Mrisho Mpoto akizungumza na wadau. Msanii wa muziki, Mrisho Mpoto ambaye pia ni Balozi wa Mamlaka ya Hifadhi ya Ngorongoro baada ya wiki ...
Mrisho Mpoto akizungumza na wadau.
Msanii wa muziki, Mrisho Mpoto ambaye pia ni Balozi wa Mamlaka ya Hifadhi ya Ngorongoro baada ya wiki hii kuachia wimbo wake mpya ‘Kitendawili’ akiwa amemshirikisha muimbaji Kassim Mganga, Ijumaa hii ametua jijini Arusha kwaajili ya maonesho ya 24 ya kilimo na sherehe za ‘Nanenane’ mwaka 17 Kanda ya Kaskazini.
Bendi yake wakicheza.
Mshairi huyo ambaye amekuwa mstari wa mbele katika kutangaza vivutio vya utalii nchini pamoja na utamaduni wa Tanzania, amewataka wakulima pamoja na watanzania nchini kutembelea hifadhi ya Ngorongoro ili kujifunza na kuona mambo mengi ambayo hayapatikani sehemu yoyote zaidi ya Tanzania.
Bendi ya Mpoto imetoa burudani pamoja na elimu kwa umati mkubwa wa watu uliojikusanya katika banda hilo huku burudani hiyo ikiambatana elimu kuhusu hifadhi hiyo.
Wakizidi kukamua.
Akiongea na waandishi wa habari waliojitokeza katika maonyesha hayo, Mpoto amewaka wananchi kujiwekea utamadani wa kutembelea hifadhi za taifa kwa kuwa ni sehemu ambao inaweza kuwajenga watu na kufahamu mambo mengi kuhusu rasilimali walizonazo.
Burudani zikiendelea.
“Hii ni Nane Nane na tukizungumzia Nane Nane ni wakulima au mazao ya kilimo yanayozalishwa ndani na kusindikwa kuwa bidhaa. Lakini mimi kama balozi wa Hifadhi ya Ngorongoro ndani ya siku hii muhimu kwa taifa letu nikiwa pamoja na hifadhi ya Ngorongoro tumekuletetea ofa ya kwenye Ngorongoro katika msimu huu wa Nanenane kwa kiwango cha chini zaidi ili kila mtu aende kujionea maajabu, ni shilingi 50,000 tu ukiwa hapa Arusha mjini itaweza kukupeleka Ngorongoro hiyo hiyo usafiri wa kwenda na kurudi, chakula, kiingilio pamoja na kupewa mtu ambaye atakuongoza kukupeleka katika vivutio vyote vya Ngorongoro,” alisema Mpoto.
Mashabiki wakimshuhudia mpoto.
Aliongeza, “Kuna wakati tunaona mambo ni magumu unahitaji bajeti kubwa kumbe sio, ukiwa na pesa kama hiyo unafurahi kabisa,tena watoto ni tsh 20000 tu sasa kazi ni kwako kuna siku tatu kuanzia tarehe 6,7 na 8,”
Mpoto akizungumza na wadau.
Kwa upande wa Afisa Hifadhi ya Ngorongoro, Peter Makutian. amesema Ngorongoro bado inahitaji watanzania wengi kwa kuwa ina vitu vingi ambavyo kila mtanzania anahitaji kuvijunia huku akieleza kituko kipya cha hivi karibuni kilichotokea kwenye hifadhi hiyo baada ya Simba kuonekana akimnyonyesha mtoto wa Chui.
Akipiga picha na watoto.
“Ngorongoro kuna mambo mengi sana kama mlivyosikia hivi karibuni kuna Simba ameonekana akimnyonyesha mtoto wa chui, hiyo ni kweli imetokea ni kitu ambacho hakijawahi kutokea na kuonekana duniani kwa sababu ni wanyama ambao kila mmoja ana mfumo wake wa maisha, kwa hiyo mnakaribishwa kushuhudia hilo,” alisema.