Mtayarishaji wa muziki nchini Tanzania, Abba amefunguka na kudai si kweli ukimya wa Darassa unatokana na matumizi ya dawa za kulevya kama...
Mtayarishaji wa muziki nchini Tanzania, Abba amefunguka na kudai si
kweli ukimya wa Darassa unatokana na matumizi ya dawa za kulevya kama
baadhi ya watu wanavyodhani na kuwataka wawe wavumilivu kwani muhusika
mwenyewe atakuja kujitokeza.
Abba
ametoa kauli alipokuwa anazungumza kwenye kipindi cha eNewz inayorushwa
na EATV baada ya kuonea mfululizo wa tetesi zinazomuhusisha Darasa na
matumizi ya dawa za kulevya na kupelekea kupotea katika tasnia ya muziki
mpaka hii leo.
"Nashindwa kuwaelewa kwa jinsi mnavyosema Darasa haonekani sasa mmemuona vipi akiwa anatumia dawa za kulevya ?. Darasa yupo poa kabisa na labda hayo madude wanaosema wao wanayatumia wenyewe kwenye ndoto zao wanaoziota hao watu", amesema Abba.
Pamoja na hayo, Abba ameendelea kwa kusema "Darasa yupo poa na familia yake na wala hatumi kitu chochote mimi kama mwanae nasema yupo 'fresh' na kila siku nipo na Darasa na muda wote nikimuhitaji huwa nampata".
Mtazame hapa chini mtayarishaji wa muziki Abba akifunguka mengine zaidi kuhusu ukimya wa Darassa