Watendaji 20 wa vijiji ambao walishinda usaili uliofanyika tarehe 01 na 02 Februari 2018 wamejaza fomu za Mkataba wa Ajira Serikalini...
Watendaji 20 wa vijiji ambao walishinda usaili uliofanyika
tarehe 01 na 02 Februari 2018 wamejaza fomu za Mkataba wa Ajira
Serikalini na mifuko ya hifadhi ya jamii ,hii ni baada ya kupewa semina
elekezi juu ya kanuni za maadili ya utendaji katika utumishi wa Umma na
sheria muhimu kwa uongozi wa ofisi za Kata,Serikali za Vijiji,Wenyeviti
wa Vitongoji na wenyeviti wa mitaa.
Akizungumza wakati wa semina elekezi kwa watendaji hao Mkuu
wa Idara ya Utumishi na Rasilimali watu Grace A. Mbilinyi amewahimiza
watendaji hao wa vijiji kutekeleza majukumu yao kwa kuzingatia Sheria
,Kanuni Na taratibu za Utumishi wa Umma,nukuu “mmepewa ofisi za umma
kuwatumikia wananchi na kutatua kero zao”
Aidha Semina hiyo imefanywa na Halmashauri ya Meru kupitia
idara ya Utumishi na Rasilimali watu ikiwa ni baada ya vyeti vya
watumishi hawo kuhakikiwa na Baraza la Mtihani Tanzania (NECTA) na
kuthibitika kua ni halali
Picha za tukio.
Mkuu wa Idara ya Utumishi na Rasilimali watu Grace A. Mbilinyi akizungumza na watendaji wa Vijiji.
Mmoja wa Watendaji wa Vijiji waliajiriwa akiuliza swali ili kupata uelewa zaidi
Watendaji wa Vijiji walioajiriwa wakifuatilia kwa makini semina elekezi.
Watendaji wa Vijiji walioajiriwa wakifuatilia kwa makini semina elekezi.

Watendaji wa Vijiji walioajiriwa wakifuatilia kwa makini wakati wa seminaCREDITY NGILISHONEWS



