http://wepesimedia.blogspot.com/p/blog-page.html

post-feature-image

Mbowe na vigogo Chadema waachiwa baada ya kuhojiwa kwa saa tano


TANGAZA NASISI KWA BEI NAFUU NA UPATE MATOKEO MAZURI KATIKA BIASHARA YAKO.

Mwenyekiti wa Chadema, Freeman Mbowe na viongozi wengine wachama hicho wameachiwa kwa dhamana baada ya kuhojiwa Kituo Kikuu cha Polisi ...

Kiongozi wa upinzani amfuata Magufuli
KILIMANJARO. Mchungaji ashikiliwa na polisi kwa uchochezi wa kisiasa
RAIS JACOB ZUMA KUSHTAKIWA KWA MAKOSA 18 YA RUSHWA
Mwenyekiti wa Chadema, Freeman Mbowe na viongozi wengine wachama hicho wameachiwa kwa dhamana baada ya kuhojiwa Kituo Kikuu cha Polisi tangu saa 6:50 mchana

Viongozi hao walifika kituoni hapo leo Jumanne Februari 27, 2018 na kuachiwa saa 1:02 usiku, kuitikia wito wa polisi.

Walikwenda kituoni hapo baada ya Mbowe kumaliza mkutano wake na waandishi wa habari makao makuu ya chama hicho yaliyopo mtaa wa Ufipa, Kinondoni.

Mmoja wa mawakili wa viongozi hao, Frederick Kihwelo amesema kuwa wote wameachiwa kwa dhamana kwa kutakiwa kuwa na mdhamini mmoja na kutakiwa kuripoti tena kituoni hapo Machi 5, 2018 saa 1 asubuhi.

Amesema viongozi hao walianza kuhojiwa saa 8:30 mchana, baada ya kufanya mazungumzo ya tuhuma zinazowakabili.

Februari 20, 2018 Polisi Kanda Maalum ya Dar es Salaam iliagiza kukamatwa viongozi saba waandamizi wa Chadema akiwamo Mbowe.

Wito huo ulikuja siku chache baada ya tukio la kuuawa kwa mwanafunzi wa Chuo cha Taifa cha Usafirishaji (NIT), Akwilina Akwilini.

Akwilina aliuawa kwa kupigwa risasi akiwa ndani ya daladala eneo la Mkwajuni, Kinondoni jijini Dar es Salaam wakati polisi wakiwatawanya wafuasi wa Chadema waliokuwa wakienda ofisi za mkurugenzi wa Halmashauri ya Kinondoni kudai viapo kwa mawakala wao.

Viongozi wengine waliohojiwa sambamba na Mbowe ni  naibu makatibu wakuu, John Mnyika (Bara) na Salum Mwalimu (Zanzibar).

Pia, wamo mwenyekiti wa Baraza la Wanawake Chadema (Bawacha), Halima Mdee; mwenyekiti wa Kanda ya Serengeti, John Heche na Esther Matiko ambaye ni mweka hazina wa Bawacha.

Mdee, Matiko, Heche na Mnyika walisharipoti awali na walitakiwa kurejea kituoni leo. Viongozi wengine waliwakilishwa na wanasheria.

Katibu Mkuu wa chama hicho, Dk Vicent Mashinji  hakwenda polisi kwa kuwa yupo nje ya nchi.

Name

BIASHARA NA UCHUMI BREAKING NEWS BURUDANI ENGLISH NEWS GOSIIP GOSPEL HABARI HABARI PICHA MAGAZETI MAKALA MATUKIO MICHEZO MUSIC VIDEO WAZO LANGU
false
ltr
item
WEPESI MEDIA : Mbowe na vigogo Chadema waachiwa baada ya kuhojiwa kwa saa tano
Mbowe na vigogo Chadema waachiwa baada ya kuhojiwa kwa saa tano
https://blogger.googleusercontent.com/img/b/R29vZ2xl/AVvXsEjDDWhRdHlpt8WfvlXZSxtLUJ9bB009owJ6PHRpiFiZPAM5NsddWHvmRn4wouoZFHJJFtyR51mmre7qeHfXWMTeQzQshYb0k1hwOG66I4xHG2bwwdkVIoiLnQ05kcqchc98cKIFikfJzlk/s640/1.jpg
https://blogger.googleusercontent.com/img/b/R29vZ2xl/AVvXsEjDDWhRdHlpt8WfvlXZSxtLUJ9bB009owJ6PHRpiFiZPAM5NsddWHvmRn4wouoZFHJJFtyR51mmre7qeHfXWMTeQzQshYb0k1hwOG66I4xHG2bwwdkVIoiLnQ05kcqchc98cKIFikfJzlk/s72-c/1.jpg
WEPESI MEDIA
https://wepesimedia.blogspot.com/2018/02/mbowe-na-vigogo-chadema-waachiwa-baada.html
https://wepesimedia.blogspot.com/
http://wepesimedia.blogspot.com/
http://wepesimedia.blogspot.com/2018/02/mbowe-na-vigogo-chadema-waachiwa-baada.html
true
925270315725722404
UTF-8
Not found any posts VIEW ALL Readmore Reply Cancel reply Delete By Home PAGES POSTS View All

USIPITWE NA HIZI HAPA CHINI LABEL ARCHIVE SEARCH ALL POSTS Not found any post match with your request Back Home Sunday Monday Tuesday Wednesday Thursday Friday Saturday Sun Mon Tue Wed Thu Fri Sat January February March April May June July August September October November December Jan Feb Mar Apr May Jun Jul Aug Sep Oct Nov Dec just now 1 minute ago $$1$$ minutes ago 1 hour ago $$1$$ hours ago Yesterday $$1$$ days ago $$1$$ weeks ago more than 5 weeks ago Followers Follow THIS CONTENT IS PREMIUM Please share to unlock Copy All Code Select All Code All codes were copied to your clipboard Can not copy the codes / texts, please press [CTRL]+[C] (or CMD+C with Mac) to copy