http://wepesimedia.blogspot.com/p/blog-page.html

post-feature-image

Zijue Sababu za Mwanamme/Mwanamke Kusalitiwa


TANGAZA NASISI KWA BEI NAFUU NA UPATE MATOKEO MAZURI KATIKA BIASHARA YAKO.

KWENYE ulimwengu wa mapenzi, hakuna kitu kibaya kama kusalitiwa na mpenzi wako tena unayempenda kwa dhati. Ni jambo linalouma sana kiasi ...

HADITHI YA KUSISIMUA:- DALILI YA MVUA NI MAWINGU...!
FAIDA ZA KUTUMIA JUICE YA TANGAWIZI AU CHAI YA TANGAWIZI
SILOAM: SIYO KUPATWA KWA JUA NI ‘ JUA LA HAKI’





KWENYE ulimwengu wa mapenzi, hakuna kitu kibaya kama kusalitiwa na mpenzi wako tena unayempenda kwa dhati. Ni jambo linalouma sana kiasi cha kuwafanya baadhi ya watu kuchukua uamuzi wa kujiua kwa kunywa sumu na wengine kuchanganyikiwa.

Lakini mara nyingi sana wengi wanapenda kujua sababu zinazowafanya wepenzi wao wawasaliti ili waweze kuchukua hatua za kuhakikisha hayawakuti hayo. Leo kupitia ukurasa huu nimeona nikupe baadhi ya sababu ambazo huwafanya watu walio kwenye uhusiano kusaliti.



Sababu za wanaume
Wanaume walio wengi wameingia kwenye mapenzi na wanawake wasioendana nao.

Hapa namaanisha kwamba wapo ambao anakutana na mwanamke, anaingia naye kwenye uhusiano kisha baada ya siku chache anagundua mtu huyo hakuwa mtu sahihi kwake. Matokeo yake sasa anashawishika kutoka nje ya uhusiano wake.
Ucheshi wa mwanamke

Wanaume walio wengi hawapendi wanawake watulivu. Hapa siongelei wanawake micharuko, naomba nieleweke vizuri. Wanaume hasa vijana wa sasa wanapenda wanawake ambao wapo kiuchangamfu zaidi, yaani amechangamka kwenye ubunifu wa mambo, utundu wa chumbani na hata ushapu kwenye mambo ya kidunia yanayoendelea.



Asikudanganye mtu kuwa siku hizi wanaume eti wanapenda mwanamke ambaye ni wa kijijini, anayeanza naye moja kwenye kumfundisha. Aisee utashangaa mwenzako anakuacha ndani kisha anakwenda kwa mwanamke mwingine ambaye yupo tofauti na wewe.


Tendo la ndoa

Usije kujidanganywa kuwa eti kwa sababu uko poa kwenye mambo yetu ya sita kwa sita basi huwezi kusalitiwa, lahasha! Kumbuka kuwa tendo hilohilo linaweza kununuliwa akafanya yake na akamaliza lakini jiulize wale wanaosaliti halafu wanahamia moja kwa moja kwa wanawake inakuwaje? Kule hafuati tendo, kuna kitu cha ziada atakuwa anakifuata.


Mapishi na usafi

Kama wewe mwanamke hujui kuufanyia usafi mwili wako na hata mazingira ya nyumbani kwako, jua moja kwa moja mumeo atakusaliti na kwako atarudi kulala tu ilimradi kutimiza ndoa.



Pia kuna suala la mapishi, kama wewe mwanamke hujui kumpikia mumeo chakula kizuri na kukibadili kila siku utasalitiwa tu. Wanaume ni watu wa kukinai mara moja unatakiwa kuwa mbunifu kwenye kila kitu.


Kuboreka



Hapa ndiYo nasisitiza lile suala la mwanamke kuwa mcheshi kwa mumewe, mfano kumtania mume, kuwa na furaha uwapo naye wakati wote. Wanaume ni wepesi kuboreka, kama atakuja nyumbani na kukukuta kwenye hali ya kila siku, mara ooh! Naumwa.



Mara ooh! Jirani kanifanyia hivi, yaani lawama… lawama… mpaka usiku unaisha mnalala, mume ataboreka na kuhamia kwingine. Akina mama wengi wanapenda sana lawama, hawajui kuwa wanaume mambo hayo wakati mwingine hawayapendi.



Kama una lawama zako hebu subiri basi siku za wikiendi mkiwa mmetulia hasa mida ya chai ndiyo umpe lawama zote lakini siyo kila akirudi nyumbani.



Vijana wanakwambia unamkata ‘stimu’, kama alikuwa na hamu ya kitu kutoka kwako akikukuta uko kwenye mudi za lawama na visirani, anaishia hapo.



Kwa upande wa mwanamke Nao huwa na sababu za kusaliti lakini hapa nitaziongelea sababu kuu mbili ambazo mwanaume ukiziibua, mwanamke ni rahisi sana kuhamisha hisia na kuzipeleka kwingine.


Kutokumfuatilia

Kwa mwanamke, mwanaume akiacha kumfuatilia ni kosa kubwa sana kwani moja kwa moja ataona kuwa huna mapenzi naye tena kama zamani na yeye kama ni mtu wa kusaliti, atasaliti tu kwani wanawake kiukweli wanapenda ‘atensheni’.


Kumridhisha kwenye tendo la ndoa

Kama mwanaume utakuwa humridhishi mkeo kwenye tendo la ndoa ni wazi moja kwa moja akipata mjanja atakusaliti.

Name

BIASHARA NA UCHUMI BREAKING NEWS BURUDANI ENGLISH NEWS GOSIIP GOSPEL HABARI HABARI PICHA MAGAZETI MAKALA MATUKIO MICHEZO MUSIC VIDEO WAZO LANGU
false
ltr
item
WEPESI MEDIA : Zijue Sababu za Mwanamme/Mwanamke Kusalitiwa
Zijue Sababu za Mwanamme/Mwanamke Kusalitiwa
https://globalpublishers.co.tz/wp-content/uploads/2017/06/african-wedding-couple.jpg
WEPESI MEDIA
https://wepesimedia.blogspot.com/2017/06/zijue-sababu-za-mwanammemwanamke.html
https://wepesimedia.blogspot.com/
http://wepesimedia.blogspot.com/
http://wepesimedia.blogspot.com/2017/06/zijue-sababu-za-mwanammemwanamke.html
true
925270315725722404
UTF-8
Not found any posts VIEW ALL Readmore Reply Cancel reply Delete By Home PAGES POSTS View All

USIPITWE NA HIZI HAPA CHINI LABEL ARCHIVE SEARCH ALL POSTS Not found any post match with your request Back Home Sunday Monday Tuesday Wednesday Thursday Friday Saturday Sun Mon Tue Wed Thu Fri Sat January February March April May June July August September October November December Jan Feb Mar Apr May Jun Jul Aug Sep Oct Nov Dec just now 1 minute ago $$1$$ minutes ago 1 hour ago $$1$$ hours ago Yesterday $$1$$ days ago $$1$$ weeks ago more than 5 weeks ago Followers Follow THIS CONTENT IS PREMIUM Please share to unlock Copy All Code Select All Code All codes were copied to your clipboard Can not copy the codes / texts, please press [CTRL]+[C] (or CMD+C with Mac) to copy