Wananchi wakiwa katika jengo kujionea jinsi moto ulivyoteketeza nyumba ya mwenyekiti milango unayoona ndiyo vyumba 6 vya biasghara vilivyot...
Wananchi wakiwa katika jengo kujionea jinsi moto ulivyoteketeza nyumba ya mwenyekiti milango unayoona ndiyo vyumba 6 vya biasghara vilivyoteketea kabisa bila kusalia chochote

Baadhi ya wananchi wakiangalia jinsi nyumba ilivyoteketea

Moja ya Nyumba ya mwenyekiti wa mtaa wa olkungu kata ya murieti iliyoungua moto

Bi veronica Julias Ambaye nyumba yake imeteketea kwa moto

Mwenyekiti wa mtaa wa olkungui kata ya Muriety Bw Julius Lenina ambaye pia ni mmiliki wa jengo lililoteketea kwa moto akiwa katika hali ya majonzi akiwa na majirani waliomtembelea kumfariji

Mbao zilizokolewa kwenye moto ambao umeteketeza vyumba sita vya biashara jijini arusha

Numbani kwa mwenyekiti wa mtaa wa olkungu akiwa na majirani waliofika kumfariji baada ya tukio la moto
Vyumba 6 vya biashara vimeteketea kwa moto katika mtaa wa olkung"u kata ya Terati jijini arusha na kusababisha hasara ya zaidi ya shilingi milioni 80 ambayo ni Mali ya mwenyekiti wa mtaa huo bwana Julius lenina.
Akizungumzia chanzo cha moto huo Mwenyekiti huyo ambaye ndiye mmiliki wa nyumba hiyo amesema kuwa chanzo cha moto huo ni majani ambayo yalikuwa karibu na chumba cha kulala watoto na hakuna mtu ambaye amepata madhara kutoka na moto huo ambao umeteketez kila kitu katika jengo hilo.
Ameongeza kuwa moto huo ulianza majira ya saa nane usiku wakati wakiwa wamelaa na umeteketeza mali zenye dhamani ya zaidi ya sh.ml 80 ambayo ni maduka na vitu vilivyokuwa ndani ya nyumba hiyo ambayo ilikuwa imepangishwa na wapangaji kwa ajili ya biashara.
Amesema kuwa walishindwa kuzima moto kutokana na nguvu ya moto huo kwa kuwa wamewaokoa Watoto japokuwa gari la zomamoto lilichelewa kufika kutokana na kupotea njia.
Ameeleza kuwa siku za nyuma kabla ya tukio hilo alipata maneno ya vitisho kutoka kwa mfanyakazi wake kwamba atamfanyia kitu kibaya na kumsambaratisha ndipo baada ya siku kadhaa moto ukawaka katika nyumba yake
Upande wa Diwani wa kata hiyo ya Terati bwana mosses obedi mengoriki amekemea vikali kitendo hicho cha moto na kuitaka serikali kufuatilia na kubaini mtu aliyekusika na ukatili huo
Akizungumza mama Mwenye nyumba hiyo iliyoteketea Bi veronica Julius ameshukuru kunusurika kwa Watoto wake wawili ambao walikuwa wamelala kwenye chumba ambacho nacho kilishika moto.
Tukio hilo siyo la kwanza kutokea katika jiji la arusha ikumbukwe kuwa tukio kama hili liliwahi kutokea katika kata ya lemara jijini arusha jambo ambalo linatia wasiwasi kwa baadhi ya wananchi