http://wepesimedia.blogspot.com/p/blog-page.html

post-feature-image

RIDHIWANI ASAIDIA MAGODORO 50 MORETO BAADA YA BWENI KUUNGUA


TANGAZA NASISI KWA BEI NAFUU NA UPATE MATOKEO MAZURI KATIKA BIASHARA YAKO.

BWENI la wanafunzi wasichana katika shule ya sekondari ya Moreto iliyopo tarafa ya Msoga wilaya ya Bagamoyo mkoani Pwani, baada ya kuungua ...

Waziri Ummy apiga marufuku mikopo midogo 'NI UPUUZI'
Uchaguzi wa TLS: Lissu apendekezwa kutetea Urais wake, ajengewa hoja mbili
Diamond Amuhakikishia mama yake kufunga ndoa mwaka huu.



BWENI la wanafunzi wasichana katika shule ya sekondari ya Moreto iliyopo tarafa ya Msoga wilaya ya Bagamoyo mkoani Pwani, baada ya kuungua kwa moto na kusababisha mali zote za wanafunzi hao kuteketea kwa moto. (Picha na Mwamvua Mwinyi)

Na Mwamvua Mwinyi, Bagamoyo

MBUNGE wa jimbo la Chalinze, mkoani Pwani, Ridhiwani Kikwete, ametoa magodoro 50, yenye thamani ya sh.mil 2.225 kwa wanafunzi wa kike wa shule ya sekondari Moreto, waliounguliwa na bweni lao na kusababisha mali zote kuteketea kwa moto.

Wanafunzi hao wapatao196, katika shule hiyo iliyopo kata ya Lugoba tarafa ya Msoga, wilaya ya Bagamoyo, wamenusurika kifo baada ya bweni hilo kuteketea kwa moto siku ya october 5.

Moto huo umeteketeza mali zote zilizokuwemo ambazo hadi sasa hazijajulikana thamani yake.

Kufuatia kutokea kwa tukio hilo, Ridhiwani alifika shuleni hapo kutembelea na kutoa pole kwa kutokea janga hilo.

Alisema wakumshukuru ni mungu kwani pamoja na kutokea kwa hasara ya kuteketea kwa mali lakini hakuna madhara kwa wanafunzi yaliyotokea.

Ridhiwani aliwapa pole walimu na wanafunzi kijumla na kuwaomba wadau wengine kujitokeza kwenda kusaidia pale watakapojaaliwa.

Kwa mujibu wa mwalimu mkuu wa shule ya sekondari Moreto, Justine Lyamuya alielezea kuwa, tukio hilo limetokea October 5,majira ya asubuhi ambapo walianza kuona moshi mzito katika bweni mojawapo wanaloishi wasichana wa shule hiyo.

Alisema wakati moto huo unazuka wanafunzi hao walikuwa kwenye masomo yao darasani.

“Tulifuatilia na kukuta moto umeshashika kwenye bweni hilo na jitihada za kuuzima zilishindikana”alisema mwalimu Lyamuya.

Lyamuya alisema mali zote za wanafunzi wanaolala kwenye bweni hilo zimeteketea kwa moto hivyo kwa sasa wanafanya tathmini kujua gharama zilizopotea.

Katika hatua nyingine jeshi la polisi mkoani Pwani linafanya uchunguzi wa tukio hilo ili kubaini chanzo cha moto.

Kamanda wa polisi mkoani Pwani, Boniventure Mushongi, alielezea kuwa mazingira ya jengo hilo ni yenye kutumia nishati ya solar power hivyo ni lazima kufanya uchunguzi wa kina kujua kiini cha kuzuka kwa moto huo.

Alisema bweni hilo linakadiriwa kuwa na wanafunzi 196.

Kamanda Mushongi alisema thamani za mali za wanafunzi katika moto huo bado hazijafahamika.

Name

BIASHARA NA UCHUMI BREAKING NEWS BURUDANI ENGLISH NEWS GOSIIP GOSPEL HABARI HABARI PICHA MAGAZETI MAKALA MATUKIO MICHEZO MUSIC VIDEO WAZO LANGU
false
ltr
item
WEPESI MEDIA : RIDHIWANI ASAIDIA MAGODORO 50 MORETO BAADA YA BWENI KUUNGUA
RIDHIWANI ASAIDIA MAGODORO 50 MORETO BAADA YA BWENI KUUNGUA
http://fullshangweblog.com/home/wp-content/uploads/2016/10/more.jpg
WEPESI MEDIA
https://wepesimedia.blogspot.com/2016/10/ridhiwani-asaidia-magodoro-50-moreto.html
https://wepesimedia.blogspot.com/
http://wepesimedia.blogspot.com/
http://wepesimedia.blogspot.com/2016/10/ridhiwani-asaidia-magodoro-50-moreto.html
true
925270315725722404
UTF-8
Not found any posts VIEW ALL Readmore Reply Cancel reply Delete By Home PAGES POSTS View All

USIPITWE NA HIZI HAPA CHINI LABEL ARCHIVE SEARCH ALL POSTS Not found any post match with your request Back Home Sunday Monday Tuesday Wednesday Thursday Friday Saturday Sun Mon Tue Wed Thu Fri Sat January February March April May June July August September October November December Jan Feb Mar Apr May Jun Jul Aug Sep Oct Nov Dec just now 1 minute ago $$1$$ minutes ago 1 hour ago $$1$$ hours ago Yesterday $$1$$ days ago $$1$$ weeks ago more than 5 weeks ago Followers Follow THIS CONTENT IS PREMIUM Please share to unlock Copy All Code Select All Code All codes were copied to your clipboard Can not copy the codes / texts, please press [CTRL]+[C] (or CMD+C with Mac) to copy