http://wepesimedia.blogspot.com/p/blog-page.html

post-feature-image

Zitambue Simu ambazo hazifanyi kazi tena na WhatsApp.!


TANGAZA NASISI KWA BEI NAFUU NA UPATE MATOKEO MAZURI KATIKA BIASHARA YAKO.

Wakati wa kuanzishwa kwa WhatsApp, simu nyingi za smartphone zilikuwa za Blackberry na Nokia Huduma ya WhatsApp haitumiki tena katika ain...

Serikali Yaunda Tume Yakupambana na Picha na Video za Ngono
Majambazi wavamia ofisi za DRFA na kutaka shilingi milioni 150
Polisi waua mtu mmoja akidaiwa kuwa jambazi

Wakati wa kuanzishwa kwa WhatsApp, simu nyingi za smartphone zilikuwa za Blackberry na Nokia

Huduma ya WhatsApp haitumiki tena katika aina kadha za simu za zamani zikiwemo zile zinazotumia mfumo wa Windows Phone 7.1, Android 2.1 na Android 2.2, na simu aina ya iPhone 3GS/iOS 6.

Kampuni ya Facebook inayomiliki huduma hiyo ilisema inataka kuangazia kustawisha "huduma katika mifumo inayotumiwa na watu wengi."

WhatsApp, ilipangiwa kuacha kufanya kazi katika mifumo hiyo ya programu mwishoni mwa Desemba 2016.

Hatua hiyo ilikuwa imetangazwa na Facebook mapema mwezi Februari mwaka jana.
Jinsi ya kuweka bold na italiki katika WhatsApp

Kampuni hiyo ilikuwa imeorodhesha simu za BlackBerry OS, BlackBerry 10, Nokia S40 na Nokia Symbian S60 kuwa miongoni mwa simu ambazo zingekatiwa huduma mwishoni mwa mwaka 2016 lakini ikabadilisha uamuzi wake na kuongeza muda hadi Juni 30, 2017.

Kampuni hiyo ilijitetea na kusema kwamba haikusudii kuwatupa wateja wake ambao wamechangia sana katika ufanisi wake lakini ni kutokana na mabadiliko ya teknolojia.

"Simu hizi hazina uwezo wa kiteknolojia tunaohitaji kuendelea kuimarisha huduma yetu siku zijazo," kampuni hiyo ilisema.WhatsApp hutumiwa na watu bilioni moja duniani

Orodha kamili ya mifumo ya simu ambayo wateja hawataweza tena kutumia WhatsApp ni hii hapa:
Android 2.1 na Android 2.2
Windows Phone 7
iPhone 3GS/iOS 6

Simu ambazo wateja wake hawataweza kutumia Whatsapp ifikapo Juni 30,2017 ni:
BlackBerry OS and BlackBerry 10
Nokia S40
Nokia Symbian S60

Wanaotumia simu za aina hiyo wameshauriwa kununua simu za kisasa zaidi.

Kampuni hiyo imesema wakati wa kuanzishwa kwa WhatsApp mwaka 2009, asilimia 70 ya simu wakati huo zilikuwa za BlackBerry na Nokia.Simu ya Blackberry

Lakini sasa asilimia 99.5 ya simu zinatumia mifumo ya Google, Apple na Microsoft.

SOURCE..................BBC

Name

BIASHARA NA UCHUMI BREAKING NEWS BURUDANI ENGLISH NEWS GOSIIP GOSPEL HABARI HABARI PICHA MAGAZETI MAKALA MATUKIO MICHEZO MUSIC VIDEO WAZO LANGU
false
ltr
item
WEPESI MEDIA : Zitambue Simu ambazo hazifanyi kazi tena na WhatsApp.!
Zitambue Simu ambazo hazifanyi kazi tena na WhatsApp.!
http://ichef.bbci.co.uk/news/660/cpsprodpb/A6C7/production/_93259624_93a8ff19-86bc-4596-b2fc-8152be6cccee.jpg
WEPESI MEDIA
https://wepesimedia.blogspot.com/2017/01/zitambue-simu-ambazo-hazifanyi-kazi.html
https://wepesimedia.blogspot.com/
http://wepesimedia.blogspot.com/
http://wepesimedia.blogspot.com/2017/01/zitambue-simu-ambazo-hazifanyi-kazi.html
true
925270315725722404
UTF-8
Not found any posts VIEW ALL Readmore Reply Cancel reply Delete By Home PAGES POSTS View All

USIPITWE NA HIZI HAPA CHINI LABEL ARCHIVE SEARCH ALL POSTS Not found any post match with your request Back Home Sunday Monday Tuesday Wednesday Thursday Friday Saturday Sun Mon Tue Wed Thu Fri Sat January February March April May June July August September October November December Jan Feb Mar Apr May Jun Jul Aug Sep Oct Nov Dec just now 1 minute ago $$1$$ minutes ago 1 hour ago $$1$$ hours ago Yesterday $$1$$ days ago $$1$$ weeks ago more than 5 weeks ago Followers Follow THIS CONTENT IS PREMIUM Please share to unlock Copy All Code Select All Code All codes were copied to your clipboard Can not copy the codes / texts, please press [CTRL]+[C] (or CMD+C with Mac) to copy