Mtoto anayekadiriwa kuwa na umri wa miaka sita mpaka nane mkazi wa kijiji cha Nyakatuntu wilayani Biharamulo mkoani Kagera amefariki dun...

Mtoto anayekadiriwa kuwa na umri wa miaka sita mpaka nane mkazi wa kijiji cha Nyakatuntu wilayani Biharamulo mkoani Kagera amefariki dunia papo hapo huku mwenzake akinusurika baada ya kugongwa na gari lililopoteza mwelekeo katika maegesho ya magari ya kanisa katoliki kigango cha biharamulo mjini mda mfupi kabla ya kuingia kanisani kusali misa ya tatu ambayo ni misa ya watoto
Mtoto huyo aliyefariki ametambulika kwa jina la James Charles Mwendapole ambapo gari iliyosababisha ajali ni aina ya Noa yenye namba T 784 DHM ambapo ilikuwa ikiendeshwa na muumini aliyetoka kanisani kusali misa ya pili na kwa bahati mbaya wakati akitoa gari lake kwenye maegesho ya kanisa akamgonga mtoto huyo aliyekuwa akisubiria kuingia misa ya tatu huku waumini wakitoa maoni kuhusiana na tukio hilo.
Mganga mkuu wa hospitali teule ya wilaya ya Biharamulo Dr. Gresimus Sebuyoya amesema kuwa kifo cha mtoto huyo kimetokana na majeraha makubwa aliyoyapata kichwani pamoja na kuvuja damu nyingi wakati wa ajali hiyo na amefikishwa hospitalini akiwa tayari amefariki licha ya kwamba kanisa hilo lipo mita chache mkabala na hospitali teule ya wilaya ya Biharamulo
Jeshi la polisi wilaya ya Biharamulo linamshikilia mtuhumiwa wa ajali hiyo pamoja na gari aina ya NOA lenye namba za usajili T 784 DHM kwa uchunguzi zaidi wa tukio hilo lililoacha simanzi kwa familia na wakristo wote waliokuwa wamefika kanisani hapo kwa ajili ya Ibada.



