Mamlaka ya Mapato Tanzania (TRA) mkoani Arusha imevifungia vituo 57 vya kuuza dizeli, petroli na mafuta ya taa kutokana na kutokuwa na mash...

Mamlaka ya Mapato Tanzania (TRA) mkoani Arusha imevifungia vituo 57 vya kuuza dizeli, petroli na mafuta ya taa kutokana na kutokuwa na mashine za kielektroniki za kutoa risiti (EFDs).
Akizungumza na wanahabari juu ya hatua hiyo Meneja wa Mamlaka hiyo mkoani Arusha Bwana Apili Mbaruku amesema vituo hivyo vipo katika Wilaya za Arusha mjini; Karatu; Monduli; Arumeru; Loliondo pamoja na Longido.
Ameongeza kuwa waliochelewa kufunga hizo mashine za kielektroniki za kutoa risiti (EFDs); adhabu yao ni kati ya shilingi milioni tatu na milioni nne.
Mkurugenzi wa Huduma na Elimu kwa Mlipa Kodi wa TRA Richard Kayombo amesema kwamba wanaendelea na kazi hiyo nchi nzima ili kuhakikisha sheria inatekelezwa.



