http://wepesimedia.blogspot.com/p/blog-page.html

post-feature-image

Polepole Aitaka CCM Imchukulie Hatua za Kinidhamu Nape Nnauye


TANGAZA NASISI KWA BEI NAFUU NA UPATE MATOKEO MAZURI KATIKA BIASHARA YAKO.

Katibu wa Itikadi na Uenezi wa Chama Cha Mapinduzi (CCM), Humphrey Polepole amelaani vikali kauli iliyotolewa na mtangulizi wake ambaye n...

Mkurugenzi wa Facebook, Mark Zuckerberg Atiwa kikaangoni
Rais John Magufuli atengua uteuzi wa Mwenyekiti wa Bodi ya Wakurugenzi ya Shirika la Nyumba la Taifa(NHC),
Amuua Mkewe na Kuificha Maiti Kwenye Mbuyu kwa Miaka 8

Katibu wa Itikadi na Uenezi wa Chama Cha Mapinduzi (CCM), Humphrey Polepole amelaani vikali kauli iliyotolewa na mtangulizi wake ambaye ni mbunge wa jimbo la Mtama, Nape Nnauye kuwa alisaidia kukitoa chama hicho shimoni.


Nape alitoa kauli hiyo dakika chache baada ya mkutano wake na waandishi wa habari kuzuiwa na kutishiwa bastola na mtu mmoja, siku moja baada ya kuondolewa kwenye nafasi ya Uwaziri wa Habari, Utamaduni, Sanaa na Michezo.


Polepole alisema kuwa kauli hiyo ya Nape sio kauli sahihi ya kiongozi na kwamba yeye pekee hawezi kukitoa chama shimoni huku kukiwa na wanachama milioni nane na maelfu ya viongozi.


“Mwanachama anayejitambua hawezi kusema anakibeba chama, wanachama wote milioni nane walikuwa wapi? Viongozi wote maelfu walikuwa wapi? Nape ni kiongozi wetu kwenye chama, kama kweli alisema maneno hayo alikengeuka sana,” Polepole anakaririwa na Mwananchi.


Katibu huyo wa Itikadi na Uenezi wa CCM alisema kuwa Kamati ya Maadili inapaswa kuliangalia suala hili na kumchukulia hatua Nape.


“Tuna kila sababu za kumshauri Mzee Mangula wa Kamati ya maadili kuwa hatuwezi kuwa na viongozi wa aina hii. Chama chenye watu milioni nane unakitoa shimoni na nini? Unakitoa na ngazi, ulitumia kamba kukitupia shimoni, uliita zimamoto? "Alihoji.


Hata hivyo, Polepole alisema kuwa hatua zinazopaswa kuchukuliwa kwa viongozi kama Nape sio za kuwawekea ukomo bali kuwalea kimaadili kwa kutumia hekima na busara ili watambue kuwa chama sio punda anayeweza kutumbukia shimoni.


Hivyo, alisema CCM iko kwenye mpango wa kuanzisha chuo kikuu kitakachotoa mafunzo kwa makada wake kuhusu nidhamu na maadili.

Name

BIASHARA NA UCHUMI BREAKING NEWS BURUDANI ENGLISH NEWS GOSIIP GOSPEL HABARI HABARI PICHA MAGAZETI MAKALA MATUKIO MICHEZO MUSIC VIDEO WAZO LANGU
false
ltr
item
WEPESI MEDIA : Polepole Aitaka CCM Imchukulie Hatua za Kinidhamu Nape Nnauye
Polepole Aitaka CCM Imchukulie Hatua za Kinidhamu Nape Nnauye
https://blogger.googleusercontent.com/img/b/R29vZ2xl/AVvXsEgUErbRh-a5KsNuFUjyFuuFLHAl-JlqW9m4_ns1P5L01w93R1A4DMcR8pSu6DKV_pzY5809dcOkvJxFJWT0CzXkaM3b15tYbulZ05HXLTsjlj_Mk1rGLLn-BY0oFKDRdyqD9Kvfob6e5qXJ/s640/1.jpg
https://blogger.googleusercontent.com/img/b/R29vZ2xl/AVvXsEgUErbRh-a5KsNuFUjyFuuFLHAl-JlqW9m4_ns1P5L01w93R1A4DMcR8pSu6DKV_pzY5809dcOkvJxFJWT0CzXkaM3b15tYbulZ05HXLTsjlj_Mk1rGLLn-BY0oFKDRdyqD9Kvfob6e5qXJ/s72-c/1.jpg
WEPESI MEDIA
https://wepesimedia.blogspot.com/2017/04/polepole-aitaka-ccm-imchukulie-hatua-za.html
https://wepesimedia.blogspot.com/
http://wepesimedia.blogspot.com/
http://wepesimedia.blogspot.com/2017/04/polepole-aitaka-ccm-imchukulie-hatua-za.html
true
925270315725722404
UTF-8
Not found any posts VIEW ALL Readmore Reply Cancel reply Delete By Home PAGES POSTS View All

USIPITWE NA HIZI HAPA CHINI LABEL ARCHIVE SEARCH ALL POSTS Not found any post match with your request Back Home Sunday Monday Tuesday Wednesday Thursday Friday Saturday Sun Mon Tue Wed Thu Fri Sat January February March April May June July August September October November December Jan Feb Mar Apr May Jun Jul Aug Sep Oct Nov Dec just now 1 minute ago $$1$$ minutes ago 1 hour ago $$1$$ hours ago Yesterday $$1$$ days ago $$1$$ weeks ago more than 5 weeks ago Followers Follow THIS CONTENT IS PREMIUM Please share to unlock Copy All Code Select All Code All codes were copied to your clipboard Can not copy the codes / texts, please press [CTRL]+[C] (or CMD+C with Mac) to copy