mangekimambi_ Kwa wale wanaodhani eti mimi siogopi, naogopa sana tuuuuuu. Hamjaniona kila siku asubuhi navyopiga sala kabla sijawas...
- mangekimambi_Kwa
wale wanaodhani eti mimi siogopi, naogopa sana tuuuuuu. Hamjaniona kila
siku asubuhi navyopiga sala kabla sijawasha gari yangu kwa kuogopa
italipuka nikiiwasha. Au jinsi navyowasimamisha wanangu nje ya gari
naingia mwenyewe naiwasha kwanza ndo nawaingiza watoto. Au jinsi
navyotoa mimacho kila pande napokuwa nawashusha watoto shule au nikiwa
nawachukua. Au jinsi navyoogopa kwenda kwenye maandamano Washington DC
tarehe 25 April sababu sasa wanajua exactly wapi watanipatia ila ni
lazma niende. Siwezi kukosa!!! Ila lazma niombe polisi hata wawili waje
kwenye maandamano, chezea kufa wewe🤣🤣 angalau nikitunguliwa na wao
wakamatwe..
.
.
Ndio naogopa kufa, tena najua Kagame anauwaga maadui zake nchi yoyote ile na sasa hivi mtu anaetaka kumtoa Magufuli madarakani Kagame hawezi kumwacha salama maana sasa dream yake ya kuicontrol TZ imecome true. Kumbuka Kagame mpaka katoa jeshi lake kumlinda Magufuli.
.
.
My point is ndio naogopa kufa, staki kuacha watoto wangu bado wadogo but guess what na Nyerere angesema aogope ingekuwaje? Mandela angesema aogope kufa ingekuwaje? Kina Martin Luther King kina Malcom X wangesema waongope kufa ingekuwaje?? Ndio naogopa kufa ila siwezi kuacha kuitetea haki eti sababu ya kifo. Ni bora nife nikiipigania haki kuliko niishi maisha yasiyo na purpose!
.
.
Mijitu ya CCM eti oooh njoo huku na wewe uandamane? Hivi you fools think mi naogopa kuja bongo? Siogopi kufungwa, nachoogopa ni kitu kimoja tu hapa duniani, nachoogopa ni kutokuwa na msaada wowote kwa wanyonge.Na nikirudi TZ ni straight jela sitokuwa na Msaada wowote hata hayo maandamano sitoyaona kwenye TV.
.
.
Unaeniambia mimi nirudi kuongoza maaandamano jua kuwa nipo tayari kurudi hata leo ila not for nothing, Magufuli anipe something in return. Magufuli akikubali kuwapa watanzania katiba mpya na kutoa ahadi kuwa hatokaaa kubadili katiba kujiongezea muda narudi Tanzania on the next flight. Hiyo ni sababu nzuri ya mimi kufungwa. Ila eti nijilete nifungwe kisenge tu for nothing. Never!
.
.
Sasa shemeji yenu ananitaniaga eti siku hao watu wako wakitokea na bunduki zao ntatimua mbio hizo hutoamini ni mimi 😂