http://wepesimedia.blogspot.com/p/blog-page.html

post-feature-image

MFANYABIASHARA AUAWA CHOONI AKIWA CLUB


TANGAZA NASISI KWA BEI NAFUU NA UPATE MATOKEO MAZURI KATIKA BIASHARA YAKO.

Angel Edward enzi za uhai wake Kamanda wa polisi mkoa wa Singida ACPDebora Magiligimba. **** JESHI la Polisi mkoani Singida linawa...

ANGALIA MTOTO ATAKAYELIPWA MILIONI 134 KWA AMRI YA MAHAKAMA
Mwalimu Mkuu Ajinyonga Akiwa Ofisini Kwake baada ya kugawa chaki kwa walimu ,aandika Ujumbe Mzito
ANGALIA MWANAMKE ALIYEMUOA MWANAMKE MWENZAKE,NI RAIA KUTOKA AFRIKA

Angel Edward enzi za uhai wake


Kamanda wa polisi mkoa wa Singida ACPDebora Magiligimba.
****

JESHI la Polisi mkoani Singida linawashikilia watu wawili kutokana na kifo cha mashaka cha mfanyabiashara, Tausi Hamisi au Angel Edward (39) mkazi wa eneo la Ipembe mjini Singida.

Kamanda wa polisi mkoa wa Singida, Debora Magiligimba aliwataja wanaoshikiliwa kuwa ni Haruna Athuman (34) mlinzi wa Katala Beach Hotel (KBH) ambaye anaishi eneo la Kindai mjini Singida na Salma Mohamed (28) mkazi wa Majengo katika Manispaa ya Singida.

Magiligimba alisema kuwa tukio hilo ni la Agosti 24, mwaka huu saa 11.30 alfajiri ambapo inadaiwa kuwa mwili wa mfanyabiashara huyo ulikutwa pembeni mwa choo cha wanawake katika hoteli hiyo.

Alisema kuwa siku ya Jumatano Agosti 23, mwaka huu majira ya jioni marehemu aliondoka nyumbani kwao akiwa na gari yake ndogo kisha kuungana na wenzake kwenda ukumbi wa Taasisi ya Uhasibu (TIA) eneo la Ginnery mjini hapa ambapo kulikuwa na harusi.

Hata hivyo, Magiligimba alidai kuwa baadae usiku huo marehemu akiwa na wenzake walienda Skyway Night Club eneo la Kibaoni alikokuwa anatumbuiza mwanamuziki mashuhuri, Christian Bella kuendelea na starehe.

Inadaiwa baada ya muda, alitoka Skyway na kwenda KBH akiwa ameambatana na rafiki yake aitwaye Salma Mohamed pamoja na mwanaume mmoja ambaye hakufahamika jina wala makazi yake mara moja ambapo inasemekana waliendelea na starehe hotelini hapo.

"Ilifika muda marehemu alienda kujisaidia chooni ndipo mwanaume huyo aliyekuwa amekaa naye alimfuata. Hakuweza kurejea tena hadi mlinzi alipogundua mwili wa marehemu alfajiri. Muuaji aliondoka na simu ya marehemu huku akiacha gari lake hotelini hapo", alisema.

Kwa mujibu wa Kamanda Magiligimba, uchunguzi wa daktari unaonesha kuwa chanzo cha kifo cha marehemu ni kukosa hewa na kwamba hakuna dalili zozote za kunyongwa shingo.

Ametoa wito kwa wakazi wa mkoa huo kubadilika na kuacha tabia ya kuambatana na watu wasiowafahamu kwenye maeneo ya starehe na inapotokea wawe wepesi wa kudadisi na ikiwa watamtilia shaka watoe taarifa polisi haraka.

Na Abby Nkungu

Name

BIASHARA NA UCHUMI BREAKING NEWS BURUDANI ENGLISH NEWS GOSIIP GOSPEL HABARI HABARI PICHA MAGAZETI MAKALA MATUKIO MICHEZO MUSIC VIDEO WAZO LANGU
false
ltr
item
WEPESI MEDIA : MFANYABIASHARA AUAWA CHOONI AKIWA CLUB
MFANYABIASHARA AUAWA CHOONI AKIWA CLUB
https://2.bp.blogspot.com/-O3D24_1BFLg/WaL4Gb5QwSI/AAAAAAAARiM/uB5coZfpe1oGO0sH2LDfWICYuhX0xo4bwCLcBGAs/s640/IMG-20170825-WA0031.jpg
https://2.bp.blogspot.com/-O3D24_1BFLg/WaL4Gb5QwSI/AAAAAAAARiM/uB5coZfpe1oGO0sH2LDfWICYuhX0xo4bwCLcBGAs/s72-c/IMG-20170825-WA0031.jpg
WEPESI MEDIA
https://wepesimedia.blogspot.com/2017/08/mfanyabiashara-auawa-chooni-akiwa-club.html
https://wepesimedia.blogspot.com/
http://wepesimedia.blogspot.com/
http://wepesimedia.blogspot.com/2017/08/mfanyabiashara-auawa-chooni-akiwa-club.html
true
925270315725722404
UTF-8
Not found any posts VIEW ALL Readmore Reply Cancel reply Delete By Home PAGES POSTS View All

USIPITWE NA HIZI HAPA CHINI LABEL ARCHIVE SEARCH ALL POSTS Not found any post match with your request Back Home Sunday Monday Tuesday Wednesday Thursday Friday Saturday Sun Mon Tue Wed Thu Fri Sat January February March April May June July August September October November December Jan Feb Mar Apr May Jun Jul Aug Sep Oct Nov Dec just now 1 minute ago $$1$$ minutes ago 1 hour ago $$1$$ hours ago Yesterday $$1$$ days ago $$1$$ weeks ago more than 5 weeks ago Followers Follow THIS CONTENT IS PREMIUM Please share to unlock Copy All Code Select All Code All codes were copied to your clipboard Can not copy the codes / texts, please press [CTRL]+[C] (or CMD+C with Mac) to copy