http://wepesimedia.blogspot.com/p/blog-page.html

post-feature-image

Fisi waua watoto wawili na kujeruhi wengine,Arusha.


TANGAZA NASISI KWA BEI NAFUU NA UPATE MATOKEO MAZURI KATIKA BIASHARA YAKO.

Fisi wa Hifadhi ya Ngorongoro mkoani Arusha wamevamia boma la Wamasai katika kata ya Nainokanoka na kuwala watoto wawili, akiwemo wa miezi...

Mbowe na vigogo Chadema waachiwa baada ya kuhojiwa kwa saa tano
WATENDAJI 20 WA VIJIJI WAAJIRIWA HALMASHAURI YA MERU
Kumi wakamatwa mauaji diwani CHADEMA



Fisi wa Hifadhi ya Ngorongoro mkoani Arusha wamevamia boma la Wamasai katika kata ya Nainokanoka na kuwala watoto wawili, akiwemo wa miezi tisa na kujeruhi watu wengine kadhaa, watoto waliouawa wametajwa kuwa ni Akapuko Ngaruma (4) na mdogo wake Esupati Ngaruma aliyekuwa na miezi tisa tu.

Diwani wa Kata ya Nainokanoka, Edward Maura, ambaye pia ni Mwenyekiti wa Baraza la Wafugaji Ngorongoro, amethibitisha tukio hilo na kuongeza kuwa kwa mujibu wa mila za Kimasai, mabaki ya miili ya watoto hao waliouawa na fisi, yalizikwa Jumapili mchana katika eneo hilo.

Walioshuhudia tukio hilo walisema kwa nyakati kuwa ilikuwa saa 5:00 usiku, siku ya Jumamosi ya Machi 4, mwaka huu wakati fisi walipovamia nyumba hiyo inayomilikiwa na Ngaruma Parisuloi (38) katika kijiji cha Olojomenoku, Kata ya Nainokanoka, na kwenda hadi kwenye chumba walicholala watoto.

Mama yao Naitopi Ngaruma, ndiye alikuwa mtu wa kwanza kufika eneo la tukio na kukuta fisi mmoja akiwa tayari amepasua vichwa vya watoto wake na ubongo kutapakaa kitandani na sakafuni, huku mnyama huyo akiendelea kuitafuna miili yao.

Mama huyo alipiga kelele zilizomleta baba wa Boma, Ngaruma Parisuloi ambaye hadi kufika chumbani humo tayari fisi alikuwa amewaacha watoto na kuanza kumshambulia mkewe. Mnyama huyo alikuwa amemkaba yule mama shingoni akiwa amemuumiza vibaya.

Ngaruma ikabidi aanze kumshambulia fisi katika jitihada za kumnusuru mkewe lakini mnyama huyo alimvamia pia. Baba huyo naye aling’atwa mkono na kujeruhiwa vibaya, kabla majirani hawajafika kutoa msaada.

Fisi huyo aliuawa baada ya kukurupushwa kutoka ndani na kukimbilia zizini ambako pia aliishambulia mifugo na kuua ndama mmoja, mbuzi na kondoo kabla ya kuzidiwa nguvu na watu waliokusanyika bomani hapo kumshambulia.

Fisi hao pia wanadaiwa kuwajeruhi watu wengine kadhaa, wanne kati yao vibaya na ambao kwa sasa wamelazwa katika hospitali ya wilaya ya Karatu huku mipango ikiendelea ili wahamishiwe jijini Arusha kwa matibabu zaidi.

By: Emmy Mwaipopo

Chanzo: Habari Leo

Name

BIASHARA NA UCHUMI BREAKING NEWS BURUDANI ENGLISH NEWS GOSIIP GOSPEL HABARI HABARI PICHA MAGAZETI MAKALA MATUKIO MICHEZO MUSIC VIDEO WAZO LANGU
false
ltr
item
WEPESI MEDIA : Fisi waua watoto wawili na kujeruhi wengine,Arusha.
Fisi waua watoto wawili na kujeruhi wengine,Arusha.
http://www.bongo5.com/wp-content/uploads/2017/03/fisi_210_120.jpg
WEPESI MEDIA
https://wepesimedia.blogspot.com/2017/03/fisi-waua-watoto-wawili-na-kujeruhi.html
https://wepesimedia.blogspot.com/
http://wepesimedia.blogspot.com/
http://wepesimedia.blogspot.com/2017/03/fisi-waua-watoto-wawili-na-kujeruhi.html
true
925270315725722404
UTF-8
Not found any posts VIEW ALL Readmore Reply Cancel reply Delete By Home PAGES POSTS View All

USIPITWE NA HIZI HAPA CHINI LABEL ARCHIVE SEARCH ALL POSTS Not found any post match with your request Back Home Sunday Monday Tuesday Wednesday Thursday Friday Saturday Sun Mon Tue Wed Thu Fri Sat January February March April May June July August September October November December Jan Feb Mar Apr May Jun Jul Aug Sep Oct Nov Dec just now 1 minute ago $$1$$ minutes ago 1 hour ago $$1$$ hours ago Yesterday $$1$$ days ago $$1$$ weeks ago more than 5 weeks ago Followers Follow THIS CONTENT IS PREMIUM Please share to unlock Copy All Code Select All Code All codes were copied to your clipboard Can not copy the codes / texts, please press [CTRL]+[C] (or CMD+C with Mac) to copy