sana, sasa hivi mimi na Bill Nas ni washikaji sana maana siri yake ndiyo siri yangu, Bill Nas ndiye aliyenishauri nibadilike kwenye muziki na kunipa ‘connection’ na ‘Producer’ T Touch, yeye ndiye aliniambia nibadili mfumo mzima wa muziki wangu na ndiyo nikafanya hivyo” alisema Linah kwenye kipindi cha Planet Bongo cha East Africa Radio.
Source:Eatv