http://wepesimedia.blogspot.com/p/blog-page.html

post-feature-image

MAMBO YATAKAYOKUFANYA UDUMU KATIKA NDOA/MAPENZI


TANGAZA NASISI KWA BEI NAFUU NA UPATE MATOKEO MAZURI KATIKA BIASHARA YAKO.

HAKUNA muda ambao hisia za mapenzi na msisimko huwa mkubwa kama kipindi ambacho upo kwenye penzi jipya. Ukiwauliza watu wengi leo ambao ...

Wachungaji 10 matajiri zaidi Duniani (hawa hapa)
Aanzisha Kampeni ya Kula Wabubu china
Vinywaji Vya Kutia Mwili Nguvu, Vina Athari Za Kiafya
HAKUNA muda ambao hisia za mapenzi na msisimko huwa mkubwa kama kipindi ambacho upo kwenye penzi jipya. Ukiwauliza watu wengi leo ambao wanateswa na mapenzi, wanata­mani siku zirudi nyuma ili warudie kufaidi mapenzi kama ilivyokuwa siku za mwanzomwanzo.
Hata hivyo, ni wachache wanaojua nini cha kufanya unapoanzisha penzi jipya ili hisia na msisimko unaoupata, udumu kwa muda mrefu na uendelee kuyafurahia maisha ya kimapenzi. Mapenzi ni kama nyumba, ukijenga msingi imara, nyumba yako itakuwa imara na ukijenga msingi legelege, usitegemee nyumba yako kuja kudumu baadaye.Kama upo kwenye mapenzi mapya na unatamani raha na msisimko unaoupata leo udumu, ni vizuri ukazingatia mambo yafuatayo:
MUONYESHE HESHIMA NA SHUKRANI
Wanandoa, wachumba au wapenzi wengi, hulalamika kwamba wenzi wao hawawaheshimu, hawana shukrani na ndiyo maana hawafurahii maisha yao ya kimapenzi. Unapokuwa kwenye hatua za mwanzo za mapenzi, jenga heshima kwa mwenzi wako bila kujali umri, cheo au hali ya kiuchumi. Hata kama mwenzi wako ana udhaifu fulani, kwa sababu umem­penda na kuamua kuwa naye, jifunze kumheshimu.
Pia jifunze kuwa na shukrani hata kwa yale mambo ma­dogo anayokufanyia. Wen­gi huwa hawaoni umuhimu wa kuwashukuru wenzi wao na matokeo yake wanajenga ufa am­bao baadaye unasa­babisha matatizo makubwa.
Hata kama mwenzi wako ame k u n u n u l i a pipi, akikupa shukrani kwa sababu ameku­fikiria ndiyo maana akakununulia. Hata kama mwenzi wako amekupa zawadi au kitu ambacho hujakipenda, badala ya kukimbilia ku­kosoa, onyesha kwanza shukrani, kesho na kes­hokutwa atapata nguvu ya kukutafutia vitu vizuri zaidi.

PATA MUDA WA KUMCHUN­GUZA KWA KINA
K u c ­h u n g u ­zana nina­komaani ­sha hapa, siyo ku­taka ku­jua kabla y a k o
alikuwa na nani au amewahi kutoka na nani, wahenga wanasema bata ukimc­hunguza sana huwezi kumla. Kuchungu­zana ninakokuzungumzia hapa, ni vizuri kufuatilia kwa kina ili ujue mwenzi wako anapenda nini, hapendi nini, kitu gani kinamfurahisha na kitu gani kinamtia hasira.
Mchunguze akiwa na hasira anakuwa­je na akiwa na furaha anakuwaje, ana­penda sana kufanya mambo gani (hobi) au anapenda sana zawadi za namna gani. Ukishamjua, ni rahisi sana kuishi naye hata pale anapokasirika au ana­pokerwa na jambo fulani kwani tayari utakuwa unajua kwamba akiwa hivi, ujue amekasirika au akifanya hivi ujue jambo fulani halipendi.
Pia itakusaidia kwenda naye sawa kwa sababu akikasirika, utajua ufanye nini ili afurahi kwa sababu tayari unavi­jua vitu vinavyomfurahisha. Ni makosa makubwa kufanya jambo wakati unajua kabisa mwenzi wako hapendi.
JENGA UTARATIBU WA KUMUOM­BA MSAMAHA UNAPOKOSEA
Wanaume wengi wanaamini kwamba hata wakikosea, hawatakiwi kuomba msamaha kwa sababu kuomba msama­ha ni ishara ya udhaifu, matokeo yake wanaendekeza mfumo dume bila kujua kwamba mapenzi ni demokrasia!
Bila kujali kwamba wewe ni mwa­naume au mwanamke, mkubwa au mdogo, una fedha au huna, inapotokea umeziumiza hisia za mwenzi wako, iwe kwa jambo dogo au kubwa, ni lazima uombe msamaha na kuahidi kutorudia makosa.
Ukishajenga utara­tibu huu, hata kama mwenzi wako hakuwa na kawaida ya kuom­ba msamaha, tara­tibu utambadilisha. Utashangaa na yeye anaomba msamaha na huo unakuwa mfu­mo wa maisha yenu. Kuwa makini kwamba ukiomba msamaha leo, siyo kesho unarudia tena kosa lilelile, ataona unam­fanyia makusudi.
Ukizingatia mambo haya machache, ukazidisha mapenzi na kumjali mwen­zi wako, ukawa mwa­minifu na mkweli, hisia tamu za mapenzi unazozihisi leo, zitadumu na u t a y a f u r a ­hia maisha yako ya ki­mapenzi.

Name

BIASHARA NA UCHUMI BREAKING NEWS BURUDANI ENGLISH NEWS GOSIIP GOSPEL HABARI HABARI PICHA MAGAZETI MAKALA MATUKIO MICHEZO MUSIC VIDEO WAZO LANGU
false
ltr
item
WEPESI MEDIA : MAMBO YATAKAYOKUFANYA UDUMU KATIKA NDOA/MAPENZI
MAMBO YATAKAYOKUFANYA UDUMU KATIKA NDOA/MAPENZI
https://matukiotz.co.tz/wp-content/uploads/2018/03/Anita-Nderu-e1498548822498-678x381.jpg
WEPESI MEDIA
https://wepesimedia.blogspot.com/2018/03/mambo-yatakayokufanya-udumu-katika.html
https://wepesimedia.blogspot.com/
http://wepesimedia.blogspot.com/
http://wepesimedia.blogspot.com/2018/03/mambo-yatakayokufanya-udumu-katika.html
true
925270315725722404
UTF-8
Not found any posts VIEW ALL Readmore Reply Cancel reply Delete By Home PAGES POSTS View All

USIPITWE NA HIZI HAPA CHINI LABEL ARCHIVE SEARCH ALL POSTS Not found any post match with your request Back Home Sunday Monday Tuesday Wednesday Thursday Friday Saturday Sun Mon Tue Wed Thu Fri Sat January February March April May June July August September October November December Jan Feb Mar Apr May Jun Jul Aug Sep Oct Nov Dec just now 1 minute ago $$1$$ minutes ago 1 hour ago $$1$$ hours ago Yesterday $$1$$ days ago $$1$$ weeks ago more than 5 weeks ago Followers Follow THIS CONTENT IS PREMIUM Please share to unlock Copy All Code Select All Code All codes were copied to your clipboard Can not copy the codes / texts, please press [CTRL]+[C] (or CMD+C with Mac) to copy