http://wepesimedia.blogspot.com/p/blog-page.html

post-feature-image

Polisi waua mtu mmoja akidaiwa kuwa jambazi


TANGAZA NASISI KWA BEI NAFUU NA UPATE MATOKEO MAZURI KATIKA BIASHARA YAKO.

Mkazi wa kijiji cha Shiponga, Hanang Mkoani Manyara anayedaiwa kuwa jambazi, Hamisi Athumani (32), amefariki dunia baada ya kupigwa risasi ...

BREAKING NEWS: Kijana wa Miaka 18 Aliyekamatwa Kwa Tuhuma ya Utekaji na Uuaji wa Watoto Arusha Afariki
PICHA: NG'OMBE 600 WACHINJWA KATIKA SHEREHE YA EID AL ADHA JIJINI DAR ES SALAAM
Mwanamke akifanyiwa hiki atakuheshimu - Lusekolo

Mkazi wa kijiji cha Shiponga, Hanang Mkoani Manyara anayedaiwa kuwa jambazi, Hamisi Athumani (32), amefariki dunia baada ya kupigwa risasi kiunoni na askari polisi wakati akiwa katika harakati ya kutoroka.

Kamanda wa Jeshi la Polisi Mkoani hapa, ACP Debora Magiligimba, amesema tukio hilo limetokea Agosti 25 mwaka huu saa nane mchana, huko katika kijiji cha Mgori tarafa ya Ngimu wilaya ya Singida.

Amefafanua kuwa Hamisi (marehemu) alipigwa risasi na askari polisi wakati akijaribu kuwatoroka mara baada kuonyesha bunduki aina ya rifle yenye namba 7358 na risasi zake tano.

Amesema bunduki hiyo iliyokuwa imekatwa mtutu na risasi zake tano zilikuwa zimefichwa kwenye soksi, vitu hivyo vilikuwa vilihifadhiwa kwenye mfuko wa sandarusi, na kufichwa chini ya jiwe.

ACP Magiligimba amesema Agosti 23 mwaka huu, mtuhumiwa alikamatwa na wananchi wa kijiji cha Ngamu, na kufikishwa katika kituo cha polisi cha kijiji hicho kwa tuhuma ya kujihusisha na matukio ya ujambazi.

“Kesho yake mtuhumiwa alihojiwa na kukiri kujihusisha na matukio ya ujambazi wa kutumia silaha katika mikoa mbalimbali. Pia aliahidi kuwapeleka askari kuwaonyesha mahali alikoificha silaha anayoitumia kwenye matukio hayo ya ujambazi,” amesema ACP Magiligimba.

Kamanda huyo amesema Agosti 25 mwaka huu saa sita mchana, askari polisi wakiwa na mtuhumiwa, walikwenda katika pori la kijiji cha Mgori mahali alipokuwa ameficha bunduki hiyo aina ya rifle.

“Mara tu baada ya kuwaonyesha askari hao silaha hiyo na wakati askari wanaendelea kufanya upekuzi katika eneo hilo, mtuhumiwa alijaribu kutoroka askari kwa kukimbia” amesema na kuongeza.

“Askari mmoja alifyatua risasi tatu hewani akimtaka asimame, lakini hakutii. Ndipo alipompiga risasi moja iliyompata sehemu ya kiunoni”.

Amesema jereha hilo la risasi lilisababisha mtuhumiwa Hamisi avuje damu nyingi, na hivyo kufariki dunia wakati akikimbizwa hospitali ya mkoa kwa matibabu.

“Jeshi la Polisi Mkoa wa Singida linaendelea kutoa wito kwa wananchi waote kutoa taarifa zitakazosaidia kubaini wahalifu katika maeneo yao ili hatua ziweze kuchukuliwa kudhibiti vitendo vya kihalifu,” amesema kamanda huyo.

Name

BIASHARA NA UCHUMI BREAKING NEWS BURUDANI ENGLISH NEWS GOSIIP GOSPEL HABARI HABARI PICHA MAGAZETI MAKALA MATUKIO MICHEZO MUSIC VIDEO WAZO LANGU
false
ltr
item
WEPESI MEDIA : Polisi waua mtu mmoja akidaiwa kuwa jambazi
Polisi waua mtu mmoja akidaiwa kuwa jambazi
http://dewjiblog.co.tz/wp-content/uploads/2017/08/IMG_4783-750x375.jpg
WEPESI MEDIA
https://wepesimedia.blogspot.com/2017/08/polisi-waua-mtu-mmoja-akidaiwa-kuwa.html
https://wepesimedia.blogspot.com/
http://wepesimedia.blogspot.com/
http://wepesimedia.blogspot.com/2017/08/polisi-waua-mtu-mmoja-akidaiwa-kuwa.html
true
925270315725722404
UTF-8
Not found any posts VIEW ALL Readmore Reply Cancel reply Delete By Home PAGES POSTS View All

USIPITWE NA HIZI HAPA CHINI LABEL ARCHIVE SEARCH ALL POSTS Not found any post match with your request Back Home Sunday Monday Tuesday Wednesday Thursday Friday Saturday Sun Mon Tue Wed Thu Fri Sat January February March April May June July August September October November December Jan Feb Mar Apr May Jun Jul Aug Sep Oct Nov Dec just now 1 minute ago $$1$$ minutes ago 1 hour ago $$1$$ hours ago Yesterday $$1$$ days ago $$1$$ weeks ago more than 5 weeks ago Followers Follow THIS CONTENT IS PREMIUM Please share to unlock Copy All Code Select All Code All codes were copied to your clipboard Can not copy the codes / texts, please press [CTRL]+[C] (or CMD+C with Mac) to copy