http://wepesimedia.blogspot.com/p/blog-page.html

Mtoto auawa kinyama, ang'olewa Sehemu za Siri na Macho

Katika hali isiyokuwa ya kawaida mtoto wa miaka 12, Dorcas Meshak mkazi wa kitongoji cha Mbughantigha kijiji cha Matongo tarafa ya Ikungi,...

Katika hali isiyokuwa ya kawaida mtoto wa miaka 12, Dorcas Meshak mkazi wa kitongoji cha Mbughantigha kijiji cha Matongo tarafa ya Ikungi, ameuawa na watu wasiojulikana na kunyofolewa baadhi ya viungo vyake.

Akizungumza kuhusu tukio hilo, Kaimu Kamanda Jeshi la Polisi mkoani hapa, SSP Isay Mbugh alisema Mei, 18 mwaka huu saa sita mchana wakati ambao Dorcas alipoondoka nyumbani kwao kwa lengo la kwenda shambani kuchuma mahindi, umbali wa kilometa 70.

Alisema mtoto huyo amenyofolewa macho yote mawili, kukatwa matiti yote na kuondolewa sehemu zake za siri.

“Mtoto Dorcas hakuweza kurudi nyumbani kitendo kilichosababisha ipigwe yowe ili watu wakusanyike kwa ajili ya kumtafuta. Haikuchukua muda mrefu, mwili wa Dorcas ulikutwa ukiwa umenyongwa hadi kufa kwa kamba ya ngozi,” alisema.

Alisema uchunguzi wa awali umebaini kuwa mauaji hayo yanahusishwa na imani za ushirikina na hadi sasa hakuna watu waliokamatwa kuhusiana na mauaji hayo.

Katika tukio la pili, Kaimu Kamanda Mbugh, alisema watu wawili wamepoteza maisha kufuatia kutokea ajali ya gari anina ya Noah, tukio ambalo lilitokea Mei, 20 mwaka huu saa 6.45 mchana huko katika kijiji cha Mwaja tarafa ya Unyankumi Manispaa ya Singida.

“Ajali hiyo imehusisha noah T.402 DFH iliyokuwa ikiendeshwa na Said Shaban (33), na chanzo cha ajali ni mwendo kasi kitendo kilichosababisha ashindwe kulimudu. Waliofariki kwenye ajali hiyo,ni Elia Daniel (34) mkulima kijiji cha Mwankoko na mwanamke mmoja ambaye jina wala makazi yake,hayajafahamika,” alisema.

Aidha, aliwataja majeruhi wa ajali hiyo kuwa ni Mratibu Elimu kata ya Mtamaa, Nicodem Elias (45), Juma Ramadhan, mwalimu Chuo cha Maendeleo ya Wananchi, Elia Bilau mkulima na mkazi wa Magungumka Kapela Donad (28).

Kaimu kamanda huyo, alisema dereva wa Noah hiyo Said Shaban anashikiliwa na Jeshi la Polisi na upepelezi ukikamilika atafikishwa mahakamani kujibu tuhuma zinazomkabili.

CREDIT: Mo Blog

COMMENTS


TANGAZA NASISI KWA BEI NAFUU NA UPATE MATOKEO MAZURI KATIKA BIASHARA YAKO.

MAGAZETI$type=sticky$count=4


Name

BIASHARA NA UCHUMI BREAKING NEWS BURUDANI ENGLISH NEWS GOSIIP GOSPEL HABARI HABARI PICHA MAGAZETI MAKALA MATUKIO MICHEZO MUSIC VIDEO WAZO LANGU
false
ltr
item
WEPESI MEDIA : Mtoto auawa kinyama, ang'olewa Sehemu za Siri na Macho
Mtoto auawa kinyama, ang'olewa Sehemu za Siri na Macho
https://blogger.googleusercontent.com/img/b/R29vZ2xl/AVvXsEipdNRAMjV-eY4guFWK1LUZM1WoMKeYssaCevEpWGPPILXcU8IUvHrkjUOcvxPNQ1Cm83zL0KiyUVuuJBf0lOzXsPbhUpqnxh8jVMyqWYBnGZNwicp4OaBErGY3b0ed50auy-CUEih_yv_3/s640/bad_news.jpg
https://blogger.googleusercontent.com/img/b/R29vZ2xl/AVvXsEipdNRAMjV-eY4guFWK1LUZM1WoMKeYssaCevEpWGPPILXcU8IUvHrkjUOcvxPNQ1Cm83zL0KiyUVuuJBf0lOzXsPbhUpqnxh8jVMyqWYBnGZNwicp4OaBErGY3b0ed50auy-CUEih_yv_3/s72-c/bad_news.jpg
WEPESI MEDIA
https://wepesimedia.blogspot.com/2017/05/mtoto-auawa-kinyama-angolewa-sehemu-za.html
https://wepesimedia.blogspot.com/
http://wepesimedia.blogspot.com/
http://wepesimedia.blogspot.com/2017/05/mtoto-auawa-kinyama-angolewa-sehemu-za.html
true
925270315725722404
UTF-8
Not found any posts VIEW ALL Readmore Reply Cancel reply Delete By Home PAGES POSTS View All

USIPITWE NA HIZI HAPA CHINI LABEL ARCHIVE SEARCH ALL POSTS Not found any post match with your request Back Home Sunday Monday Tuesday Wednesday Thursday Friday Saturday Sun Mon Tue Wed Thu Fri Sat January February March April May June July August September October November December Jan Feb Mar Apr May Jun Jul Aug Sep Oct Nov Dec just now 1 minute ago $$1$$ minutes ago 1 hour ago $$1$$ hours ago Yesterday $$1$$ days ago $$1$$ weeks ago more than 5 weeks ago Followers Follow THIS CONTENT IS PREMIUM Please share to unlock Copy All Code Select All Code All codes were copied to your clipboard Can not copy the codes / texts, please press [CTRL]+[C] (or CMD+C with Mac) to copy