Kila mmoja wetu ana namna yake ambavyo anaweza akapima upendo kutoka kwa mtu ampendaye, lakini licha ya kupima aina hiyo ya upendo kutoka ...
Kila mmoja wetu ana namna yake ambavyo anaweza akapima upendo kutoka kwa mtu ampendaye, lakini licha ya kupima aina hiyo ya upendo kutoka kwa mtu ampendaye, ukweli ambao hauna kificho ni kwamba upendo wowote ule ni lazima ubebe vitu hivi viwili vikubwa ili uwe na maana katika sayari ya mahusiano.1. Jambo la kwanza ni Kujali.
Kuna wanaoamini kuwa kujali tuu inatosha kuonyesha kuwa unampenda fulani, au fulani kuonyesha anakujali basi hiyo ndio maana halisi ya upendo. Wengi hujikuta wakitumia muda mwingi kutafuta zawadi na surprises za ‘nguvu’ kama sehemu kuu ya kuonyesha upendo wao. Aina hii ya upendo inahusika sana hasa kwa watu waliopo mashuleni na vyuoni. Wengi wanaoamini maana hii ya upendo, husisitiza sana kuogopwa/kunyenyekewa kama sehemu ya kuonyeshwa kuwa nao wanapendwa.
2. Jambo la pili ni Kujitoa kafara:
Katika maana hii, upendo ni swala la jinsi gani unavyojitoa kwa mwingine ili kuona anakuwa na furaha na ajihisi kuwa salama kutokana na uwepo wako. La msingi katika aina hii ya upendo ni kupenda kumfahamu vema mwenzi wako, kujua shida zake, na ndoto zake, na kujitoa kwa hali na mali kuhakikisha anaona uwepesi katika shida zake, na kuwa anakuwa na matumaini ya kuwa ndoto zake zitatimia. Upendo wa namna hii huwa na subira, na huonekana zaidi kwa waliokomaa kifikra, na wenye kujiheshimu wao wenyewe.
Hivyo machaguo ni yako ni aina ipi ya upendo utakayoamua kumpa mpenzi wako, aidha kuamua kupenda kwa kujali au kupenda kwa kujitoa kafara au vyote kwa pamoja.
Asante na Endelea kutembelea wepesi media kila wakati.



