http://wepesimedia.blogspot.com/p/blog-page.html

post-feature-image

MBUNGE COSATO CHUMI AANZA KUTATUA TATIZO LA MAJI KWENYE SHULE ZA JIMBO LA MAFINGA MJINI


TANGAZA NASISI KWA BEI NAFUU NA UPATE MATOKEO MAZURI KATIKA BIASHARA YAKO.

Bw Donsun Lee ambaye ni Mkurugenzi wa NGO ya Kutoka Korea ya Serving Friends International akikagua pump kwenye moja ya kisima kwenye sh...

Ahadi tisa za Makonda 2016 alizofungia ‘kabatini’
Muungano wa Madaktari wa Kenya (KMPDU), wawakataa Madaktari wa Tanzania
Dk Shein hakuna wa kumuondoa madarakani

Bw Donsun Lee ambaye ni Mkurugenzi wa NGO ya Kutoka Korea ya Serving Friends International akikagua pump kwenye moja ya kisima kwenye shule ya Msingi Makalala, anayetizama ni Mbunge wa Mafinga Mjini Cosato Chumi

Bw Donsun Lee ambaye ni Mkurugenzi wa NGO ya Kutoka Korea ya Serving Friends International akimsikiliza
kwa makini Mhandisi wa Maji wa Mji wa Mafinga Eng Eradius.

Pichani baadhi ya wanafunzi na waalimu wa shule ya Msingi Makalala wakiwa katika picha ya pamoja na Mrs Lee na Mbunge wa Mafinga Mjini Cosato Chumi.
………………………………………….

na fredy mgunda,iringa

MBUNGE wa jimbo Mafinga mjini Cosato Chumi ameendeleza juhudi zake za kuwatafutia maendeleo wananchi wa jimbo lake kwa kufanya kazi kwa ukaribu na taasisi za kiserikali na zisizo za kiserikali za nje ya nchi ya Tanzania pamoja na taasisi za ndani.


Hivi karibu balozi wa korea nchini Tanzania Bw Song Geum Young akiwa na NGO ya Kutoka Korea ya World share alitembelea jimbo la mafinga mjini kwa lengo la kujionea changamoto za jimbo hilo na kutafuta njia za kutoa msaada wa kutatua baadhi ya changamoto hizo na walitoa msaada wa taa ndogo za solar kwa kaya masiki mia saba.


Baada ya balozi huyo kurudi jijini Dar es Salaam alimuagiza Mkurugenzi wa NGO ya Kutoka Korea ya Serving
Friends International Bw Donsun Lee kutembelea jimbo la mafinga mjini na kuzifanyia tafiti kwa kina baadhi ya changamoto za jimbo hilo ambazo alikuwa amezianisha hapo awali ili kuweza kusaidia kuzitatua.
Aidha mkurugenzi wa NGO ya Kutoka Korea ya Serving Friends International Bw Donsun Lee
alifanikiwa kutembelea baadhi ya shule za jimbo la mafinga mjini na kuzifanyia tafiti changamoto zilizopo kama uhaba wa maji na kuahidi kuzitatua kwa kuwa ameshazifanyia utafiti.

“Leo nimetembelea Shule za Msingi Makalala, Mkombwe, Ndolezi na Mwongozo na Shule ya Sekondari Luganga na nimejionea shidaya upatikanaji wa maji hivyo kwa kuwa NGO yetu inajihusisha
na uchimbaji wa visima hivyo tumewasilisha taarifa hizi makao makuu ya ofisi zetu na tunasubili majibu”alisema Bw Donsun Lee.

Bw Donsun Lee alimpongeza mbunge wa jimbo mafinga mjini Cosato Chumi kwa juhudi alizozifanya za
kuwashawishi kutembelea jimbo hilo na kujionea baadhi ya changamoto ambazo wanaweza kuzitatua kwa kushiriana na mbunge huyo.

Katika ziara hiyo Bw Lee na timu yake walitembelea Shule za Msingi Makalala, Mkombwe, Ndolezi na Mwongozo
na Shule ya Sekondari Luganga.
Aidha baada ya tafiti hizo, Bw Lee atawasilisha taarifa zake Makao Makuu ya NGO ya Serving Friends
International huko Seoul, Korea.
Nia ya kufanya tafiti hizo ni kuiweka Katika Mipango Halmashauri ya Mji wa Mafinga kwa sababu ndo
utaratibu wa NGO hiyo ambayo kwa Sasa wanachimba visima mkoani Singida
Kwa upande wake mbunge wa jimbo la mafinga Cosato Chumi amemshukuru Mkurugenzi wa NGO ya Kutoka Korea ya Serving Friends International Bw Donsun Lee kwa kufanikisha kufanya tafiti ambazo amejine mwenye na kuleta matumaini kwa wananchi wa jimbo hilo la kutatuliwa tatizo la maji kwa kuchimbiwa visima na taasisi hiyo.


Chumi ameongeza kuwa haya ni matokeo ya ziara ya Balozi wa Korea ambaye alitembelea jimbo la Mafinga Mwezi
mmoja uliopita na kujionea changamoto hizo.

Lakini mbunge Chumi amewataka wananchi wa jimbo la mafinga kufanya kazi kwa kujituma na kuunganisha
na nguvu za mbunge wao ili kupata maendeleo kwa kasi inayotakiwa.


“Unakuta mbunge nahangaika kuwaletea maendeleo wananchi wangu kama hivi mnavyoona lakini ukienda vijiweni unakuta wananchi wanacheza bao,pooltable na wengi wanapiga soga zisizo na
malengo,wakati wangeutumia muda huo kufanya kazi jimbo la mafinga mjini
litakuwa na maendeleo ya kasi sio muda”.alisema Chumi

Name

BIASHARA NA UCHUMI BREAKING NEWS BURUDANI ENGLISH NEWS GOSIIP GOSPEL HABARI HABARI PICHA MAGAZETI MAKALA MATUKIO MICHEZO MUSIC VIDEO WAZO LANGU
false
ltr
item
WEPESI MEDIA : MBUNGE COSATO CHUMI AANZA KUTATUA TATIZO LA MAJI KWENYE SHULE ZA JIMBO LA MAFINGA MJINI
MBUNGE COSATO CHUMI AANZA KUTATUA TATIZO LA MAJI KWENYE SHULE ZA JIMBO LA MAFINGA MJINI
https://blogger.googleusercontent.com/img/b/R29vZ2xl/AVvXsEhnh1bvr9uDLyWTJLDfoGLSK40UvaBHTze_mNw05VPc7Lpi8kZGPJrt0abiZUqu7U1Eq7Zflc4x_qwbJZcjjNnCfe8xj8y_Eks2h60MlEea5r6JCQ31dgJXKRTxb3l6LHzb52X1ViMN-F8m/s640/IMG-20160907-WA0132.jpg
https://blogger.googleusercontent.com/img/b/R29vZ2xl/AVvXsEhnh1bvr9uDLyWTJLDfoGLSK40UvaBHTze_mNw05VPc7Lpi8kZGPJrt0abiZUqu7U1Eq7Zflc4x_qwbJZcjjNnCfe8xj8y_Eks2h60MlEea5r6JCQ31dgJXKRTxb3l6LHzb52X1ViMN-F8m/s72-c/IMG-20160907-WA0132.jpg
WEPESI MEDIA
https://wepesimedia.blogspot.com/2016/09/mbunge-cosato-chumi-aanza-kutatua.html
https://wepesimedia.blogspot.com/
http://wepesimedia.blogspot.com/
http://wepesimedia.blogspot.com/2016/09/mbunge-cosato-chumi-aanza-kutatua.html
true
925270315725722404
UTF-8
Not found any posts VIEW ALL Readmore Reply Cancel reply Delete By Home PAGES POSTS View All

USIPITWE NA HIZI HAPA CHINI LABEL ARCHIVE SEARCH ALL POSTS Not found any post match with your request Back Home Sunday Monday Tuesday Wednesday Thursday Friday Saturday Sun Mon Tue Wed Thu Fri Sat January February March April May June July August September October November December Jan Feb Mar Apr May Jun Jul Aug Sep Oct Nov Dec just now 1 minute ago $$1$$ minutes ago 1 hour ago $$1$$ hours ago Yesterday $$1$$ days ago $$1$$ weeks ago more than 5 weeks ago Followers Follow THIS CONTENT IS PREMIUM Please share to unlock Copy All Code Select All Code All codes were copied to your clipboard Can not copy the codes / texts, please press [CTRL]+[C] (or CMD+C with Mac) to copy