http://wepesimedia.blogspot.com/p/blog-page.html

post-feature-image

CHECK MAMBO YA KUFANYA KABLA YA KUINGALIIA KWENYE NDOA


TANGAZA NASISI KWA BEI NAFUU NA UPATE MATOKEO MAZURI KATIKA BIASHARA YAKO.

DUNIA ya sasa si kama ya zamani. Ndoa zimekuwa hazidumu kama ilivyokuwa zamani. Hii yote imetokana na mmonyoko wa maadili ambao umeiond...

JE! MUNGU ANAMPA MWANAMKE HAKI YA KUTOA MIMBA IWAPO NI MHANGA WA UBAKAJI?
Faida 10 za kunywa maji ya limao kila siku asubuhi
Zijue Sababu za Mwanamme/Mwanamke Kusalitiwa
DUNIA ya sasa si kama ya zamani. Ndoa zimekuwa hazidumu kama ilivyokuwa zamani. Hii yote imetokana na mmonyoko wa maadili ambao umeiondoa dhana halisi ya ndoa na watu kuifanya kama fasheni. Uhalisia wa ndoa na maisha haupo. Watu sasa hivi wanaoana ilimradi tu kutimiza matamanio. Mwanamke umri umekwenda, anataka tu na yeye aitwe mke wa fulani, basi analazimika kuingia kwenye ndoa. Mwanaume anaoa kwa sababu anaona amechoka kujipikia chakula.
Watu wanaoana ili tu wafanye maonesho katika mitandao ya kijamii. Marafiki wajue kwamba fulani naye ameoa, hakuna tena maadili ya ndoa. Mtu ameolewa, lakini bado anatamani kutanga na dunia, mathalan aende klabu, ajirushe na marafiki. Athari za maadili zilizoanzia kutoka kwa baadhi ya wazazi ndizo zilizosababisha majanga makubwa kwa kizazi cha sasa. Wazazi wamewapa uhuru sana vijana wao, matokeo yake wanajikuta wakitengeneza ‘bomu’ ambalo hulipuka muda wowote.
Changamoto za ndoa hawazijui. Hawana uvumilivu, wakikutana na magumu kidogo tu, hukimbilia kuachana. Kizazi kimejeruhiwa kwelikweli. Kila mwanamke unayekutana naye ameshakuwa sugu kwa kuumizwa. Ameshaongopewa ndoa kiasi cha kutosha. Amekutana na majambazi, wezi na watu wasiofaa katika jamii. Kutokana na sarakasi hizo alizopitia, mwanamke haitamani tena ndoa. Anacholilia yeye kinakuwa ni kupata mtoto, maisha yaendelee.
Mwanaume naye vivyo hivyo, ameshakutana na matapeli wa mapenzi kiasi cha kutosha. Haoni hata mke wa kumuoa, anabaki kuwa mhuni tu miaka yote. Jamani tukubali tukatae, kuna vitu tunavikosea. Wengi wetu tunaingia kwenye ndoa pasi na kujua misingi yake. Hatujui kanuni zake. Hatujui nini tunapaswa kufanya kabla hatujajiingiza kwenye ndoa na ndiyo maana hata tukiingia tunaishia kuishi miaka miwili au mitatu, ndoa chali! Badala ya kusikilizana, kwenye ndoa kila mmoja anajifanya mjuaji.
Mwanaume anapambana kusaka kuwa kichwa cha familia, mwanamke naye anataka kuwa msemaji mkuu wa familia. Hakuna wa kumsikiliza mwenzake, nyumba inatawaliwa na ugomvi kila siku. Ndugu zangu, kabla ya kuingia kwenye ndoa yakupasa kwanza ujitathmini. Ujue ujijue kwamba wewe ni nani na unataka kuingia kwenye ndoa ya aina gani.
Una-taka kui-ngia kwenye ndoa, upo tayari kua-cha mambo ya kitoto? Upo tayari kuacha uhuni, starehe za kijingajinga? Upo tayari kukutana na misukosuko? Unakwenda kwenye ndoa, umejiandaa kuwa baba? Umejiandaa kuihudumia familia? Upo tayari kushirikiana na mwenzako katika uzima na magonjwa? Unajua mikikimikiki ya ndugu wa pande zote mbili? Ukijiridhisha wewe una hizo sifa, angalia na upande wa pili.
Unayetaka kuanzisha naye uhusiano, je, ana sifa hizo? Ni mvumilivu? Anaweza kukabiliana na changamoto kama ulizojitathmini wewe? Kama hana ni bora kuachana naye mapema katika kipindi cha urafiki ili usije kujilamu baadaye. Kubwa kuliko yote jitahidi uingie na mtu kwenye ndoa ambaye ana utu, ana hofu ya Mungu. Eneo hili ni la kuwa makini, waswahili wanasema bora ukosee njia, lakini si kuoa. Hakikisha unakuwa mtu sahihi na unatafuta mtu sahihi vilevile.
Mtu atakayeweza kuvumilia kipindi ambacho mtakuwa kwenye wakati mgumu. Tafuta mtu ambaye tatizo lako litakuwa lake na lake litakuwa lako. Mtu asiye na tamaa za kijinga au mwenye hulka ya umalaya. Mtu ambaye kweli ameamua kwa dhati kuishi maisha ya ndoa na si kutamani sherehe. Na Erick Evarist.

Name

BIASHARA NA UCHUMI BREAKING NEWS BURUDANI ENGLISH NEWS GOSIIP GOSPEL HABARI HABARI PICHA MAGAZETI MAKALA MATUKIO MICHEZO MUSIC VIDEO WAZO LANGU
false
ltr
item
WEPESI MEDIA : CHECK MAMBO YA KUFANYA KABLA YA KUINGALIIA KWENYE NDOA
CHECK MAMBO YA KUFANYA KABLA YA KUINGALIIA KWENYE NDOA
https://matukiotz.co.tz/wp-content/uploads/2018/03/Grace-Msalame_INSTAGRAM-678x381.jpg
WEPESI MEDIA
https://wepesimedia.blogspot.com/2018/03/check-mambo-ya-kufanya-kabla-ya.html
https://wepesimedia.blogspot.com/
http://wepesimedia.blogspot.com/
http://wepesimedia.blogspot.com/2018/03/check-mambo-ya-kufanya-kabla-ya.html
true
925270315725722404
UTF-8
Not found any posts VIEW ALL Readmore Reply Cancel reply Delete By Home PAGES POSTS View All

USIPITWE NA HIZI HAPA CHINI LABEL ARCHIVE SEARCH ALL POSTS Not found any post match with your request Back Home Sunday Monday Tuesday Wednesday Thursday Friday Saturday Sun Mon Tue Wed Thu Fri Sat January February March April May June July August September October November December Jan Feb Mar Apr May Jun Jul Aug Sep Oct Nov Dec just now 1 minute ago $$1$$ minutes ago 1 hour ago $$1$$ hours ago Yesterday $$1$$ days ago $$1$$ weeks ago more than 5 weeks ago Followers Follow THIS CONTENT IS PREMIUM Please share to unlock Copy All Code Select All Code All codes were copied to your clipboard Can not copy the codes / texts, please press [CTRL]+[C] (or CMD+C with Mac) to copy