Staa wa rnb kutoka Marekani Rihanna amepata shavu kubwa sana la kuigiza kwenye filamu ya Ocean Eight, ikiwa inahusu toleo la wanawake. Ri...
Staa wa rnb kutoka Marekani Rihanna amepata shavu kubwa sana la kuigiza kwenye filamu ya Ocean Eight, ikiwa inahusu toleo la wanawake.
Rihanna ataigiza na wasanii kama Anne Hathaway, Sandra Bullock, Cate Blanchett, Helena Bonham Carter, Mindy Kaling, na Nora Lum aka Awkwafina).
Filamu itaongozwa na Gary Ross aliyeongoza filamu kama The Hunger Games na itatayarishwa na Steven Soderbergh. Filamu inaanza kurekodiwa October mwaka huu.
Soderbergh aliongoza utayarishaji wa filamu za Ocean toka mwaka 2001 Ocean Eleven, 2004 na Ocean Twelve,na 2007 Ocean Thirteen. Mpaka sasa filamu hizi zimetengeneza dola za kimarekani bilioni $1.12 zikiwa na mastaa kama George Clooney, Brad Pitt, Matt Damon, Don Cheadle, na Bernie Mac.
Ukiacha filamu hio RiRi ataonekana kwenye filamu ya Luc Besson Valerian and the City of a Thousand Planets mwaka ujao akiwa na mastaa Cara Delevingne, Ethan Hawke, John Goodman, Clive Owen.Kwenye filamu tulimuona Rihanna kwenye Battleship mwaka 2012 na mwaka 2015 kwenye Home.