Mwanamuziki wa Bongo fleva kutoka label ya WCB Harmonize kwa mara ya kwanza amefungukia suala la kuvunjika kwa Mahusiano ya Zari na Dia...
Mwanamuziki
wa Bongo fleva kutoka label ya WCB Harmonize kwa mara ya kwanza
amefungukia suala la kuvunjika kwa Mahusiano ya Zari na Diamond
Platnumz.
Miezi
miwili iliyopita siku ya wapendanao Zari alitumia ukursa wake wa
Instagram kumwaga aliyekuwa mpenzi wake Diamond baada ya kuzidisha
michepuko ingawa suala hilo lilitokea muda mrefu uliopita lakini mpaka
leo linatrend.
Harmonize
mbali ya kuwa msanii wa Diamond lakini pia ni mtu wa karibu ambaye pia
alikuwa na ukaribu na Zari kwaiyo alipoulizwa anachukuliaje wawili hao
kuachana alisema anaheshimu maamuzi ya Zari.
Kwenye
mahojiano aliyofanya na Funiko Base ya Radio Five, Harmonize amefunguka
na kusema kuwa yeye binafsi anaheshimu maamuzi ya Zari kwa sababu ana
maamuzi yake binafsi.
"Mimi
naheshimu sana maamuzi ya mtu siwezi kuongea kama ni vibaya au ni
vizuri Kwanza muda wa kumshauri mtu kuhusu Mahusiano Yake ndio sina”.
Lakini
pia Harmonize alisisitiza kuwa hawezi kumuongelea sana Zari na
kuorodhesha mambo ambayo alimsaidia kwani unaweza ukaonekana mnafki.