http://wepesimedia.blogspot.com/p/blog-page.html

post-feature-image

Kuku wamtoa roho Mwanaume mmoja


TANGAZA NASISI KWA BEI NAFUU NA UPATE MATOKEO MAZURI KATIKA BIASHARA YAKO.

Mwanaume mmoja mkazi wa kitongoji cha Busulwa kata ya Ngulla Wilaya ya Kwimba Mkoani Mwanza ameuawa na kikundi cha watu wasiyojulikana...

Flora ajibu kuhusu mtoto
SIRI YA KITAMBI CHA JB KUYEYUKA!
Sharobaro Yamkuta Mazito Muhimbili!




Mwanaume mmoja mkazi wa kitongoji cha Busulwa kata ya Ngulla Wilaya ya Kwimba Mkoani Mwanza ameuawa na kikundi cha watu wasiyojulikana kwa kosa la kuiba kuku watano wa Ester Robert ambaye ni mkazi wa Kijiji cha Ngulla.

Kamanda wa Polisi Mkoani Mwanza, DCP Ahmed Msangi amemtaja mwanaume huyo kuwa ni Leonard Mathias (23) ambapo kabla ya kuuawa alipigwa fimbo na mawe sehemu mbalimbali za mwili wake kisha kuchomwa moto hadi kupoteza maisha na kikundi cha watu wanaojichukulia sheria mkononi mnamo tarehe 21.08.2017 majira ya saa 2:45 asubuhi.

Inasemekana kuwa marehemu aliiba kuku hao nyumbani kwa Bi. Ester kisha kukimbia nao kijiji cha jirani cha Mwabomba ambako huko mwananchi walipomuona walipata mashaka kisha kumkamata na baadaye kutoa taarifa Kijiji cha Ngula ndipo mwenye Kuku alipofika na kukabidhiwa kuku wake.

DCP Msangi amesema mara baada mwenye mali kupokea Kuku wake, wananchi walimchukua na kwenda naye kituo cha Polisi lakini wakiwa njiani walianza kumshambulia kwa kumpiga kwa fimbo na mawe sehemu mbalimbali za mwili wake na baadae kumchoma moto. Polisi walipata taarifa kutoka kwa raia wema ndipo walifanya ufuatiliaji wa haraka hadi eneo na tukio na kufanikiwa kuwakamata watu saba ambao wanadaiwa kuhusika kwa namna moja ama nyingine katika mauaji hayo.

Jeshi la Polisi linaendelea na mahojiano ya watuhumiwa hao na pindi uchunguzi utakapokamilika kishha ikithibitika kuwa walihusika katika mauaji hayo watafikishwa Mahakamani.

Name

BIASHARA NA UCHUMI BREAKING NEWS BURUDANI ENGLISH NEWS GOSIIP GOSPEL HABARI HABARI PICHA MAGAZETI MAKALA MATUKIO MICHEZO MUSIC VIDEO WAZO LANGU
false
ltr
item
WEPESI MEDIA : Kuku wamtoa roho Mwanaume mmoja
Kuku wamtoa roho Mwanaume mmoja
http://www.eatv.tv/sites/default/files/styles/detailpageimg/public/news/2017/08/22/Kuku.jpg?itok=ARCZdccJ×tamp=1503403735
WEPESI MEDIA
https://wepesimedia.blogspot.com/2017/08/kuku-wamtoa-roho-mwanaume-mmoja.html
https://wepesimedia.blogspot.com/
http://wepesimedia.blogspot.com/
http://wepesimedia.blogspot.com/2017/08/kuku-wamtoa-roho-mwanaume-mmoja.html
true
925270315725722404
UTF-8
Not found any posts VIEW ALL Readmore Reply Cancel reply Delete By Home PAGES POSTS View All

USIPITWE NA HIZI HAPA CHINI LABEL ARCHIVE SEARCH ALL POSTS Not found any post match with your request Back Home Sunday Monday Tuesday Wednesday Thursday Friday Saturday Sun Mon Tue Wed Thu Fri Sat January February March April May June July August September October November December Jan Feb Mar Apr May Jun Jul Aug Sep Oct Nov Dec just now 1 minute ago $$1$$ minutes ago 1 hour ago $$1$$ hours ago Yesterday $$1$$ days ago $$1$$ weeks ago more than 5 weeks ago Followers Follow THIS CONTENT IS PREMIUM Please share to unlock Copy All Code Select All Code All codes were copied to your clipboard Can not copy the codes / texts, please press [CTRL]+[C] (or CMD+C with Mac) to copy