KAMANDA WA POLISI KILIMANJARO WILBROD MTAFFUNGWA JESHI la polisi mkoani Kilimanjaro, linawashikilia watu watatu raia wa Ethiopia kwa tu...
![]() |
| KAMANDA WA POLISI KILIMANJARO WILBROD MTAFFUNGWA |
Kamanda wa polisi mkoani hapa, Wilbrod Mtafungwa alisema jana kuwa watu hao walikamatwa katika kituo cha mabasi cha Bomang’ombe wilaya ya Hai wakitokea mkoani Arusha wakiwa njiani kuelekea mjini Moshi kwa ajili ya kuendelea na safari zao.
Kamanda aliwataja raia hao ambao walikutwa na hati za kusafiria zinazodaiwa kuwa ni bandia kuwa ni Bakari Mohamed (19), Khayati Ndushi (19) na Iclam Zadi (19) ambao wanaendelea kuhojiwa kwa ushirikiano wa idara ya uhamiaji na polisi ili baadaye kufikishwa mahakamani.
Watu hao walikamatwa Aprili 4 majira ya saa 5.00 usiku kutokana na msako unaoendeshwa na jeshi la polisi mkoani hapa.
Katika tukio jingine, watu wengine wawili wakazi wa kijiji cha Holili kata ya Holili wilayani Rombo wamekamatwa kwa tuhuma za kusafirisha na kuingiza bidhaa nchini kwa kutumia njia za panya bila kulipa ushuru.
Alisema Aprili 5 majira ya saa 7.00 mchana, polisi walimkamata Santolin Urio (32) akiendesha pikipiki akiwa amebeba katoni 10 za chumvi na mifuko 10 ya plastiki akitokea Kenya kuingia nchini.
Kadhalika polisi ilimkamata mkazi mwingine wa Holili, William Patrick (29), akiendesha pikipiki aina ya Skygo yenye namba KMCK 2755 akiwa amebeba makasha 10 ya dawa aina ya Medcot akitokea Kenya bila kulipia ushuru.




