Dar es Salaam. Mabingwa wa Kombe la FA, Simba imefanikiwa kuwasajili wachezaji wawili beki wa Toto Africans, Yusuph Mlipili pamoja na Ahm...
Dar es Salaam. Mabingwa wa Kombe la FA, Simba imefanikiwa kuwasajili wachezaji wawili beki wa Toto Africans, Yusuph Mlipili pamoja na Ahmed Msumi wa Ndanda.
Chanzo cha uhakika kutoka ndani ya Simba kilisema wachezaji hao kila mmoja ametimiziwa matakwa yake aliyotaka kabla ya kutia saini.
"Mazungumzo na Msumi yalianza mapema zaidi na sasa tutamalizana naye, tunashukuru Mungu tumekamilisha usajili huo," alisema.
"Kikosi kimeanza mazoezi leo Jumamosi katika Uwanja wa Polisi Kurasini kwa ajili ya maandalizi
ya Kombe la SportPesa," alisema.
Kigogo huyo alisema kuwa usajili wa Yusuph ulikuwa wa ushindani kwani Yanga, Azam na Singida United walikuwa wanamuhitaji pia.
"Tunaendelea na usajili wetu kimya kimya, lakini katika wachezaji ambao tumeshawasajili hakukua na vikwazo vingi kama tulivyokutana navyo kwa Yusuph," alisema.
Simba bado tunaendelea na usajili na tupo katika mazungumzo na wachezaji wengi wa ndani na nje ya nchi na muda si mrefu tutamalizana nao kama tulivyofanya kwa hawa wengine.
"Kama ripoti ya kocha inavyosema kuwa tunatakiwa kusajili wachezaji katika baadhi ya maeneo ambayo yalikuwa na mapungufu msimu uliopita basi kamati ya usajili ikiongozwa na Hans Pope wataendelea kukamilisha zoezi hilo," alisema.
Simba wameingia kambini chini ya kocha Joseph Omog na Nicko Kihondo wakiwa na wachezaji Juma Luizio, Agyei, James Kotei, Fredreck Blagnon, Basela Bokungu, Peter Manyika, Denis Richad, Mohamed Kijiko na wachezaji wengine kutoka timu ya vijana.
"Wachezaji hao ndio wapo kambini kwa sasa huku kocha Jackson Mayanja akiwa hajawasili bado kwa kuwa na matatizo ya kifamilia huko kwao Uganda na timu inafanya mazoezi mara moja kwa siku na kesho,Jumapili tutacheza mechi ya kirafiki hapa hapa katika uwanja wa Polisi Kurasini," alisema