http://wepesimedia.blogspot.com/p/blog-page.html

post-feature-image

Waziri Mwigulu : Aliyemtishia Nape kwa bastola sio polisi


TANGAZA NASISI KWA BEI NAFUU NA UPATE MATOKEO MAZURI KATIKA BIASHARA YAKO.

Waziri wa Mambo ya Ndani, Mwigulu Nchemba amesema mtu aliyemtishia kwa bastola aliyekuwa Waziri wa Habari, Utamaduni, Sanaa na Michezo, N...

Watumishi vyeti feki warudi kazini
Breaking News: Matokea Kidato cha 6 Mwaka 2017 Yametoka.....Bofya hapa kuyatazama
VITUO 57 VYA MAFUTA VYAFUNGIWA ARUSHA KWA KUKOSA MASHINE ZA EFD,s

Waziri wa Mambo ya Ndani, Mwigulu Nchemba amesema mtu aliyemtishia kwa bastola aliyekuwa Waziri wa Habari, Utamaduni, Sanaa na Michezo, Nape Nnauye si askari wa Jeshi la Polisi, lakini ameshapatikana na atashughulikiwa kwa mujibu wa utaratibu wa ulinzi na usalama.


Mwigulu alisema hayo baada ya kufungua mkutano wa kazi wa mwaka wa maofisa waandamizi wa polisi, makamanda wa mikoa na wakuu wa vikosi wa Jeshi la Polisi ambao unafanyika mjini hapa.


“Ameshapatikana (aliyemtishia Nape) na atashughulikiwa kwa mujibu wa taratibu za ulinzi na usalama ambazo zimekuwa zikifanyika ndani, lakini hazitangazwi,”alisema.


Hata hivyo, Mwigulu alikataa kuelezea kwa undani kuhusu mtu huyo kwa kubainisha anatoka taasisi gani wala jina la mtuhumiwa kwa madai kuwa ni kwa sababu ya usalama wake.


Baadhi ya taasisi za ulinzi na usalama nchini ni Jeshi la Wananchi wa Tanzania, Usalama wa Taifa na Takukuru.


Mtu huyo alifanya kitendo hicho wakati Nape, ambaye alikuwa Waziri wa Habari, alipokuwa anaelekea Hoteli ya Protea alikopanga kuzungumza na waandishi wa habari baada ya mbunge huyo wa Mtama kuachwa katika mabadiliko madogo ya Baraza la Mawaziri.


Mtu huyo alikuwa pamoja na wenzake wawili ambao kwa pamoja walikuwa wakimlazimisha arudi kwenye gari lake na kuondoka, lakini Nape alibisha na ndipo mtu huyo aliporudi nyuma, kuchomoa bastola kutoka kiunoni na kisha kumtishia kabla ya kutulizwa na mwenzake.


Watu hao walitoweka eneo hilo muda mfupi baadaye.


Siku moja baada ya tukio hilo Mwigulu alimwagiza Mkuu wa Jeshi la Polisi, Ernest Mangu kumtafuta mtu huyo.


Mwigulu aliandika katika ukurasa wake wa twitter akisema:


“Mh Nape sio jambazi, hana record za uhalifu. Kitendo cha kutolewa bastola si cha Kitanzania na si cha kiaskari. Nimemuagiza IGP achukue hatua.”


Tukio hilo lilitokea siku chache baada ya RC Paul Makonda kuvamia kituo cha televisheni cha kampuni ya Clouds Media, akiwa na askari wenye silaha za moto na kulazimisha arekodiwe mahojiano baina ya watangazaji wa kipindi cha Shirika la Wambeya Duniani (Shilawadu) na mwanamke anayedai kuzaa na Askofu wa Kanisa la Ufufuo na Uzima, Josephat Gwajima, ambaye ameibukia kuwa mpinzani wa kiongozi huyo.


Hadi sasa, Jeshi la Polisi halijaeleza kuhusu askari hao waliojumuika kufanikisha uvamizi huo.

Name

BIASHARA NA UCHUMI BREAKING NEWS BURUDANI ENGLISH NEWS GOSIIP GOSPEL HABARI HABARI PICHA MAGAZETI MAKALA MATUKIO MICHEZO MUSIC VIDEO WAZO LANGU
false
ltr
item
WEPESI MEDIA : Waziri Mwigulu : Aliyemtishia Nape kwa bastola sio polisi
Waziri Mwigulu : Aliyemtishia Nape kwa bastola sio polisi
https://blogger.googleusercontent.com/img/b/R29vZ2xl/AVvXsEga3AjFvvQK7wFxGxA57k2VrGTwgnRkwS_DK2dlBZ4GI9j0_HC_qYphyphenhyphenvYrrTvW2D-EHtKOVNP3iyG4fD54z165jsHoeFdAuP7LjIqcUVPo3OLEaAEBQhKntbphJgu4E9pGOsfTZ8j3DgcB/s640/1.jpg
https://blogger.googleusercontent.com/img/b/R29vZ2xl/AVvXsEga3AjFvvQK7wFxGxA57k2VrGTwgnRkwS_DK2dlBZ4GI9j0_HC_qYphyphenhyphenvYrrTvW2D-EHtKOVNP3iyG4fD54z165jsHoeFdAuP7LjIqcUVPo3OLEaAEBQhKntbphJgu4E9pGOsfTZ8j3DgcB/s72-c/1.jpg
WEPESI MEDIA
https://wepesimedia.blogspot.com/2017/03/waziri-mwigulu-aliyemtishia-nape-kwa.html
https://wepesimedia.blogspot.com/
http://wepesimedia.blogspot.com/
http://wepesimedia.blogspot.com/2017/03/waziri-mwigulu-aliyemtishia-nape-kwa.html
true
925270315725722404
UTF-8
Not found any posts VIEW ALL Readmore Reply Cancel reply Delete By Home PAGES POSTS View All

USIPITWE NA HIZI HAPA CHINI LABEL ARCHIVE SEARCH ALL POSTS Not found any post match with your request Back Home Sunday Monday Tuesday Wednesday Thursday Friday Saturday Sun Mon Tue Wed Thu Fri Sat January February March April May June July August September October November December Jan Feb Mar Apr May Jun Jul Aug Sep Oct Nov Dec just now 1 minute ago $$1$$ minutes ago 1 hour ago $$1$$ hours ago Yesterday $$1$$ days ago $$1$$ weeks ago more than 5 weeks ago Followers Follow THIS CONTENT IS PREMIUM Please share to unlock Copy All Code Select All Code All codes were copied to your clipboard Can not copy the codes / texts, please press [CTRL]+[C] (or CMD+C with Mac) to copy