Msanii wa nyimbo za Injili Flora Mbasha ambaye alikuwa mke wa mwanamuziki wa Injili Emmanuel Mbasha, amefunguka juu ya kitendo cha aliye...
Msanii wa nyimbo za Injili Flora Mbasha ambaye alikuwa mke wa
mwanamuziki wa Injili Emmanuel Mbasha, amefunguka juu ya kitendo cha
aliyekuwa mume wake kumlalamikia kumnyima mtoto kwenye mitandao ya
kijamii.
Akizungumza na mwandishi wa eatv
Flora Mbasha amesema hawezi kulizungumzia suala la hilo kwenye vyombo
vya habari au kwenye mitandao, kwani yeye ndio anaujua ukweli, na iwapo
mahakama ilimpa haki ya kumuona mtoto, kuandika kwenye instagram sio
sahihi kwani mahakama haipo instagram.
“Siwezi kulizungumzia suala hilo kwenye vyombo vya habari, hilo suala kama aliandika kwenye instagram nami jibu ningelitolea instagram, na ukweli hamuujui sisi ndio tunaujua, na kama mahakama iliamua hivyo, na yeye kuandika instagram, kama mahakama iko instagram basi sawa acha aandike, ila siwezi kuliweka wazi”, amesema Flora Mbasha.
Wawili hao walitalikiana baada ya kesi aliyokuwa akituhumiwa Emmanuel kuisha na kukutwa hana hatia, na kisha Flora kuolewa na mwanaume mwengine.

Alichopost Emmanuel Mbasha instagram kuhusu mtoto wake na Flora.