http://wepesimedia.blogspot.com/p/blog-page.html

post-feature-image

Bahati Bukuku-Mimi ndoa ilinishinda


TANGAZA NASISI KWA BEI NAFUU NA UPATE MATOKEO MAZURI KATIKA BIASHARA YAKO.

Mwanamuziki mkongwe wa nyimbo za Injili Bahati Bukuku amefunguka na kuweka wazi kuwa ndoa ilimshinda na kusema katika harakati za maisha y...

Video,Petit Money na Esma Platnumz warudiana kwa kishindo kikubwa.
Mr Touch na Nay Wa Mitego wazungumzia ugomvi wao, sababu ni nini haswa.
Hii video mpya ya Wale ‘My PYT’ Itazame hapa.

Mwanamuziki mkongwe wa nyimbo za Injili Bahati Bukuku amefunguka na kuweka wazi kuwa ndoa ilimshinda na kusema katika harakati za maisha yeye alipishana na aliyekuwa mume wake kufikia hatua ya kutengana na sasa kila mmoja kuishi kivyake.


Bahati Bukuku akizungumza kwenye cha Kikaangoni alisema wimbo wake wa 'Dunia haina huruma' si kama alimwimbia huyo aliyekuwa mume wake bali anakiri kuwa ni kisa cha kweli kilichotokea lakini hayo mambo aliyekuwa mumewe alikuwa hayafanyi.

"Aliyewahi kuwa mume wangu hakufanya hilo tukio ila kile kisa ni kweli kilitokea sehemu, lakini aliyekuwa mume wangu hakuwa na matatizo haya, ila tu katika harakati zetu za maisha kuna kupishana hivyo nilipishana naye tu. Siwezi kuongea uongo kwa mtu aliyekuwa mume wangu, hata nikiandika kitabu siwezi kuruka hili popote nikisimama nitasema niliolewa ndoa ikanishinda" alisema Bahati Bukuku

Kuhusu skendo kuwa ndoa nyingi za "watu wa dini" hazidumu, Bahati amesema wanaume wengi wanakosea kufikiri kuwa wakioa wanawake ambao ni watu wa dini au watu wa injili kama yeye, wanakuwa wameoa watu wasio na makosa..

"Wengi hudhani ukioa mtu wa kanisani umeoa malaika ambaye hakosei, sasa wakishaanza maisha anakuta tofauti, hapo ndipo ndoa inaweza kuvunjika, jama hata sisi ni binadamu pia" Alisema Bahati

Baadhi ya mashabiki walitaka kujua endapo alipata watoto katika ndoa hiyo, ambapo Bahati alikataa kuongea chochote kuhusu yeye kuwa na watot au la, na kusema kuwa hayuko tayari kuongea chochote huku akisema kuwa ana watoto wengi

"Hili swala la watoto sitaki kuzungumzia, mimi nina watoto wengi tu, kwahiyo kwenye ndoa yangu nisingependa kuongelea swala la watoto" alisema Bahati

Mbali na hilo Bahati Bukuku anasema watu ambao walimzushia kifo ni watu wake wa karibu ambao anafanya nao kazi na huenda walifanya hivyo ili kutaka kumpunguzia mashabiki wake.

"Walionizushia kifo ni watu ambao nafanya nao kazi, walidhani watanipunguzia mashabiki lakini pia ni kazi ya shetani hiyo, hivyo walijifanya ile taarifa imeanzia Congo lakini ni wa hapahapa ila mamlaka za mawasiliano bado zinaendelea kufuatilia ingawa mpaka sasa tayari wameshafahamika" alisema Bahati Bukuku

Katika hatua nyingine, Bahati amesema hivi sasa anaandaa movie ambayo pia itakuwa na lengo la kuinjilisha, na kufikisha ujumbe wa Mungu kama ambavyo amekuwa akifanya kwenye uimbaji. "Kwanza kabla sijatoa wimbo mpya, natoa filamu yangu mpya inayoitwa 'Mwalimu wa Ndoa', ambayo baada ya wiki moja itakuwa madukani, niliipeleka BASATA, tayari wameshaipitia, ina mafundisho mengi mazuri kuhusu ndoa, nawashauri wanawake, mabinti wote waitafute" Amesema Bahati huku akisita kutaja mastaa walioshiriki katika movie hiyo

Credity East Africa Televition

Name

BIASHARA NA UCHUMI BREAKING NEWS BURUDANI ENGLISH NEWS GOSIIP GOSPEL HABARI HABARI PICHA MAGAZETI MAKALA MATUKIO MICHEZO MUSIC VIDEO WAZO LANGU
false
ltr
item
WEPESI MEDIA : Bahati Bukuku-Mimi ndoa ilinishinda
Bahati Bukuku-Mimi ndoa ilinishinda
https://blogger.googleusercontent.com/img/b/R29vZ2xl/AVvXsEgOzG0_2axpBjiKSKXAZebv5OJ9tZcrR7owWVSd42Tf7N1zhlUSLhWnjGSAF0OnkD_bCBwXYf39cvbNnZqaEXpoen0VZNLk_Ht6c5oSeLYZN4qFScit7KlT_yL4Yt7_tQXfDrYmrGIMJ4Qi/s640/61yH1BJRStL._SL500_AA280_.jpg
https://blogger.googleusercontent.com/img/b/R29vZ2xl/AVvXsEgOzG0_2axpBjiKSKXAZebv5OJ9tZcrR7owWVSd42Tf7N1zhlUSLhWnjGSAF0OnkD_bCBwXYf39cvbNnZqaEXpoen0VZNLk_Ht6c5oSeLYZN4qFScit7KlT_yL4Yt7_tQXfDrYmrGIMJ4Qi/s72-c/61yH1BJRStL._SL500_AA280_.jpg
WEPESI MEDIA
https://wepesimedia.blogspot.com/2017/01/bahati-bukuku-mimi-ndoa-ilinishinda.html
https://wepesimedia.blogspot.com/
http://wepesimedia.blogspot.com/
http://wepesimedia.blogspot.com/2017/01/bahati-bukuku-mimi-ndoa-ilinishinda.html
true
925270315725722404
UTF-8
Not found any posts VIEW ALL Readmore Reply Cancel reply Delete By Home PAGES POSTS View All

USIPITWE NA HIZI HAPA CHINI LABEL ARCHIVE SEARCH ALL POSTS Not found any post match with your request Back Home Sunday Monday Tuesday Wednesday Thursday Friday Saturday Sun Mon Tue Wed Thu Fri Sat January February March April May June July August September October November December Jan Feb Mar Apr May Jun Jul Aug Sep Oct Nov Dec just now 1 minute ago $$1$$ minutes ago 1 hour ago $$1$$ hours ago Yesterday $$1$$ days ago $$1$$ weeks ago more than 5 weeks ago Followers Follow THIS CONTENT IS PREMIUM Please share to unlock Copy All Code Select All Code All codes were copied to your clipboard Can not copy the codes / texts, please press [CTRL]+[C] (or CMD+C with Mac) to copy