http://wepesimedia.blogspot.com/p/blog-page.html

post-feature-image

Diamond Platnumz na Alikiba Ndani ya Wimbo Mmoja....>>>>


TANGAZA NASISI KWA BEI NAFUU NA UPATE MATOKEO MAZURI KATIKA BIASHARA YAKO.

KUELEKEA fainali ya kombe la Mataifa Afrika kwa vijana chini ya miaka 17 nchini Gabon, kamati ya hamasa kwa Serengeti Boys inayoongozwa ...

Audio: Shilole Ageuka Mbogo Hewani Alipoulizwa Maswali ya Jike Shupa na Nuh Mziwanda
Video: Diamond Aweka Sanamu za Mafuvu ya Watu Ofisini Kwake, Je ni Ishara ya ‘Kifreemasons’ ?
ZariTheBossLady Amtaja Ivan kwenye Post Moja na Diamond Platnumz




KUELEKEA fainali ya kombe la Mataifa Afrika kwa vijana chini ya miaka 17 nchini Gabon, kamati ya hamasa kwa Serengeti Boys inayoongozwa na Mwenyekiti Charles Hilal imeandaa wimbo wa pamoja utakaoimbwa na wasanii maarufu wa muziki wa Bongo Fleva, Naseebb Abdul ‘Diamond’ na Ali Saleh ‘King Kiba' pamoja na wasanii wengine.

Wimbo huo wa pamoja ni maalum kwa ajili ya kuhamasisha kampeni za kuchangia timu ya taifa ya vijana chini ya umri wa miaka 17, Serengeti Boys itakayofanyika mwezi wa tano nchini Gabon ambapo zitapatikana nchi nne zitakazokwenda kombe dunia la vijana nchini India.

Mwenyekiti wa kamati hiyo, Charles Hilal amesema kuwa kwa pamoja wimbo utakaowahusisha wasanii wengine mbalimbali utakuwa na lengo kuu la kuhamasisha wananchi, wadau na wapenda michezo kuichangia timu hiyo ya vijana kwa lengo la kuisaidia malengo waliyokuwa wameyafikia ya kuipeleka timu hiyo kwenye fainali za kombe la Dunia nchini India.

Hilal amesema kuwa hatua hii ya kusaidia Serengeti Boys kutawajenga vijana hawa kufanya vizuri katika michuano ya mataifa Afrika kwa vijana ikiwa ni pamoja na kupata kambi nje ya nchi na kucheza mechi kadhaa za kirafiki kutoka nchini jirani lakini hata hivyo bado wanafikria kutafuta mechi ya kirafiki itakayochezwa hapa hapa Jijini Dar es salaam ikiwa ni kwa ajili ya kuwaaga kuelekea nchini Gabon.

Mjumbe wa Kamati ya Serengeti Boys, Maulid Kitenge amesema kwamba tayari ala za wimbo huo zimekwishatengenezwa na wasanii hao wote wametumiwa kwa ajili ya kuingiza sauti, ili mara moja wimbo huo ukamilishwe na kuanza rasmi kusaidia kampeni ya kuhamasisha Serengeti Boys.

“Tayari wasanii Ali kiba na Diamond wameshakubali kurekodi nyimo hiyona wameahidi kufanya haraka kuingiza sauti kwenye ala ambazo tumeshawatumia na baadae wasanii wengine kama Mwasiti Almasi, Darasa na Vanesa Mdee nao wataweka sauti zao,"amesema Kitenge.

Kiba na Diamond wote wapo kwenye Kamati iliyoundwa na Waziri wa Habari, Vijana, Utamaduni na Michezo, Nape Nnauye ya kuhamasisha na kuwaunganisha Watanzania kwa pamoja ili kuichangia Serengeti Boys iliyofuzu Fainali za Afrika nchini Gabon Mei mwaka huu.

Katibu wa Kamati hiyo ni Mwesigwa Selestine ambaye pia ni Katibu Mkuu wa Shirikisho la Soka Tanzania (TFF) wakati wajumbe ni Kitenge wa EFM Radio na TV, Mkurugenzi wa Mahusiano wa kampuni ya Airtel Tanzania, Beatrice Singano na Mrembo wa Tanzania wa mwaka 1999, Hoyce Temu, yumo Mkurugenzi wa Habari katika Wizara ya Habari, Utamaduni, Sanaa na Michezo, Hassan Abbas, Mkurugenzi wa Global Publishers Limited, Eric Shigongo na Mkurugenzi wa Radio Clouds, Ruge Mutahaba.

Pia, Serikali iliridhia kuwa mshiriki wa karibu kwa kila hatua kuanzia Bodi ya Mfuko wa Maendeleo ya timu za taifa, Kamati ya Hamasa kwa lengo la kupanga pamoja na kushirikiana kwa pamoja.

Mwenyekiti wa kamati ya hamasa kwa Serengeti Boys , Charles Hilal akizungumza na waandishi wa habari kuhusiana na maendeleo ya Serengeti Boys kueleka kwnye kombe la Mataifa Afrika chini ya miaka 17 yatakayofanyika nchini Gabon. Kushoto ni Mkurugenzi wa Habari katika Wizara ya Habari, Utamaduni, Sanaa na Michezo, Hassan Abbas na Mkurugenzi wa Mahusiano wa kampuni ya Airtel Tanzania, Beatrice Singano

Mwenyekiti wa kamati ya hamasa kwa Serengeti Boys , Charles Hilal akiwa pamoja na Mjumbe wa Kamati ya Serengeti Boys, Maulid Kitenge wakiwasikilizisha waandishi ala za wimbo unaotarajiwa kutumika kwa ajili ya kuhamasisha kuichangia Serengeti Boys

Name

BIASHARA NA UCHUMI BREAKING NEWS BURUDANI ENGLISH NEWS GOSIIP GOSPEL HABARI HABARI PICHA MAGAZETI MAKALA MATUKIO MICHEZO MUSIC VIDEO WAZO LANGU
false
ltr
item
WEPESI MEDIA : Diamond Platnumz na Alikiba Ndani ya Wimbo Mmoja....>>>>
Diamond Platnumz na Alikiba Ndani ya Wimbo Mmoja....>>>>
https://blogger.googleusercontent.com/img/b/R29vZ2xl/AVvXsEjVb2ztTWkfRobutBzVrHKCnI_fTrC8VvqmzgxiHHpwkqTYnYNGl5rYVbFib0QLXKMuDGuO17Oz-eZSt2iRefsSt3DStpfdxIhyTmmmeOkZID_XqRJXEcyz-L_kYps3cqEhBkEci9G-dEEE/s640/%255BUNSET%255D.jpg
https://blogger.googleusercontent.com/img/b/R29vZ2xl/AVvXsEjVb2ztTWkfRobutBzVrHKCnI_fTrC8VvqmzgxiHHpwkqTYnYNGl5rYVbFib0QLXKMuDGuO17Oz-eZSt2iRefsSt3DStpfdxIhyTmmmeOkZID_XqRJXEcyz-L_kYps3cqEhBkEci9G-dEEE/s72-c/%255BUNSET%255D.jpg
WEPESI MEDIA
https://wepesimedia.blogspot.com/2017/03/diamond-platnumz-na-alikiba-ndani-ya.html
https://wepesimedia.blogspot.com/
http://wepesimedia.blogspot.com/
http://wepesimedia.blogspot.com/2017/03/diamond-platnumz-na-alikiba-ndani-ya.html
true
925270315725722404
UTF-8
Not found any posts VIEW ALL Readmore Reply Cancel reply Delete By Home PAGES POSTS View All

USIPITWE NA HIZI HAPA CHINI LABEL ARCHIVE SEARCH ALL POSTS Not found any post match with your request Back Home Sunday Monday Tuesday Wednesday Thursday Friday Saturday Sun Mon Tue Wed Thu Fri Sat January February March April May June July August September October November December Jan Feb Mar Apr May Jun Jul Aug Sep Oct Nov Dec just now 1 minute ago $$1$$ minutes ago 1 hour ago $$1$$ hours ago Yesterday $$1$$ days ago $$1$$ weeks ago more than 5 weeks ago Followers Follow THIS CONTENT IS PREMIUM Please share to unlock Copy All Code Select All Code All codes were copied to your clipboard Can not copy the codes / texts, please press [CTRL]+[C] (or CMD+C with Mac) to copy